Huu ni utapeli, wizara ya elimu mnajua hili? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huu ni utapeli, wizara ya elimu mnajua hili?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ntemi Kazwile, Jul 6, 2012.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  Jul 6, 2012
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kuna mtindo umeibuka kwa shule za binafsi kuwalazimisha watoto wa shule kuchangia ujenzi wa hostel za shule (mfano St. Anthony), siyo hilo tu bali wanafunzi pia hutakiwa kulipa gharama za ukarabati wa majengo mbali ya kuwa karo katika shule hizi ni za juu sana.
  Ninatoa wito kwa wizara ya elimu kuharakisho mwongozo wa ada na michango kwenye shule binafsi vinginevyo wananchi tutaendelea kunyonywa.
   
 2. E

  EJL Member

  #2
  Jul 6, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 80
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 15
  Hili lina muda mrefu na shule nyingi zinafanya hivi. Angalia orodha malipo ya shule kama Star high school(Arusha), JOHA (Dsm)

  KIFUNGILO girls wameweka kipengele hiki cha majengo; lakini awali ilikuwa kiasi kidogo sana kama 10,000 au 15,000. Na walipohitaji kuongeza nyumba za walimu (ili kuwezesha walimu kuishi hapo shule wakiwa na familia zao) walituma wajumbe wa bodi kuzunguka kila mkoa na kukutana na wazazi kujadili na kuamua nini kifanyike. Wazazi wakaafiki ni vema kuongeza kipengele hicho kwa muda fulani. Nakumbuka wazazi wa Arusha (wakati huo nikuwa huko na nilishiriki kikao) tukapendekeza kuwa kwa vile nyumba tunazihitaji haraka na kuchangia huku kidogo kidogo itachelewesha kupatika kwa nyumba ni vema shule ikaomba mkopo then michango hio itakayokuwa ikikusanywa iwe inalipa deni hili.

  Tatizo la shule nyingine ni kuwa hawashirikishi wazazi katika michango hiyo, haijulikani mzazi ataendelea kulipa kiasi hicho kwa muda gani, na hata kiwango cha kuchangia kuandikwa tu pasi na kuwafahamisha wazazi gharama nzima ya ujenzi huu. Mzazi mmoja alimuandikia Headmaster wa Star high school "hivi kwa michango hii mtoto wangu akimaliza kidato cha 4 hapa si atakuwa amekamilisha chumba kimoja yeye peke yake?" Maana kiasi cha Star sch mwaka 2008 kilikuwa kinakaribia laki 4.

  Ushauri wangu, kwa kuwa hii ni biashara wamiliki wa shule wanapaswa kukamilisha ujenzi na mahitaji yote ndipo waruhusu kuandika watoto. Usajiri wa shule usifanyike kabla shule haijakamilika.

  Wenye watoto katika shule hizi wa binafsi au taasisi za dini chukueni hatua ya kuhoji malipo haya; si vema kukaa kimya tu kwa vile leo una fedha ya kulipa. Kumbuka unalea tatizo ambalo tuendako halikomi.
  Angalia shule sa Serikali/ kata ulipoanza mtindo wa kuchangia madawati tukanyamaza kwa vile tulikuwa na hela ya kulipia. Leo hii shule nyingine zina mwaka wa 10 tangu waanze style ya kila mtot kuchangia dawati 1 lakini madawati hayaja jaa, watoto bado wanakaa chini. Hata ukitafuta yaliyovunyika huoneshwi. HUU NI MRADI USIOLIPIWA KODI!
  Wakaanza na style ya kila mtot alete ream 1 ya karatasi (wengine kwa mwaka mara 1 au 2). Fikiria shule yenye watoto 400 kila mtoto analeta ream 1 (na ni lazima maana hakuna mwanafunzi anayekwepa hili aidha hufukuzwa shule). Shule ina ream 4000. Lakini tembelea stoo ya shule baada ya mwezi 1 tangu wakusanye ream ukikuta ream 100 nitafute nikupe zawadi!
  Ndugu mmoja alisema; UFISADI TZ UPO KILA MAHALI.BAHATI MBAYA TUNAMTAZAMA LOWASSA NA CHENGE TU, TUNASAHAU MAFISADI TUNAOISHI NAO HUKU CHINI, AMBAO NI WABAYA ZAIDI MARA 1000 KULIKO HAO 2!

  EJL
   
 3. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #3
  Jul 6, 2012
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  EJL shule kama zilivyo biashara zingine zinatakiwa zitafute mitaji kwenye masoko ya mitaji kama vile mabenki ili kugharimia ujenzi/ukarabati wa majengo ya shule zao, siyo sawa hata kidogo kufanya kama wanavyofanya sasa kwani wanatumia shida za wazazi kuona watoto wao wakipata elimu bora kujineemesha kwa kuwalazimisha wazazi kuchangia wakati zikikamilika zinabaki kuwa mali za wenye shule. Hii ni sawa na walivyofanya CCM kwenye majengo na viwanja vilivyojengwa kwa nguvu za wananchi wote ambavyo sasa vinanufaisha CCM peke yake.
   
 4. james chapacha

  james chapacha JF-Expert Member

  #4
  Jul 6, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 942
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Ndg yangu ulichokisema ni sahihi kabisa,ila fanya utafiti ujuwe nani wamiliki wa izi shule au wabia wao.na isipo chukuliwa atua kuna siku hata wamiliki wa nyumba kama ile ya JOSEPHAT JOSEPH nawao watadai michango ya majengo.
   
Loading...