Huu ni unyama au ulimbukeni au ni nini ndugu zanguni???

CharmingLady

JF-Expert Member
Apr 16, 2012
18,250
12,868
habari zenyu bhana!
Hii ni story ya kweli na wala si ya kutunga.... Kwanza naomba niwape majina hawa wahusika ili twende pamoja. Kuna mkaka anaitwa Juma na mdada anaitwa Fatu na pia kuna mdada mwingine anaitwa Jamila.

Juma na Fatuma walikuwa wapenzi then wachumba kisha wakafunga ndoa wiki mbili zilizopita. Pamoja na Juma kuwa mchumba wa Fatu lakini alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Jamila.

Ilipokaribia siku ya kufunga ndoa kati ya Juma na Fatu, Juma alimgharamia Jamila kwa kila kitu kilichokuwa kinahusiana na harusi... kama mjuavyo sie akina dada kwenye sherehe tunavotupia iwe viatu, nguo na kila kitu, basi pamoja na hayo Juma alimkatia tiketi ya ndege Jamila ili Jamila ahudhurie katika harusi yake (Juma).

Bila hiyana wala mshipa wa aibu kwa Jamila, Jamila alifunga safari kwenda kwenye harusi ya Juma. Basi kufika huko Jamila ndo kwanza akawa Cameraman wa maharusi tena kimbelembele kweli. Sasa hapo najiuliza huo ni ulimbukeni, unyama au tuuiteje...

Ninamsikitikia sana Fatu make najua mahusiano kati ya jamila na Juma hayataisha hivi karibuni. jamani wadada na wakaka ya JF hili mnalionaje??????
 
kwa kweli huku kimanzichana sijawahi kuona ndo mara ya ngu ya kwanza!!!!!!!!!!! hadi nimeukumbuka msemo wa wahenga "kuwa uyaone" ...
 
Wanaosema Poa! Wanapenda Mapenzi ya Kushare... ukimuudhi tu Anamcall Jamila hahahahaha
 
hiyo imekaa vibaya sana. ila ndo maisha ya cku hiz yalivo. Nyumba ndozo zipo kibao
 
Sasa hapo unyama ni upi? Nilidhani huyo Jamila alileta fujo kwenye harusi. Mbona hii ni poa tu. Sioni tatizo hapo
 
tamaduni haziruhusu!

Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya firauni........mie hawara wa ex-hubby alikuja kanisani(tulikua kwenye rehearsal) kumpa mchango wa harusi sasa sijui hapa we ungefanyaje?niligombana sana siku hiyo nikanuna sanaaa lkn haikusaidia na harusi ndio ilikua siku mbili zijazo. Na harusini alikuja na kucheza sanaaaa na baada ya harusi waliendelea kumegana mpaka walipoamua kusitisha wenyewe kwa mapenzi yao(sikumshurutisha amuache). Haya niambie unaionaje hii?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom