Huu ni utapeli uliohalalishwa

Gluk

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
1,855
2,953
Habari wanaJF;

Leo nataka niongelee UTAPELI uliohalalishwa, nao ni hizi kampuni zinazofanya biashara ya mtandao
(Network Marketing) Nimeshudia vijana wengi wakilizwa na hizi biashara hususani mawanawake na wanafunzi wa chuo.

Hawa jamaa wanakushawishi kwa ahadi kuwa ukitoa kiasi fulani utaingiza watu kadhaa na wewe utajipatia mamilioni ya pesa kwa lugha yao huita pea ( pair).
Ukijiroga ukaingia unabaki na kazi ya kuanza kuvaa shati nyeupe na suruali nyeusi na kuaminisha kuwa wewe ni bilionea mtarajiwa kumbe moyoni unaugulia maumivu..

Siku moja niliwahi kuhudhuria semina zao uli kufanya utafiti wangu mmoja kasimama mbele na kujinasibu kuwa kafanikiwa sana na anaingiza mamilioni ya pesa kwa wiki na anabadili magari apendavyo, jioni tulivyotoka nikamkuta standi ya daladala na tugagombania DCM za Mbagara pamoja.

NB: Ukiitwa kwenye fursa tambua kuwa wewe ndiyo fursa yenyewe.
 
wewe utakua unamzungumzia SIR JEFF ON DEMAND 🏃‍♂️ 🏃‍♂️ 🏃‍♂️ 🏃‍♂️ 🏃‍♂️ 🏃‍♂️ 🏃‍♂️
 
wewe utakua unamzungumzia SIR JEFF ON DEMAND
Apana simzunguzii huyo, ila nimezungumzia wale wote wanaotumia mianya ya hali ngumu kiuchumi kujipatia kipato kwa njia ya udanganyifu hususani hawa wanaojiita network marketing
 
Hakuna aliyehalalisha huu utapeli. Ni wabongo ndio tunakuwa wagumu kishtuka na kupenda mteremko
 
Matapeli ni wale wanaowafanya mnatapeliwa mwaka huu na ujao.
Habari wanaJF;

Leo nataka niongelee UTAPELI uliohalalishwa, nao ni hizi kampuni zinazofanya biashara ya mtandao
(Network Marketing) Nimeshudia vijana wengi wakilizwa na hizi biashara hususani mawanawake na wanafunzi wa chuo.

Hawa jamaa wanakushawishi kwa ahadi kuwa ukitoa kiasi fulani utaingiza watu kadhaa na wewe utajipatia mamilioni ya pesa kwa lugha yao huita pea ( pair).
Ukijiroga ukaingia unabaki na kazi ya kuanza kuvaa shati nyeupe na suruali nyeusi na kuaminisha kuwa wewe ni bilionea mtarajiwa kumbe moyoni unaugulia maumivu..

Siku moja niliwahi kuhudhuria semina zao uli kufanya utafiti wangu mmoja kasimama mbele na kujinasibu kuwa kafanikiwa sana na anaingiza mamilioni ya pesa kwa wiki na anabadili magari apendavyo, jioni tulivyotoka nikamkuta standi ya daladala na tugagombania DCM za Mbagara pamoja.

NB: Ukiitwa kwenye fursa tambua kuwa wewe ndiyo fursa yenyewe.
 
Kikawaida hakuna mbongo aliyefanikiwa atayekupa mchongo wa kupata mamilion uwe kama yeye. Ukielewa hili hautasumbuka na utapeli wenye sura ya fursa
 
Forever living walinipata nikiwa chuon 2011 na nimeenda enda vi tour vyao vya ndani ya bongo.Hasa arusha.
Habar za kutengenza network sijui ilinupate hela so kwakua siko vibaya sana kwenye convincing nika recruit wat wa 3 faster sanaa.Binafsi sikua interested na eneo la ku sell products so waliponipa tu yale ma vitu yao nikayatumia mwenyeww.Vingine nikampa sister vingine nikamtumia girlfriend wangu Saut mwanza.Nilikomaa sana ku recruit watu na nikaweza lakin sasa hela nikawa sipati nazozitarajia ..nikaona upumbavu huu nikaacha.

NB.
Kilichonichochea sana kufanya hii kitu ni kwasababu nilikua nimempa mimba girl wangu na nilikua nahitaji sana pesa ya maandalizi cz mbali na bum sikua na kipato.
 
Back
Top Bottom