Huu ni mwisho wa Ze Comedy au ni Mkataba umeisha au wakiingia TBC watakuwa huru tena

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Na Rehema Mohamed

KUNDI maarufu la sanaa za maigizo The Comedy limemaliza mkataba wake na kituo cha televisheni cha East Afrika (EATV) kinachorushwa kila siku ya Alhamis.

Kutokana na kumalizika mkataba huo kipindi hicho maarufu hakitarushwa kuanzia Alhamis ijayo. Kundi hilo liliingia mkataba wa mwaka mmoja na miezi nane kufanya kazi na EATV uliofikia ukingoni juzi.

Ukiondoa Ze Comedy, naye Mratibu wa kundi hilo Sekioni David amesitisha mkataba na kituo hicho na sasa anaelekeza nguvu zake ndani ya kundi hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi hilo, Isaya Mwakilasa (Wakuvanga) alisema wameamua uamuzi huo ili kupata mapumziko kwa muda kabla ya kuendelea na sanaa hiyo.

Mwakilasa alisema wanasikitika kumaliza mkataba na EATV na hivyo wameamua kurudi nyumbani kujipanga upya lakini pia wanaweza kuingia mkataba mpya endapo watakubaliana.

"Mkataba wetu na EATV umeisha nasi tumeamua kurudi nyumbani kupumzika kwa nia njema, hasa kwa maslahi ya wengi zaidi na tulikuwa tukifanya kazi nao vizuri na huu si mwisho wetu," alisema Mwakilasa.

Mwakilasa alikanusha taarifa kuwa Ze Comedy lina mpango wa kuingia mkataba mpya na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC 1) na kuongeza kuwa sanaa ni ajira yao hivyo kama watahitajika hawasita kuingia mkataba na kituo hicho.

Kundi hilo limejipatia umaarufu mkubwa ndani na nje ya Tanzania kutokana na ubunifu wao ikiwa ni pamoja na kuwakosoa baadhi ya viongozi wa Serikali wanaokwenda kinyume na maadili ya kazi.

Kundi la The Comedy linaundwa na wasanii sita ambao ni Joseph Shamba 'Vengu', Alex Chalamila 'McRegan', Mjuni Syliveri 'Mpoki', Emmanuel Mgaya 'Masanja', Lucas Mahuvile 'Joti na Mwakilasa.
 
Kawaida sehemu yoyote kukiwa na mazingira ya kuendeleza mkataba pande mbili hazisubiri mkataba uishe kwanza zinaongea kabla ya muda.

Naingia wasiwasi mkuu kwamba jamaa watachomoa pale IPPMedia..

Yetu macho, lakini huwa kuna tetesi kwamba pale mahali masilahi huwa mmmmhhhh!!!

Sina ushahidi lakini wakuu!!!


Kuna ukweli pia uliowazi kwamba TBC1 inatisha vituo vingine!!! Jamaa taarifa za habari zao zinaangalia pande zote ndio ziende hewani... kwa hakika zinafurahisha taarifa za habari zao... mimi nimehamia huko....
 
hata huko wanakokimbilia wanaweza wakalilaliwa vilevile, inategemea wataingia mkataba wa aina gani. Nimesikitika niliposikia kuwa kwa mujibu wa mkataba uliokwisha, haki miliki ya walichokionyesha inabaki EATV!
 
hata huko wanakokimbilia wanaweza wakalilaliwa vilevile, inategemea wataingia mkataba wa aina gani. Nimesikitika niliposikia kuwa kwa mujibu wa mkataba uliokwisha, haki miliki ya walichokionyesha inabaki EATV!

Nadhani mimi sisikitiki kwa sababu moja!!! Kwamba tusisahau kwamba kituo hicho hata kama kimewanyonga lakini ndio kimewatoa kwa maneno ya kijiweni...

Sasa wanaweza kutoka wenyewe wanatakiwa kuingia mkataba mzuri... Tatizo la wasaniii wetu huwa wanadhani ukiweza kuigiza unaweza kuwa mwanasheria mzuri!!! Manager mzuri, negotiator mzuri... hapana wanatakiwa kutafuta watu wa kuwasaidia kwenye hizo field ili wapate jasho lao vizuri.

Mwisho wa Juma mwema!
 
