Huu ni Unafiki wa kisiasa, Mwenyekiti wa CCM hukuona kuwa Mbunge wa Morogoro hafai?

Magufuli atuambie kwa hili kabla ya kumshambulia abood .ni nani aliyesababisha kiwanda cha tumbaku na kile cha kutengeneza jezi morogoro vifungwe na vijana karibu 2000 kukosa ajira? Kama sio Sera mbovu za kodi za serikali ya Maghufuli?
Tumbaku na Mazava vilikuwa vinaajiri watu zaidi 2000, ajira za moja kwa moja, bado ajira zingine za suppliers wa mahitaji ya viwandani, madereva, clearing& forwarding, n.k.

Daah cha msingi tusomeshe watoto historia darasa la 1 mpaka kidato cha 6.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Eti mabasi yake (Abood) yanasafirisha watu waliokoseshwa ajira na Abood hadi wakafa...
Kwani uwongo? Kuna ma Bus ya zamani yanaitwa BUNDI wewe ukifiwa ndani ya manispaa ya Moro unawahi asubuhi mapema kuomba Bus linakuja fasta kusaidia kupeleka watu makaburini.
 
Mkuu,.
Kumbe ulifatilia na una kumbukumbu,Tena Rais akasema,Avoid awe mfano kwa wengine,anajitolra kutoa mabasi yake kwenda kuzika.
Atakuwa amepata data mpya jioni /usiku baada ya kumaliza uzinduzi wa soko...
 
Hakuna mwekezaji anaeweza kuacha kuwekeza kama huo uwekezaji ni viable!

Ukimpa mtu Kiwanda kilichokufa ukaona hajakifufua jua kuna tatizo sio ku jump kwny conclusion, udhalilishaji na kuchonganisha Raia na Mbunge wao kuwa Wanakufa kwa stress za kukoss ajira, kwani Aboud ndio anakusanya kodi zao
Sasa kama kiwanda kimekyshinda si unakirudisha ili apewe mwingine? ABOOD amegoma kurudisha mpaka wakamnyanganya kwa nguvu, mbaya zaidi amekitumia kiwanda kukopa pesa akaenda kununulia Ma Bus contrary to the agreement.
 
Hakustahili kuwa rais, maana alichoongea leo kuhusu huyo jamaa, na alichosema jana kumuhusu ni vitu viwili tofauti.

Halafu ukizingatia kuwa yeye ndio aliagiza wagombea wa ccm watangazwe washindi nchi nzima, ndio maana kila mtu inabidi ajue madhara ya madaraka makubwa ya kikatiba kwa cheo cha urais.

Ninazidi kujiridhisha huyu jamaa hakustahili kuwa rais, hasa kwa nchi yenye katiba dhaifu namna hii.
Achana na urais.

Huyu hakustahili hata kuwa baba wa mtu.
 
Magufuli atuambie kwa hili kabla ya kumshambulia abood .ni nani aliyesababisha kiwanda cha tumbaku na kile cha kutengeneza jezi morogoro vifungwe na vijana karibu 2000 kukosa ajira? Kama sio Sera mbovu za kodi za serikali ya Maghufuli?
Yaani hili la Maviga na TTPL lilitakiwa kuwa limeondoka na watu dazeni kadhaa,lakini kwa kuwa Tz mkubwa hakosei,ni tilalila tuuu.
 
Ghafla Abood amekuwa mbuzi wa Azazeli.

Ila huyu hawawezi mfanya lolote.

Alafu yawezekana kabisa hii episode ilipangwa kama utani wa kisiasa lakini lugha ya muigizaji mkuu imefanya ionekane kama tukio la kweli.

Au kwa kuwa ni Morogoro, labda huyo muigizaji mkuu ameingiliwa na mzimu wa “Chingalungalu”.
 
Huyo Mbunge Abood inabidi ajiuzulu na serikali imchukulie hatua kali bila hivyo Chama na serikali kitakuwa kinaendelea kule fake investors, wakwapuwaji wa mali za umma na kuna uwezekano kajenga kule Canada au Uarabuni kwa kutumia ndugu wa karibu, TAKUKURU ifanye kazi iache kumwachia mzigo Rais wa nchi. Ameshaua watu wangapi and coverup anawapeleka makwao kwa mazishi akijifanya anatoa misaada kumbe kauza viwanda! Kudos Rais Dr Magufuli!
 
Kwa Lugha nyepesi na ukijiongeza zaidi hapo Mbunge Abood anaambiwa ajenge Viwanda zaidi ili Ajira zipatikane na Serikali iweze Kukusanya Kodi zaidi.
Vijana wa praise and worship hamkosekani kumtetea mwenyekiti wenu hata kama kosa linaonekana wazi
 
Back
Top Bottom