Huu ni unyama kwa mtoto hapa kagera-tanzania haina mwenyewe? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huu ni unyama kwa mtoto hapa kagera-tanzania haina mwenyewe?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ta Muganyizi, Jan 20, 2011.

 1. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #1
  Jan 20, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  HUU NI UONEVU KWA WATOTO

  Kwa muda wa takribani wiki mbili sasa, wadau mbalimbali mlikuwa mkifuatilia tukio lililotendeka hapa Bukoba, Katika kitomgoji cha Bihoko, Mtaa wa Bunumkangoma ulioko kata ya Kahororo katika Manispaa ya Bukoba, Ambapo mtoto Bernard Joseph (14) alipofanyiwa ukatili kwa kuugunzwa na moto na Baba ambaye alijulikana kwa jina la EMMANUEL TX A.K.A Kipara, mfanyabihashara maarufu wa samaki Bukoba, kwa madai ya mtoto kuiba choki ya umeme.

  Mtoto Bernard Joseph aliyeunguzwa kikatili na kisu chenye moto mkali akidaiwa kuiba choki ya umeme
  Mashirika ya TADEPA na TECDEN Kagera kama wadau wa watoto mkoani Kagera, Tumeweza kufuatilia kwa karibu tukio hili, ili kuhakikisha mtoto huyu aliyefanyiwa kitendo hiki cha kinyama anapata huduma ya matibabu, lakini pia adhabu kali inatolewa kwa utuhumiwa wa tukio hilo la kinyama ili iwe fundisho kwa watu wanaodhubutu kuwafanyia matendo mauvu watoto.
  Katka kupata mtiririko mzuri wa tukio hili na kupata taarifa za uhakika, Hatua ya kwanza iliyochukuliwa ni kutafuta mwandishi wa habari wa CHANNEL TEN Bwana MATIAS BYABATO ambaye ndiye alikuwa wa kwanza kutoa taarifa za tukio zima, ili kuweza kujua taarifa za tukio na amefikia hatua gani.

  Kwa Maelezo ya Bwana MATIAS baada ya kutoa taarifa kama ilivyoripotiwa CHANNEL TEN tarehe 14/01/2011, Aliweza kupata vitisho vingi hasa kutoka kwa Askari Polisi na watu wengine asiojulikana kwa madai kuwa alitoa habari zisizo za kweli. Lakini baada ya kutibitisha kuwepo kwa tukio hilo aliambiwa atoe picha za Mtoto alizochukua eneo la tukio, Bwana MATIAS aliwakatalia na kuwaambia waende wakachukue wenyewe kwani eneo la tukio linajulikana.

  Vitisho havikuishia hapo kwani baadae askari polisi walirudi na kumwambia atangaze kuwa mtuhumiwa amukwishakamatwa, lakini MATIAS kwa ujasiri aliwajibu wakatangaze wenyewe kwani yeye alishatangaza alichokishuhudia

  Na mara ya tatu walimfuata nyumbani kwake wakihitaji Laptop yake na kumuonya asiendelee na tukio hili. Lakini pia Bw. MATIAS aliweza kutueleza kuwa tunaweza kupata taarifa zaidi kutoka kwa Mganga wa kituo cha Afya cha Kahororo ambaye baada ya kupata taarifa kuwa mtoto aliyeungzwa na moto yuko nyumbani kwa takribani siku kumi na ameshindwa kupata form no 3 ya polisi (PF3) ili aweze kupata matibabu.

  Tarehe 19/01/2011 niliamua kwenda TECDEN, kumchukua afisa mmoja wa shirika Bi. Costas Sizimwe ili kufuatilia habari hii kwa mganga wa zahanati ya Kahororo pamoja na kufika nyumbani kwa mtoto ili kuona Maendeleo yake na kuongea na wazazi wake ili tujue mpaka sasa ni hatua gani zimechukuliwa. Katika safari hii tuliweza kuambatana na mwandishi wa Redio Kasibante ili tuweze kuujulisha umma nini kunaendelea juu ya tukio hili la kinyama.

  Tulifanikiwa kumkuta mganga mkuu wa zahanati ya Kahororo ajulikanaye kwa jina la VERUS KWEYAMBA. Bwana Kweyammba aliweza kueleza alivyopata taarifa ya kutokea kwa tukio hilo la kinyama na wasamalia wema na kuambiwa kuwa mtoto yuko nyumbani na hali yake ni mbaya sana.

  Baada ya kupata taarifa hizo Bwana MATIAS aliamua kumfuata mtoto nyumbani na kumleta kitoni na kuanza kumpa matibabu bure bira kuwa na form ya polisi no 3, ambapo aliwashauri waifuatile baadae.
  Kwa sababu tatizo lilikuwa kubwa na mtoto alishaanza kuoza sehemu alizopata majeraha, aliamua kuwapa rufaa kwenda hospitali ya mkoa kwa ajiri ya matibabu zaidi.
  Mganga huyu alitushauri tufike wenyewe tuone hali sisi wenyewe Pamoja na kwamba ameanza kupata nafuu, alikili kuwa aliyefanya tendo hili afai kuitwa binadamu na anastahili kuchukuliwa hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa watu wengine, ingawa alisisitiza kuwa mtoto huyu anahitaji kufanyiwa physiotheraph vinginevyo mkono utalemaa.
  Tuliamua kuelekea nyumabi kwa mtoto huyo, tulimkuta mama mzazi wa Bernard ajulikanaye kwa jina la Anathoria Henerco (41) maarufu kama mama Mkaile ambaye pia n mlemavu wa mguu. Tuliambiwa mtoto Benard ameondoka nyumbani tangu juzi jioni tarehe 18/01/2011 na baba yake ameelekea mjini kumtafuta.

  Jambo jingine la kushangaza ni kwamba mnamo tarehe 6/12./2010 nyumba yao iliungua hivyo hawana mahali pa kuishi na nyumba ilipoungua kulikuwa na watoto wadogo tu, hivyo kila kitu cha ndani kiliteketea. Hakuna mtu yeyote aliyesaidia kuokoa kitu chochote kwani jirani wa kwanza yuko umbali wa karibu 0.5 km.
  Baada ya kujitambulisha na kueleza nia yetu ya kufika mahali pale, tuliomba mama Mkaile atupe picha ya tukio,hali ya mtoto na hatua zilizokwisha chukuliwa mpaka sasa dhidi ya mtu aliyefanya kitendo hicho cha kinyama.

  Mama mkaile alieleza kuwa tukio hili lilitendeka siku ya terehe 24/12/2010 na wahusika walikuwa ni watoto wa Bwana EMMANUEL TX au Kipala na Emmanuel mwenyewe. Sababu ya kumfanyia mtoto Benard aunguzwe kinyama mwili mzima kwa kutumia kisu chenye moto mkali, ilitokana na kupotea kwa redio ndogo na choki ya umeme kwenye familia ya Bwana Emmanuel ambako mtoto Benard na wadogo zake hufanya kazi za ndani kama kutengeneza senene na shughuli nyigine ndogo ndogo.

  Mama mkaile anasema wakati tukio hilo linatendeka yeye alikuwa amekwenda kwao kijijini (Kanazi kata ya Katerero) kwa ajili ya sikukuu ya krismas na mwaka mpya. Aliporudi tarehe 3/01/2011 alianza kupata taarifa mitaani kuwa mtoto wake aliunguzwa vibaya tangu tarehe 24/12/2010 na mpaka sasa hakuna huduma yoyote iliyotolewa dhidi yake. Baada ya kufika ndani alimkuta mtoto Benard akiwa katika hali mbaya kwani baadhi ya sehemu zilikuwa zimejaa usaha na kuanza kunuka.

