Huu ni ulevi wa madaraka!

JAYJAY

JF-Expert Member
Oct 31, 2008
7,494
7,517
Gazeti moja jana Jumapili liliripoti taarifa kuhusu uvushwaji wa sukari kwenda nchini Kenya kwenye wilaya moja huko Kilimanjaro, ambapo serikali imesimamisha uuzaji huo kupambana na upungufu wa sukari nchini.

Waziri wa kilimo anaulizwa na mwandishi kuhusiana na suala hilo na anachojibu ''nipo nje ya nchi nikirudi nitafuatilia suala hilo". angalia huyo waziri ni msomi mzuri wa ngazi ya juu katika taaluma Profesa lakini anashindwa kutoa majibu mazuri, kwa sababu ana msaidizi wake ambaye ni naibu waziri, alishindwa tu kumshauri mwandishi awasiliane na naibu wake, je mpaka arudi mambo si ndio yatakuwa yanazidi kuharibika, nimeshindwa kuelewa hizi ofisi wanaziona kama mali yao binafsi, au semina elekezi haziwasaidii? Afadhali hata mkuu wa wilaya, yeye alionesha kufahamu maana ya wasaidizi ambapo alimshauri mwandishi kumuuliza kaimu wake kwa kuwa yeye yuko likizo, sasa sijui ingekuwaje naye angemshauri mwandishi angoje mpaka atakapomaliza likizo yake.

Na kwa kumalizia nina mashaka makubwa na uadilifu wa kaimu kamanda wa mkoa huo kutokana na majibu yake juu ya suala hili ambapo alijibu "hakuna kitu kama hicho na taarifa hazina ukweli wowote". Hivi huyu mtu hafaidiki kweli na biashara hiyo kwa sababu huwezi kupinga jambo moja kwa moja bila taarifa ya kina kwa sababu taarifa ya mwandishi inasema kuwa askari wanahusika na biashara hiyo, au amesahau kuwa wakati ule mahindi yanavushwa ni polisi hao hao waliokuwa wanasindikiza magari?

Nadhani inafaa achunguzwe kama hana masalhi na hiyo biashara.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom