tikatika
JF-Expert Member
- May 6, 2011
- 2,330
- 4,115
Kumeibuka utaratibu ambao watuhumiwa huvishwa mabango na kupigwa picha kisha kubandikwa police.
Mabango yanakua na maandishi ya kosa lako .
Kwa mfano wewe ukituhumiwa kwa wizi bango linaandikwa
[ mimi naitwa fulani ni mwizi wa kitu fulani]
Au.[mimi naitwa fulani ni mchochezi]
Je ni sawa kwa police kuwaita watuhumiwa ni watendaji wa kosa fulani??
Je kisheria ni sawa police kutumia mfumo huo?
Kumbuka police hawana haki ya kuthibitisha kosa la mtu bali mahakama. Je police wakibandika mimi ni mwizi na picha zangu zikasambaa katika mitandao, baadaye nikapelekwa mahakamani nikashinda kesi itakuaje? Police watanisafishaje? Mwenye mamlaka ya kumtia mtu hatiani ni mahakama tu! Kwann police waniite mchochezi baadaye nikaachiwa huru na huku nimedhalilishwa?? Haya mabango ni udhalilishaji wa haki za binadamu.
Tuwapinge police kutuvisha mabango na kutupiga picha hawana haki hiyo kisheria niwadhalilishaji.