ibesa mau
JF-Expert Member
- Sep 17, 2015
- 2,109
- 1,692
Hii tabia ya kuzoa zoa tu vijana mtaani na kuwapeleka depo miezi 6 halafu unamwajiri ni uthibitisho tosha kwamba ipo haja ya kuongeza muda wa mafunzo toka miezi sita hadi miaka 3 hadi 5. Askali wetu wamekosa weledi wa kupambana na matukio .
Askali anakwenda kwenye kupambana na maandamano ya watu wasio na silaha halafu ameambiwa achukue risasi za rubber yeye anachukua risasi za moto,michezo kama hii tukiiachia italeta madhara kwa viongozi wetu wa juu.
Wahenga wanasema mchelea mwana kulia, hulia yeye, ipo siku inaweza ikatokea kiongozi wa juu akakagua gwaride kama mchezo wao watabeba risasi za moto baadala ya rubber halafu akatokea kichaa mmoja akamuwasha risasi ya moto sijui hapo tutasemaje.
Nashauri muda wa mafunzo uongezwe lakini pia vijana wanaochukuliwa waangaliwe. vijana wamekaa kijiweni , wamevuta bangi uraiani halafu unamchukua unampa mafunzo miezi sita anakuwa askali hii tabia iachwe waangaliwe vijana wa kuwachukua wachukuliwe hata division one na two.
Kuna kipindi cha miaka ya katikati vijana hadi wenye ziro waliingizwa jeshini hao ndio wanao tuulia watoto wetu wa vyuo wasio na hatia.
Askali wetu wanatumia nguvu nyingi kuliko akili.
Tubadilishe mitaala yao muda wa mafunzo uongezwe kijana akae hata miaka 5 ajifunze na sheria za nchi hii itasaidia kuwa na jeshi lenye weledi mkubwa kama nchi za wenzetu kenya na nyinginezo.