Huu ni ukandarasi gani?

mjarrab

Senior Member
Nov 13, 2015
108
55
Kuna barabara nyingi za kiwango cha lami katikati ya Jiji la Dodoma

Kuna barabara za lami ya kiwango cha juu zilizo jengwa kipindi cha awamu ya nne ya uongozi wa nchi.

Maeneo ya kisasa, kikuyu,chang'ombe, Arra A na maeneo ya katikati ya Jiji yalibahatika kupatiwa barabara za lami tangu wakati wa awamu ya nne.

Kwa kweli lami zilizo tandikwa zilikuwa ni za kiwango cha juu,Lakini kinacho sikitisha ni namna wakandarasi walivyo tekeleza mradi huo bila kuzingatia Mambo ya Msingi.

kukuta Bomba la maji limepasuka katikati ya barabara ya lami katika Jiji la Dodoma ni Jambo la kawaida.! Kiasi kwamba lami zinafumuliwa na Maji na kuharibu mandhari ya barabara.

Hivi kweli wakandarasi tunao wapa kazi za ujenzi wa barabara hawawezi kuangalia namna bora ya kutengeneza mifumo ya kuruhusu miundo mbinu mingine kupita bila kuleta uharibifu usio wa lazima?

Hivi inashindikana kwa mkandarasi kushirikiana na Idara ya Maji kuweka karavati kila baa ya mita 100 kwa ajili ya kupitisha miundo mbinu ya maji katika karavati na kuweka chumbers za kugawanya maji mitaani kwa kila upande wa barabara?.

kwa sababu hata Bomba likipasuka litapasukia ndani ya karavati na hivyo itakuwa rahisi kurekebisha au kubadili bomba bila kuharibu barabara!. Na vile vile karavati hizo zinaweza kupitisha pia miundo mbinu mingine inayo hitajika kuvuka barabara kupitia chini ya Ardhi.

Hebu serekali iangalie Jambo hili limekuwa ni kero katika Jiji la Dodoma!.
 
Kuna Makandarasi wengi kama Nyanza, CCC ya Kichina na wengine na wote wanashirikiana na DUWASA, TTCL na wanapofanya kazi kuna Sub Kandarasi wa mifereji nk
Tatizo la maji kumwagiga na majitaka kufurika ni sehemu za Mjini kati ambao ni Mji wa zamani miundo mbinu iliyowekwa enzi hizo haiwezi himili mahitaji ya sasa.
Angalia maeneo km Kisasa, Njedengwa, Chidachi kote kuko shwari kwani kumepimwa kuhimili onezeko lolote
 
Kuna Makandarasi wengi kama Nyanza, CCC ya Kichina na wengine na wote wanashirikiana na DUWASA, TTCL na wanapofanya kazi kuna Sub Kandarasi wa mifereji nk
Tatizo la maji kumwagiga na majitaka kufurika ni sehemu za Mjini kati ambao ni Mji wa zamani miundo mbinu iliyowekwa enzi hizo haiwezi himili mahitaji ya sasa.
Angalia maeneo km Kisasa, Njedengwa, Chidachi kote kuko shwari kwani kumepimwa kuhimili onezeko lolote
Kwani Miundo mbinu ya zamani haiwezi kufanyiwa Marekebisho na kufuata Mahitajio ya Sasa?.
Hivi ninavyo andika barabara inayo elekea chang'ombe kutokea kituo cha Daladala sunrise Maji yamefumua barabara.pia Mwanzo wa daraja la kuingia chang'ombe Maji yamefumua barabara!.
Naamini Kuna uwezekano wa kubadili mifumo ya zamani ili iendane na wakati.
Kuweka karavati kila baada ya mita 100 kwa ajili ya kupitisha miundo mbinu ya Maji naamini inawezekana.
 
Back
Top Bottom