Huu ni uthibitisho kuwa Mahakama zetu zipo huru, haziingiliwi na watawala

MJAMAAHALISI

New Member
Mar 8, 2020
1
3
Katika kuthibitisha hoja hiyo, nitafanya rejea kesi ya Mbowe na wenzake.

UTHIBITISHO WA I
Kesi iliyodumu zaidi ya miaka miwili na hukumu yake yenye urefu wa kusomwa masaa 4 aliweza kuchambua ushahidi wa mashahidi wote, kutafuta kesi za rejea na kufanikiwa kuiandika yote katika masaa 5!

Haiwezekani, hapa bila shaka hakimu alitumia "uhuru" wake kuiandika hukumu miezi kadhaa nyuma kabla hata hoja za majumuisho ya mawakili. (Kumbuka hoja za mawakili zilipelekwa Ijumaa, then Ikafuata wikiendi halafu Jumatatu ndiyo siku eti alikaa kuchambua na kuandika hukumu, Jumanne ikachapwa na kusomwa siku hiyo hiyo!)

UTHIBITISHO WA II
Kitendo cha Hakimu kuanza kusoma hukumu saa 8 huku akijua atatumia masaa 4 kumaliza kusoma, yaani kamaliza kusoma saa 12 jioni, huku akijua muda huo benki zitakuwa zimefungwa, alilenga kuhakikisha wanalala jela na pia kuwapa watu wa magazeti headline "washindwa kulipa, wapelekwa jela" Hapa pia hakimu alitumia uhuru wake kukomoa wapinzani ili apate Ujaji.

Nitaendelea kutoa uthibitisho, kwa leo tuishie kwanza hapa.

Maendeleo hayana vyama.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom