Huu ni ushamba, kupanga mstari kumsindikiza Rais akienda Ulaya

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,211
113,520

Nilidhani huyu mama yenu atakuwa tofauti na waliomtangulia.

Kwamba hatoendeleza huu ushamba wa viongozi mbalimbali wa serikali na idara kwenda uwanja wa ndege kumsindikiza aendapo safari na pale arudipo toka safarini.

Yaani majitu yote hayo, kuanzia makamu wa Rais, mawaziri, sijui mkuu wa mkoa, mkuu wa jeshi la polisi, mkuu wa jeshi la wananchi, viongozi wengine waandamizi wa kijeshi na kiaskari [nadhani nimemuona na wa magereza hapo], na chawa wengine.

Si ajabu hata yale Maharage ya Tanesco yalikuwepo hapo.

Huu ushamba ni matumizi mabaya ya muda wa uzalishaji.

Badala ya kuwa maofisini huko na sehemu zingine za kazi, majitu yote hayo yanaenda kurundikana na kupanga mstari kumsindikiza Rais akienda Ulaya.

Ushamba na ujuha wa kiwango cha juu kabisa.

Na Rais naye hana busara ya kuwaambia hakuna haja ya kunisindikiza wala kunipokea uwanja wa ndege, na badala yake endeleeni kupiga kazi.

Sisi bado sana aisee!
 
Ushamba huu alianza yule dikteta uchwara,alipoteza muda mwingi kukusanya viongozi wote wa wa juu wa Serikali kila kwenye shughuli ndogo tu ambazo hazikuhitaji jumuiko kama hilo.

Kabla hajaingia madarakani shughuli kama za kuwaapisha viongozi wa ngazi mbali mbali tulikuwa tunaziona tu kwenye taarifa za habari na kusoma kwenye magazeti lakini Mhutu alikuwa anasimamisha hata matangazo ya vyombo vyote vya habari ili aonekane yeye nchi nzima, huu ni ushamba.
 
Sijui bhana labda tunatofautiana uelewa,kwa uelewa wangu nchi sio kibandaumiza kwamba ukiwa kama mkuu wa nchi usafiri bila kuketi na wasaidizi wako wote wa sekta nyeti za nchi na kuwaachia majukumu.

Pia familia bora inapotokea mkuu wa familia mf.baba au mama anasafiri safari ya mbali lazima akae kikao japo kidogo na atakaekaimu uendeshaji wa familia na ikitokea nafasi ya kumsindikiza mpaka kituo cha kupandia usafiri sio dhambi kwa desturi zetu sisi wasukuma na pengine watanzania wote
 
Nilidhani huyu mama yenu atakuwa tofauti na waliomtangulia.

Kwamba hatoendeleza huu ushamba wa viongozi mbalimbali wa serikali na idara kwenda uwanja wa ndege kumsindikiza aendapo safari na pale arudipo toka safarini.

Yaani majitu yote hayo, kuanzia makamu wa Rais, mawaziri, sijui mkuu wa mkoa, mkuu wa jeshi la polisi, mkuu wa jeshi la wananchi, viongozi wengine waandamizi wa kijeshi na kiaskari [nadhani nimemuona na wa magereza hapo], na chawa wengine.

Si ajabu hata yale Maharage ya Tanesco yalikuwepo hapo.

Huu ushamba ni matumizi mabaya ya muda wa uzalishaji.

Badala ya kuwa maofisini huko na sehemu zingine za kazi, majitu yote hayo yanaenda kurundikana na kupanga mstari kumsindikiza Rais akienda Ulaya.

Ushamba na ujuha wa kiwango cha juu kabisa.

Na Rais naye hana busara ya kuwaambia hakuna haja ya kunisindikiza wala kunipokea uwanja wa ndege, na badala yake endeleeni kupiga kazi.

Sisi bado sana aisee!

Hapo wameaganiana wapi Dom au wameagiana Dar
 
Back
Top Bottom