Huu ni unafiki ,ushabiki,ufisadi wa demokrasia au ndio democracy ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huu ni unafiki ,ushabiki,ufisadi wa demokrasia au ndio democracy ?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by fige, Feb 11, 2011.

 1. fige

  fige JF-Expert Member

  #1
  Feb 11, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 376
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna anayeweza kupinga kuwa hali iliyokuwapo Zanzibar ilikuwa tete kabla ya muafaka, hili halipingiki .lakini kile ambacho ccm wanajivunia kuwa wameonyesha nia safi na ukomavu wa kisiasa ni wao waliotengeneza hali hiyo kwa kupora ushindi wa cuf mara kadhaa.

  Leo hii ccm wanapolazimisha wapinzani kuungana je wamekuwa wema sana ,au ni unafiki ?

  Kinachonishangaza ni kwamba imechukua miaka 15 muafaka kupatikana
  Zanzibar lakini baado ccm wanaendeleza ushabiki uleule ulioigharimu zanzibar.Siku zote ushabiki ukiambatana na kejeli huzaa chuki au wamesahau mara hii,hivi wanadhani kuendelea kuwakejeli chadema kutawaletea heshima ?

  Je wao wana nia ya umoja ? kama wana nia hiyo kwa nini hawakubali kuungana na vyama vyingine mpaka (kupata muafaka )mpaka damu imwagike ?

  Nionavyo ccm wanatengeneza machafuko mengine kwa kutumia demokrasia ya wingi wao vibaya.

  Tukiendekeza demokrasia za mkumbo bila hoja zitatufikisha pabaya wabunge wa ccm amkeni mnapandikiza chuki bila kujijua.

  Nawasilisha, na nakubali kukosolewa
  Hii hoja inatokana na mambo yanayoendelea Bungeni.
   
Loading...