  Mama Mkaile anasema hakuwa na lolote lakufanya zaidi ya kuanza kulia na kumwoma Mungu, kwani mtoto hakuwa na form ya polisi no 3 (PF3) ya kumuwezesha kupata matibabu, lakini pia hakuwa na njia yoyote ya kunsafirisha kutoka nyumbani hadi zahanati kwani wanaishi mlimani ambapo ni vigumu kwa usafiri wowote hata wa baiskeli kufika.

  Kesho yake kwa maajabu alimwona Bwana Matias na mganga mkuu wa zahanati ya Kahororo wanafika na kumsaidia kusafirisha mtoto kutoka nyumbani hadi zhanati ambapo alisaidia kumpatia mtoto huduma ya kwanza bila kuwadai PF3.
  Kutokana na tatizo kuwa kubwa mganga huyu aliwaandikia rufaa ya kwenda hospitali ya mkoa kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
  Mama mkaire anasema kutokana na uwezo wao kiuchumi kuwa mdogo sana na kutokuwa na msaada wowote hasa wa chukula, baada ya kukaa hospitali ya mkoa siku mbili waliomba kuluhusiwa ili mtoto augulie nyumbani ambapo wataweza kupata chakula.

  Baada ya kuruhusiwa walifungiwa madawa na kurudi nyumbani, ingawa kuna kila dalili kuwa mtoto asipofanyiwa physiotherapy mkono utalemaa
  Lakini pia mama analalamika kuliofanya kitendo hata hawakuweza kufika hospitali wala nyumbani kuwajulia hali au kutoa chochote tofauti na shilingi elfu tatu 3,000 Bwana Emmanuel Kipala alizotoa siku mototo alipopelekwa hospitali.

  Kabla ya kumaliza maongezi, Bwana Josephati ambaye ni baba mzazi wa Bernard alifika na kutueleza kuwa alikuwa hajaenda kumtafuta mtoto kama tulivyokuwa tumeelezwa na mama, hivyo haijulikani mtoto alipo tangu jana na yuko katika hali gani, ingawa baba anasema anajua sehemu wanakokaa huko kashai Bukoba mjini na akahaidi kumfuatilia.
  Sisi pamoja na wazazi tulikubaliana wamtafute mtoto Bernard alipo na kumleta ofisini TADEPA ili tuangalie maendeleo yake kiafya na ikibidi tusaidie kumpeleka hosipitali kwa ajili ya huduma ya physiotherapy na matibabu mengine.
  Leo hii tarehe 19/01/2011 wazazi wa Bernard waliweza kufika hapa ofisini wakiwa na mtoto wao Bernard waliyefanikiwa kumpata jana jioni muda wa saa 11.30
  Nimeweza kuomngea na Bernard ili kujua chanzo cha kuunguzwa na moto kikatili na ni nani hasa aliyehusika na kitendo hicho


  Bernard {katikati} akiwa na wazazi wake Joseph {kushoto} ambaye ni baba yake mzazi na anatoria {kulia} ambaye ni mama yake mzazi walipofika ofisini TADEPA

  Bernard anasema waliohusika ni Watoto wa Bw. Emmanuel lakini kwa maelekezo ya baba yao ambaye alikuwa akiwapa maelekezo hayo kwenye simu ya nini wafanye.
  Bernard amewataja waliohusika kwa majina kuwa ni Joely, Eli pamoja na paulina
  Joely anaongeza kuwa baada ya kugundulika kupotea kwa redio na choki ya umeme yeye hakuwepo pale nyumbani kwa Bw. Emmanuel, hivyo wakamtumia mdogo wake amtafute wakidai kuwa akimpata na kumleta pale nyumbani watamsafirisha hadi shinyanga kutembea. Mdogo wake alifanikiwa kumleta Bernard mpaka nyumbani kwa mzee kipara bila yeye kujua kinachoendelea

  Baada ya kufikishwa pale Bernard aliwekwa chini ya ulinzi na Watoto hawa wa Bw. Emmanuel ndipo walipopiga simu kwa baba yao na kuwaelekeza jinsi ya kufanya
  Bernard anasema pamoja na kuunguzwa kwa moto, lakini pia alipigwa na jiwe kubwa kifuani anmbapo anasikia maumivu anapomeza kitu na wakati mwingine anapata taabu ya kupumua.


