Huu ni Ukomavu au Udhaifu wa Mwanasiasa?

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Mar 1, 2016
4,790
2,000
Habari wana JF

Mabadiliko makubwa kwenye duru za kisiasa hapa nchini zimenifanya nijiulize hili swali, je kuhama chama kimoja na kwenda kujiunga na chama kingine ni ukomavu au udhaifu wa mwanasiasa?

Sababu kuu ya kujiuliza swali hili ni ukweli kwamba vyama vya siasa vinaundwa vikiwa na sera fulani vinavyoziamini na vikiwa na katiba ambayo inaelezea mission na vision ya vyama hiyvo. Mara nyingi, sera au katiba za vyama hazibadiliki mara kwa mara, ila uongozi. Kwa mantiki hiyo basi, sababu za mwanasiasa mahiri kujiunga na chama fulani, zinapaswa kuwa ni sera au katiba ya chama husika.

Katika duru hizi mpya za kisiasa, upepo umebadilika wapo wanasiasa ambao sasa wameacha vyama walivyoviamini na wamejiunga kwenye vyama kwasababu tofauti na sera na katiba za aidha chama anachotokea au anachoelekea. Katika duru hizi mpya za kisiasa, sababu kama uzuri wa sura ya mwenyekiti, umahiri wa mwenyekiti, utendaji kazi wa kiongozi, pesa na kufuata mkumbo zimekua ni miongoni mwa sababu zinazohusishwa na kuhama kwa wanasiasa kutoka chama kimoja kwenda kingine.

Nikiwa na lengo moja tu la kuongeza maarifa, naomba michango yenu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom