Huu ni Ugonjwa gani wa ngozi kwa Watoto?

iphoneProMAX

Senior Member
Aug 30, 2021
104
94
Habarini wana JF wenzangu.

Kuna ugonjwa wa ngozi naiona kwa watoto, si mmoja si wawili na sijajua inasababishwa na nini... Wakati mwingine huwa wanajiwasha pindi ninapo wahoji wazazi wao.

Nipeni mwongozo kama ni ugonjwa gani na suluhisho lake.

Natanguliza shukurani.

20211121_170524.jpg
 
Ahsante.. Hana ngoma, hosptal aliambiwa ni aleji.
Kutoka hapo mzazi anajua pakuanzia.

Kwanza achunguze aina za vyakula anavyokula mtoto(kwa wale waliofikia umri wa kula),mafuta anayotumia kupikia chakula cha mtoto n.k

Lakini kama mzazi anaweka blueband kwenye uji wa mtoto,aache kwa muda.Watoto wengi matumizi ya blueband yamekuwa yakiwaletea madhara kwenye ngozi.

Pia kama mtoto anatumia uji wa lishe,mzazi asiweke makorokoro mengi,wakina mama wengi hapa ndio tunaharibu.Tuna amini kuweka mavitu mengi ndio lishe,kumbe tunawatesa watoto,mwisho mtoto anapata matatizo kama kufunga choo n.k
 
Huo ni ugonjwa wa ngozi kwa kilatini unaitwa "Tinea Corporis Superficialis".... Huyo mtoto anaonekana bado anabebwa na bila shaka aliambukizwa na mtu mwenye ugonjwa huo baada ya kumbeba.

Tafuta dawa inayoitwa "Clotrimazole Cream" au "Nystatin Ointment" umpake kila siku mara mbili kwa siku hadi ngozi irudi kwenye hali yake.

Kinga: Zingatia kanuni za usafi wa mwili ikiwemo kumuogesha kwa kutumia sabuni ya Dettol Junior, Usiruhusu tabia ya kumshika shika mtoto na kumbeba hasa kwa wageni na majirani na mwisho nguo unazovaa ziwe zimefuliwa na kuanikwa juani ikibidi zipigwe pasi. ndani ya wiki moja utapata matokeo chanya..... Kila lakheri! :cool:
 
Back
Top Bottom