TUJITEGEMEE
JF-Expert Member
- Nov 6, 2010
- 24,695
- 24,722
WanaJF, jana nilikwenda kwa wauza magazeti kununua gazeti fulani. Kufika pale nikakuta gazeti nililolihitaji halipo. Kwa kuwa nilikuwa nalihitaji sana gazeti hilo nikalazimika kumuuliza muuzaji wa magazeti mahali ambapo niweza kupata gazeti hilo. Alinijibu kuwa nipitie baada ya masaa matatu atakuwa amelipata.Baadaye nilikuja kugundua kuwa wauza magazeti hao ukodisha magazeti kwa watu kwa malipo kati ya Tsh.100 mpaka 300 kulingana na muda atakoutumia (aliyelikodi) kulisoma,aina na bei ya gazeti hilo. Malipo hayo huchukuliwa na wauzaji wa magazeti hayo.Magazeti hayo yaliyokodiwa wakati mwingine ukosa wateja wa kuyanunua hivyo urudishwa kwa wakala wa magazeti hayo. WanaJF kitendo hiki cha wauza magazeti ni ujasiriamali au uharamu (hujuma ya kifedha kwa wamiliki wa magazeti)?