HUU NI UUWAJI WA WAZI: Kuna uhalali gani wa ccm kuendelea kuwepo madarakani

PISTO LERO

JF-Expert Member
Mar 8, 2011
2,819
1,454
Wakati mjumbe mmoja wa bunge la katiba akitia kibindoni shilingi laki tatu ( 300,000) kwa siku,namaanisha (kwasiku moja) tena anachagua mwenyewe aupokeaje. Kwa mezi,siku au........

Huwezi amini mwalimu ameendelea kusotea mshahara wa shilingi laki moja na elfu themanini (180,000)kwa mwezi,tena anaupata kwa mafungu,na anapangiwa lini apate,wengine wanamiezi mitatu hawajaona mshahara wao

Akiuliza kwanini anaambiwa serikali haina fedha za kutosha kuwalipa.

Huu ni unyanyasaji na uuwaji wa waziwazi.
 
Si wakatae kazi hadi mwisho, sio mgomo uchwara, kama 180,ooo haiwatoshi na wengine wanapiga 9,000,000 kwa mwezi harafu wako kazini si wajinga hao au?
 
Ujinga wao hapo ilitakiwa bonge la mgomo wakae pale viwanja vya karimjee mwezi mzima tuone kama wasingepandishiwa mshahara
 
Ndugu yangu waache walimu wajinyanyase wenyewe. Maana kikwete alishawaambia waziwazi kuwa hata wasipomchagua kura zao hazitapunguza kitu lakini wao ndio wa kwanza kuing'ang'ani ccm na hasa walimu wakuu wanajipendekeza mno utadhani wanalipwa mishahara miwili. tena wanawashawishi walimu wenzao kuwa watiifu kwa ccm kwa kuwatishia kuwa watafukuzwa kazi ama kusitishiwa mishahara yao. Na tazizo ni kuwa hata viongozi wa chama cha walimu ni walimu walewale waajiriwa wa serikali na wao pia wanaogopa kufukuzwa kazi endapo watamtetea mwalimu yeyote atakaegoma kuisujudia ccm. WAACHENI WALIMU WAJINYONGE WENYEWE KWA WOGA WAO. HAKUNA KIUMBE DHAIFU KITAKACHOUPATA UZIMA WA MILELE.
 
siku watakapoacha kutumiwa na serikali kwenye matukio kama wanasesere watadai haki zao.
 
English men say that: Do not argue with a fool because people wont notice the difference. Achana na walimu peleka stress zako kwingne!
 
You are the most hopeless man in this nation to make teacherz your less respectable people somethng should be done unto you
 
Mwanzoni nlikua nalalamika sana kwa nini walimu wanaonewa ila wakati nlivoanza kusema UDSM ndo nkapata akili kua walimu hawaonewi ila wanajionea wenyewe na sisi tunaolalamika ni kama kumpigia mbuzi gitaa mana wenyewe wameridhika na huu mshahara na ndo mana unaona walalamikaji ni sisi watu wa kawaida na walimu wanatuangalia tu.
Wakati nipo UDSM nlikua naamini mambo meng yanaweza kufanikishwa kwa njia ya maongezi ila baadae ndo nkajua kua ukitaka kufanikisha jambo kwa nchi hii ni better utumie njia ya mgomo na kweli ilifanya kazi sana na hata COET wakafanikiwa kua katika mkopo yan all COET students.Walimu migomo yao ni ya kutongozana yan unawaka leo na kesho unatulia yan hauna nguvu yoyote na hauna nguvu kwa sababu wagomaji wanabeep na hawako serious.Mkuu wa chama cha walimu kawekwa na CCM, na sioni kama wana njia yoyote ya kumuondoa mana wameridhika nae na yeye ndo anatishia kua tutagoma na akipozwa na serikali mambo yanaisha.Kulikuapo na mtu anaitwa Pasience Mlowe ambae aliwekwa uraisi wa DARUSO na watu wachache ila solidarity ya wanachuo ndio ikamtoa.
Napenda kusisitiza kua tusiwatetee walimu mana wameridhika na hali walionayo
 
Ila na ninyi walimu ndio mnajikaanga kwa mafuta yenu, mnavyojipendekeza kwa CCM. Na bado cha moto mtakiona.
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom