Huu ni ufisadi unaofanyika Makongo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huu ni ufisadi unaofanyika Makongo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Uncle Rukus, Feb 15, 2011.

 1. Uncle Rukus

  Uncle Rukus JF-Expert Member

  #1
  Feb 15, 2011
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 2,430
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Habari za jioni wakuu?

  Nina mtoto ambaye anatarajia kufanya mtihani wa kidato cha nne mwaka huu kama mtahiniwa wa kujitegemea,

  Shuleni kwao waliambiwa kuwa form hawana kwa kuwa baraza la mitihani limebadilisha mfumo wao wa utowaji hizo form, hivyo wanalazimika kuingia kwenye mtandao wa necta{website) na kujisajili kwa ku-upload picha zao na kuingiza baadhi maelezo yao na hatimaye kupata form ambayo wanatakiwa kuiprint na kwenda kulipia...

  Nime mfanyia wanangu hayo yote na kumpa hiyo form kwaajili ya kwenda kuwekwa sahihi na muhuri shuleni kwao.
  Na baada ya kuipeleka jana waliambiwa wakazichukue leo...


  Cha kushangaza ni kwamba uongozi shule ya Makongo, ameingia darasani kwao na kuwa hoji ni wanafunzi wa ngapi wameji andikisha necta, karibu wanafunzi wote walikuwa wamejisajili kasoro wa nne tu ndio walikuwa hawajajisajili.

  Baada ya kugundua wanafunzi wengi wamekwisha jisajili, bw. Maebe aliwaambia kuwa usajili wao ni batili, hivyo wanapaswa kujisajili tena hapo shuleni...
  Baada ya kumuhoji mwanangu nime gundua kuwa..
  Mwanzo uongozi wa shule ndio uliowataka wakajisajili kwenye ma-internet cafe, kwa kuwa wao scaner na printer zao zilikuwa kuwa mbovu, sasa baada ya kununua nyingine ndio wameona bora kuwadanganya wanafunzi kuwa kuna taarifa wamezipata kuwa kuna uwezekano wa baadhi yao kushindwa kufanya mtihani eti kwa kuwa inawezekana hawakujisajili vizuri..

  Hivyo watawasajili tena kwa kutumia internet ya shule na printer zao kwa gharama ya tsh elfu 5,000.

  Huu ni wizi wa hali ya juu jamani, tunapaswa kuukemea kwa nguvu zote...
   
 2. M

  MAKAH JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 1,598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nimekusoma waitu!! hapa Mbeya kuna taasisi moja imejitia kuhodhi usajili kupitia mtandao na kuwaongopea watahiniwa to be kuwa wasiende kwenye cafe kwa vile fomu za kwenye cafe ni feki. Na inasemekana sumu hiyo imemwagwa na taasisi hiyo hadi kwenye vituo vya kufanyia mitihani. mtoto akienda kulipia kituo anaambiwa ukitoka hapa nenda taasisi fulani usiende kwenye cafe fomu zao ni fake!!. Matokeo yake taasisi hiyo imeshindwa kazi watoto wamekaa hadi usiku wa saa nne hadi tano wakiminyana kupata "fomu halali". Halafu wanapeleka fomu kwa taasisi dada na kutozwa shs 5,00 zaidi ya fee ya mtihani ya 35,000/= eti za kusafirishia fomu ya ukurasa mmoja!!!. Ukijumlisha na ile ya kutolea fomu "za NECTA" shs 5,000/= inakuja shs 45,000/=. Hii inchi yetu sijui watu wakoje tena watu wenye amana kubwa.
  Itakumbukwa kuwa ni cafe hizozo ambazo ziliisaidia TCU kusajili vijana walioomba kujiunga na vyuo vikuu mwaka jana kwa ufanisi mkubwa.
  Hapa naiangushia lawama NECTA moja kwa moja kwa kutokuwa wawazi katika hili. Mbona TCU ilisambaza vitabu vyao vya miongozo hadi maktaba za mikoa na shule hadi hata mtu mjinga alifahamu afanye nini akitaka kujisajili. Matokeo yake taasisi kama hizi za NECTA zinakua kichocheo cha wananchi kuichukia serikali yao.
   
 3. Mentee

  Mentee Senior Member

  #3
  Feb 16, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 142
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Sio Makongo tu. Karibu shule zote Dar.
   
 4. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #4
  Feb 16, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Wizi kila mahali...
   
 5. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #5
  Feb 16, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,526
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Kwenye Mfumo wa elimu ndiko kwenye kitovu cha wizi. Unategemea nchi itakuwa salama? Lakini msingi wa haya yote ni kuwa, Dhamana ya elimu imekabidhiwa mikononi mwa wajinga.
   
 6. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #6
  Feb 16, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  Taasisi gani hiyo mkuu, weka wazi hapa..huwez juwa nani anasoma! Kufichaficha maradhi kutatumbua usaha.
  Ukishindwa kutaja kampuni itakuwa unafki.
   
 7. M

  MAKAH JF-Expert Member

  #7
  Feb 16, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 1,598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Inatosha kusema tbc1 wameitoa taasisi hiyo katika taarifa zake za hivi karibuni. kurudia kuitaja naona kichefuchefu
   
 8. Uncle Rukus

  Uncle Rukus JF-Expert Member

  #8
  Feb 16, 2011
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 2,430
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mkuu, usipate kichefuchefu tutajie tu itatusaidia sana, hatupaswa kuwaogopa hawa watu ni lazima tu deal naona kuhakikisha haki inatendeka...

  Asubuhi hii nimewasiliana na mkuu shule ya Makongo bw. Maebe ili anieleze ubatili wa hizo fomu, ameshindwa kunieleza na kudai kuwa kuna taarifa amezipata toka necta ambazo asingependa kuzisema hivyo akaniambia kama nina amini fomu ya mwanangu ni halali hakuna shida ila nisiwalaumu endapo mwanangu hatashindwa kufanya mtihani wake.

  Ni wizi tu na ujanja ujanja wa kutaka kula pesa za watu. Nataka niwasiliane na Necta ili kupata ukweli wa ili jambo.

  Wakuu tufanye nini kuukomesha huu wizi?
   
 9. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #9
  Feb 16, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,710
  Trophy Points: 280
  Mkuu, kwasasa ufisadi bongo wala sio kosa tushahalalisha!
   
 10. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #10
  Feb 16, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  wee! Unanitisha! Sekta hii si anaiongoza dr? Tena dr.Shukuru!na Ndalichako? Sasa wajinga gani mkuu unasema?ebu weka wazi mkuu! Kanusha au bunge la Jf litakuomba udhibitishe kwa maandishi. Ila kwa ujumla NECTA inaleta siasa za kipuuzi,mbona enzi zetu tulisoma bila kuwa na bughudha ziwapatazo vijana wa leo? Ni hatari kwa afya ya elimu yetu jamani.
   
 11. Uncle Rukus

  Uncle Rukus JF-Expert Member

  #11
  Feb 16, 2011
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 2,430
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mkuu, hakuna aliyehalalisha ufisadi bongo, sema wanatumia ujinga wetu kufanya huo ufisadi. Hamtakiwi kukata tamaa namna hii, lazima wananchi tuwe wakali kwa kupiga vita ufisadi kama huu unaondelea hapo Makongo, tukikaa kimya ndivyo nao watazidi kutuangamiza.
   
Loading...