Huu ni uzembe,ukatili au ni dharua ya wakunga wetu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huu ni uzembe,ukatili au ni dharua ya wakunga wetu?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kigarama, Oct 30, 2012.

 1. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mwezi mmoja uliopita binti mmoja (jina lake silitaji) alikwenda kujifungua kwenye Hospitali moja ya Umma na kufanikiwa kupata mtoto wa kiume. Tangu baada ya mtoto yule kuzaliwa muda mwingi wa kuwa macho aliutumia kulia tena akionyesha maumivu makali sana. Jitihada za madaktari na wazazi wake kutafuta tiba kwa kilichokuwa kinamsumbua mtoto yule ilishindikana.

  Kwa bahati kuna daktari akashauri yule mtoto apigwe X-rays (Ingawa si vizuri) ili kuona ni kitu gani hasa kinamsumbua na kweli ilisaidia kugundua kwamba yule mtoto kinachomsumbua ni kuvunjika kwa mguu wake wa kulia. Ndipo mama wa yule mama mzazi akakumbuka kwamba wakati anajifungua aliona Mkunga aliyekuwa anamzalisha kama amepigwa na butwaa na kuinama kama anaokota kitu.

  Nadharia hiyo ilimfikisha Daktari afikie kwenye hitimisho la kuamini kwamba kuvunjika kwa mguu wa mtoto yule kumesababishwa na mkunga kumwangusha wakati anazaliwa. Kama nadharia ya yule mama ni ya kweli na hitimisho la Daktari ni sahihi ni kwa nini yule mkunga hakumwambia mama mzazi kama kamwangusha mtoto wake?
   
 2. M

  Mundu JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,720
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  ...Kuna wimbo mmoja wa densi ulikuwa na kipande cha maneno haya "...nilijitahidi bila kujali wala kufikiri, kwamba kuna baadhi ya binadamu wana roho mbaya..."

  Tena wengine wanaita roho ya kijicho...Inaumiza kwakweli...
   
Loading...