Memento
JF-Expert Member
- Jun 13, 2021
- 4,423
- 9,962
Upinzani kwenye serikali yoyote ile ni lazima uwepo ili kuharakisha Maendeleo, achana na yale maneno eti upinzani ulituchelewesha.
Miaka yote CCM wanatawala wao ila hakuna jipya zaidi ya kutubadilishia tu nyimbo.
Alianza JK na Kasi mpya, ari mpya ila mwisho wa siku hakuna lolote lile, ni umasikini mwanzo mwisho kwa watanzania.
Akaja Magufuli na kauli mbiu yake ya Tanzania ya viwanda ila nao hakuna lolote lile zaidi ya porojo tu.
Sasa hivi tupo na mama, yeye anakuambia kazi iendelee. Iendelee wapi? Maneno laini, matamu ila hakuna lolote lile ni yaleyale tu.
Ni wakati muafaka sasa wa CCM kukaa pembeni ,mpishe na wengine. CCM hamjazaliwa kutawala nyie tu Tanzania.
Kwani mkiachia upinzani nao tukapata hata miaka mitano shida ipo wapi? Hapa nazungumzia upinzani Chadema na sio wale wengine wasaka tonge na uteuzi. Chama Cha upinzani makini nchi hii ni chadema tu. Huo ndio ukweli.
Nawaomba wale wote ambao tunasupport upinzani kwa hali na mali tuungane na tushikamane zaidi kuangusha hawa CCM. Hii kazi sio rahisi ila Mimi ninaona ni muda muafaka na adhimu kuwaangusha sasa, tusichoke, tusikate tamaa, wataanguka tu inahitajika nguvu kidogo sana.
Tusitarajie lolote chini ya CCM hii na yoyote itayokuja.
Hebu fikiria chama kimejaza watu wanaowaza uteuzi tu, alafu ndio hawa wanataka kuendelea kutawala. HAPANA CCM juenj kuwa siku zenu si nyingi mtaanguka.