  Sehemu ya mguu wa Bernard aliyeunguzwa kwa moto kwa kutumia kisu chenye moto mkali

  Aidha Bernard anasema kuwa lengo lao lilikuwa ni kumuua kwani baada ya mateso ya masaa sita kuanzia saa 6 mchana hadi saa 12 jioni walimwambia una bahati yak uwepo mdogo wako sash ii ungekuwa marehemu
  Kuhusu hatua zilizochukuliwa juu ya mtu aliyefanya kitendo hiki cha kinyama, mama Mkaile anasema hana taarifa yoyoyte ya nini kinaendelea na hatua gani zimechukuliwa, tofauti na habari alizopewa na askari polisi walipofika pale nyumbani na kumwambia kuwa mtuhumiwa amekamatwa na kuwekwa ndani. Lakini mama anasema mtuhumiwa alikamatwa na kulazwa ndani siku moja tu na baadae kuachiwa, hajui ni kwa dhamana au kuna njia nyingine iliyotumika. Yeye ameambiwa mtuhumiwa ameachiwa na yuko nje anafanya kazi zake kama kawaida. Alipouliza hatima ya hukumu, aliambiwa hiyo siyo kazi yake kwani kesi tayari iko mahakamani.

  Jambo jingine la kusikitisha sana, Mtoto Bernard anaishi mitaani na matatizo haya kumkuta hakuwa nyumbani tangu walipofunga shule mwezi wa 12/2010.
  Kwa maelezo ya mama yake, kila ijumaa baada ya kutoka shule Bernard hutoweka nyumbani na kurudi jumatatu asubuhi, kuvaa sare na kuchukua madaftari kwa ajili ya kwenda shuleni na kipindi cha rikizo Bernard hutoweka nyumbani na kurudi siku ya kufungua
  Kutokana na hali halisi ilivyo tunapendekeza
  • Mtoto arudishwe hosipitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa afya na kufanyiwa physiotherapy kwa mkono unaoelekea kulemaa
  • Atafutwe huyo mtu aliyefanya tendo hili la kinyama na kurudishwa ndani mpaka mtoto atakapopona kabisa na hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yake ili iwe fundisho kwa wengine
  • Uchunguzi wa kina ufanyike kubaini njia zilizotumika kumdhamini mtuhumiwa wakati mtoto akiwa mahututi.
  • Uchunguzi pia ufanyike dhidi ya maofisa wa polisi wanaotumia vitisho kuwatishia wasamalia wema wanaosaidia kuibua maovu kwenye jamii.
  • Msaada wa haraka wa kisheria utolewe kwa familia ya Bwana Joseph Benjamini ili haki itendeke, ikiwezekana atafutwe wakili wa kusimamia kesi hii kwani familia haina uwezo kabisa wa kuendesha kesi
  • Msaada wa haraka wa ujenzi wa nyumba ya Bwana Joseph ili kunusuru maisha ya wanafamilia na Watoto wengine wanaoishi katika mazingira hatarishi zaidi.
  Bwana Joseph na Bi. Anthonia ni wazazi wa Watoto wanane (8) ambao ni Bernadetha (16), Bernard (14), Benson (12), Anastuzius (10), Jesca (8), mapacha Anagrace na Gration (6) na Ester (3.5)
  Tunakaribisha michango ya hali na mali kwa wadau mbalimbali wa Watoto ndani na nje ya Tanzania ili tuweze kunusuru maisha ya familia hii

  Kachocho R. Timanywa
  OVC Program Officer- TADEPA- Kagera
  Mob: + 255 755 925228/786 608230
  Tel: +255 28 2221000
  Barua pepe: kachochot2005@yahoo.com
  tadepatz@yahoo.com

  NAONA PICHA ZA MTOTO HAZIONEKANIKANI HEBU CHEKI HAPA CHINI
   
Loading...