Huu ni Utumwa na Sio Utumishi wa Umma: Rais Magufuli awaita Mainjinia Vilaza, Wapumbavu

Wewe nawe ni mpumbavu kama hujijui, hivyo project plan iliyosema study hivyo itafanyika miezi 6 ameandika yeye? Hiyo imeandikwa wizarani na inatekelezwa na walio shinda tenda huko wizarani. Mhandisi wa wilaya ni msimamizi tuu wa huku site iweje yeye aambulie matusi kwa mambo yaliyo pangwa wizarani?
Kama kitu hujaelewa ni bora kukaa kimya au kuuliza sio unaweka hoja ya kijinga yenye dharau.

Uko sahihi kabisa ndugu....

Mimi nadhani tukubaliane tu kuwa Mr President in this context is absolutely wrong.....!!

Na kusema kuwa Rais anakosea anapodhalilisha na kutukana wafanyakazi hawa hadharani ktk namna ya kuutweza utu wao, haina maana kuwa tunakubaliana na uzembe huo....

Tatizo hapa ninaloliona mimi, ni Rais Magufuli kutumia nguvu nyingi pasipo akili na maarifa kutatua matatizo yaliyokwisha kuota mizizi ktk Taifa hili kwa miaka takribani 67 tangu tupate Uhuru....

Mbaya zaidi ni kuwa utatuzi huo anaoufanya ni wa muda tu na kamwe siyo sustainable na hataacha legacy yoyote....

Utatuzi wa matatizo haya ni kufanya mabadiliko makubwa ya KIKATIBA na KISHERIA (Legal & constitutional reforms) ili kuboresha utendaji wenye ufanisi ktk utumishi wa umma....

Kwa hili, Rais anafanya makosa na makosa haya yata - backfire tu lazima na kamwe hayawezi kumwacha salama unless atubu mapema before it's too late....
 


View attachment 1235717

Hakika kama umesoma kwa juhudi zako kisha mambo ya kitaalamu yaliyo anzia kupangwa kutokea wizarani hadi kufika katika Halmashauri yakiwa na period plan na wewe ni mhandisi mtekelezaji, basi matusi ya aina hii hadharani utakuwa sio utumishi wa umma bali ni UTUMWA.

Mhe. Rais anaona raha sana kushangiliwa na umati wa watu wasio elewa utaalam akimtukana matusi ya udhalilishaji mtumishi wa umma.

Kitendo alichokitenda kimeonyesha kumkwaza hawa Waziri wa maji Prof. Mbarawa.
Haya ndio matokeo ya miradi kuwa kiwango cha chini kama Hostel za UDSM na Terminal 3.

Hakika nyie watumishi wa umma ni wakati wa kujitathmini, kwani Leo kwa mwenzako kesho kwako wakati 2020 mnaweza kusitisha ajira ya huyo anaye watukana mbele ya hadhara.

Mnangoja nini kuchukua maamuzi?

Mtukufu raisi amesema "Ndani ya utawala wangu......" Yeye siyo kiongozi bali mtawala. Angekuwa kiongozi asingetukana.
 
Kuna mtu mmoja naona hapa bado hajafika anaitwa Jidulamambasi, hii issue inamhusu.
 
Ukweli mchungu watu walizoea lugha za kubembelezana bembelezana. Hivi kweli upembuzi wa kachujio kamoja kanachukua muda mrefu hivo? Sasa huo ujenzi utachukua muda gani? Watu waache mazoea watumie taaluma zao vizuri kwa bidii na uaminifu mkubwa. Viongozi wengine waamke nao , unakuta mkuu wa idara, ded, Dc hawana takwimu hata za miradi yao tu katika wilaya.
Mkuu kuna walakini mkubwa wa watendaji wa serikali,walizoea kubebwa.
Kama wanataka kazi wafanye kazi kwa ufasaha,kama hawataki wajaribu,waachie ngazi,wafungue makampuni yao
 
Umaskini wa mtu mweusi chanzo chake ni kutokujua maana ya muda.

Kadi imeandikwa sherehe ukumbini ni saa moja usiku maharusi wanaingia saa tatu na robo.

Kama wewe ni msomi halafu unatengeneza mazingira ya kuusogeza mbele mradi bila sababu ya msingi basi wewe ni kilaza tu.
 
Umaskini wa mtu mweusi chanzo chake ni kutokujua maana ya muda.

Kadi imeandikwa sherehe ukumbini ni saa moja usiku maharusi wanaingia saa tatu na robo.

Kama wewe ni msomi halafu unatengeneza mazingira ya kuusogeza mbele mradi bila sababu ya msingi basi wewe ni kilaza tu.
Huwa sina mashaka na uwezo wako. Lakini sijui comment hii inahusiana na thread hii au jambo lingine nje ya hili?
 
Boss Chakaza Kwa hili Rais yupo sawa, Wataalamu wetu ndio chanzo na tatizo sana Nchini.

Pili, Huyu Mtaalamu ndio Kilaza, utashindwaje kujieleza, isitoshe ushamjua Mh. Rais wakati wote akija unatakiwa uwe umeshajipanga na kuwa na majibu, Urais ni Taasisi. Rais ana Source nyingi za HABARI.

Tatu, hili sakata la Chujio, ni la muda mrefu, lilishaletwa humu JF hasa hapa Jukwaa la Siasa. Watu na Wananchi tukalijadili sana humu. Tukaona mpaka Barua za sijui Mkurugenzi akikanusha na kulitolea ufafanuzi.

Nne, Mikataba mingi, ni mibovu na haina tija kwa Taifa. Hongera Mh. Rais kwa kufumua Mikataba mibovu. Hasa kwenye Halmashauri na Kote. Watu wasiokuwa na sifa ndio wanakuwa wanapewa tenda, inhali watu wenye sifa na wanaoshinda tenda wakinyimwa.

Tano, Mh. Rais aliongea kwa Uchungu na Hasira, ila ukweli kawapa. Hayo mengine ni hali ya Kibinadamu.

Ushauri: Wataalamu wetu inabidi waamke, Wafanye kazi kwa uweledi na kufuata miiko ya Taaluma zao, Mh. Rais endelea kufumua mikataba mibovu na Wataalamu wabovu. Kuna Maeneo Mh. Rais anafanya vizuri sana, ila kuna kasoro ndogo ndogo ndio huwa anakoseaga.
Mkuu, pamoja na utetezi wako bado sikubaliani na wewe kitendo cha Rais kuwatukana watu hadharani kuwa ni Wapumbavu. Kama wewe huwa unafanya hivyo kwa wanao ukikasirika ....... avoid doing that in future.

Mtu kukasirika haina maana anaweza kutamka lolote kwa vile tu ana hasira. Kama kiongozi ni lazima ajue kucontrol hisia zake hasa akiwa hadharani!!

Kwa mtazamo wangu siyo hasira bali ni Something else ..............!!
 
JamiiForums kama kawaida yetu tunataka kujiridhisha water treatment inafanyikaje ktk mitambo na chujio . Bahati kuna mfano hai Mtambo wa kutoa taka ngumu, laini na chujio la maji Ruvu . Wataalamu wanasema maji hubadilika kutokana na msimu wa masika au kiangazi aina ya uchafu na changamoto zake .

Wataalamu wanatutembeza kuona 'chujio' na hatua za kufanya maji yawe safi na salama
 
WanaJamiiForums tupitie video hii kuona mfano chujio na mitambo ya kuchujia maji na kupima changamoto zake kibajeti na kitaalamu. Mtaalamu Eng. Joseph Mkama na Eng. Immaculata wanatutembeza hatua kwa hatua tupate ABC ya masuala ya uzalishaji mkubwa wa maji safi na salama ya matumizi ya wengi

 
Wanasiasa wanatakiwa kuwa wasikivu kwa masuala ya kitaalamu mambo ya kulazimisha yanaweza kusababisha hasara na matatizo ya kiafya kwa wananchi wanaolengwa kutumia maji hayo majumbani na viwandani.
 
Wewe nawe ni mpumbavu kama hujijui, hivyo project plan iliyosema study hivyo itafanyika miezi 6 ameandika yeye? Hiyo imeandikwa wizarani na inatekelezwa na walio shinda tenda huko wizarani. Mhandisi wa wilaya ni msimamizi tuu wa huku site iweje yeye aambulie matusi kwa mambo yaliyo pangwa wizarani?
Kama kitu hujaelewa ni bora kukaa kimya au kuuliza sio unaweka hoja ya kijinga yenye dharau.
Acha ujinga wa kipumbavu wewe jamaa hivo Navyo ni vitu vya kushindwa kuelewa? Kwani nice lazima ukipewa deadline miez 6 ucheleweshe had hiyo miez itimie?
 
Magufuli yuko sahihi, watumishi wengi ni wajinga
Unaweza kuhimiza uwajibikaji bila kudharirisha wenzio. Wanaccm msikinajisi chama kwa siasa za matusi. Chama hiki kilijaa wajenga hoja si watoa matusi. Ni kama akili pungufu au sifa za kijinga mtandaoni na wanamuziki wasakatonge. Kauli ya Kikwete ilipaswa kuwa funzo kwa kila anayejimwambafy
 
Acha ujinga wa kipumbavu wewe jamaa hivo Navyo ni vitu vya kushindwa kuelewa? Kwani nice lazima ukipewa deadline miez 6 ucheleweshe had hiyo miez itimie?
Tena wanaweza wakaja wakaomba wongezewe miezi sita mingine Vilaza wanashida sana!! in Magufuli voice!!
 
Magufuli ni mshenzi. Huo ndio ukweli.

Maneno mengine nasoma halafu nakuwa kama siamini rais mzima anaweza kusema hivi.

Naona kama habari ni ya uongo imetengenezwa kumpakazia kisiasa tu.

Halafu nakuta habari ni ya ukweli.
 
Kipindi cha JK serikali ya CCM inawalea sana wasioweza kazi

Kipindi cha JPM serikali inawaonea watu kwa kuchukua hatua haraka
Jana niliandika hapa kwamba tumetoka kwenye utawala dhaifu wa Kikwete, ruksa remix, tumeenda kwenye utawala wa Magufuli ambao ni kama wa ki Gestapo chini ya Adolf Hitler.

Pote pawili pametuumiza, tulitakiwa tupate mtu wa kukaa katikati hapo.
 
Magufuli ni mshenzi. Huo ndio ukweli.

Maneno mengine nasoma halafu nakuwa kama siamini rais mzima anaweza kusema hivi.

Naona kama habari ni ya uongo imetengenezwa kumpakazia kisiasa tu.

Halafu nakuta habari ni ya ukweli.
Huyu ndiyo Raisi tuliekua tunamlilia miaka mingi maana watu walimuona Kikwete ni mpole sana hadi kufikia hatua ya kumuita dhaifu kumbe alikua muungwana tena wa vitendo,Sasa yule Mkalimkali ndiyo huyu sasa anakanyaga kila mahali safi sana JPM wape vidonge vyao vilaza na wapumbavu wote huko serekalini!!
 
Back
Top Bottom