Nadhani mimi sisikitiki kwa sababu moja!!! Kwamba tusisahau kwamba kituo hicho hata kama kimewanyonga lakini ndio kimewatoa kwa maneno ya kijiweni...

Sasa wanaweza kutoka wenyewe wanatakiwa kuingia mkataba mzuri... Tatizo la wasaniii wetu huwa wanadhani ukiweza kuigiza unaweza kuwa mwanasheria mzuri!!! Manager mzuri, negotiator mzuri... hapana wanatakiwa kutafuta watu wa kuwasaidia kwenye hizo field ili wapate jasho lao vizuri.

Mwisho wa Juma mwema!

Tatizo la wasanii wetu ni mawenge sana.Wao siku zote wakishatoka hawalinganishi kipato chao na kazi/huduma wanayofanya, ila wanalinganisha na matumizi ya starehe wanazofanya. Sasa wakiona mapato hayakidhi starehe zao ndipo kukimbia kunapoanza.Wanazuzuka sana na misifa wanayopata.
Wakina Muumini na Ali Choki wako wapi!!? Twanga iliwatoa wakapata majina wakaona wanapunjwa sasa mbona walijitegemea wakashindwa kuzalisha ili wajilipe inavyostahili. Wasanii wetu wanakurupuka nao sana.
 
Hata kule kwenye blogu wameziwekea loki zile clipu zao au hamjachunguza ,ebu nendeni muone kama kuna cha kujiburudisha.Limebaki tambara jeupe
 
Wakiingia TBC uhuru wako wa kumwaga nyeti dhidi ya wa CCM utakuwaje ? Ndiyo wasi wasi wangu .Maana TBC si ya Watanzania bali ni mali ya CCM kwa jina la watanzania .
 
Wakiingia TBC uhuru wako wa kumwaga nyeti dhidi ya wa CCM utakuwaje ? Ndiyo wasi wasi wangu .Maana TBC si ya Watanzania bali ni mali ya CCM kwa jina la watanzania .

Si walisema TBC ilishabadilika na kuwa objective siku hizi? Anyway, tusiandikie mate, tusubiri tuone yatakayotokea
 
Kabla ya yoote naomba wajifunze kwa waliotangulia kufanya kazi IPP, je baada ya kuondoka makali yao yalizidi ama ulitokea mfubao?

Mifano io wazi kwa KAOLE SANAA GROUP, na makundi mengine ya kuigiza yaliyomaliza mikata yao na wakafikiria kutimka kivyao.

Sidhani kama kuna mtu nangewajua kama si IPP na sidhani kama wataweza kuwa kama walivyozoeleka na wengi katika mazingira mapya (endapo kama watabadili kituo).

Unajua unapobadili kituo watu wanataraji wakuone tofauti na jinsi walivyokuwa wamezoea kukuona kule mwanzo, unapokosa jipya unapoteza umaarufu. Na kwa kuwa tuna uvivu wa kubuni hilo litakuwa shida kwa hawa ndugu.

wabadili kwa hila waone kama watafika mbali. Mimi niko hapa na vidole vyangu vime-type maneno haya.
 
Wakiingia TBC uhuru wako wa kumwaga nyeti dhidi ya wa CCM utakuwaje ? Ndiyo wasi wasi wangu .Maana TBC si ya Watanzania bali ni mali ya CCM kwa jina la watanzania .

Ukiniuliza mimi TBC1 ndio watakuwa hwana tatizo maana risk zote za kutoa uozo wa serikali zitaishia kwa mhariri wa TBC1 na wala sio kwa vijana hawa.

TBC imebadilika sana wandugu mliko Dar fualitieni taarifa zao za habari they are better off than IPP Media, Probably you can compare with Channel TEN:

The only difference i saw... TBC1 haina ushabiki... inatoa habari za pande zote...
 
Kasheshe kwa muda sasa nimejaribu kufuatilia msimamo wako naujua when it comes to mambo ya JK .TBC imebadilika hata kuliko IPP na unawalinganisha na Channel ten kumbe unawajua kwamba ni wanazi na watu wa CCM na hawapendi kuelezea Umma ukweli ? Je wanaita wanaompa support JK na CCM yake na wale wanao mpinga ama ndiyo haya ya kila siku wanaleta wale wenye mawazo karibia na wao wanayo yataka kurudha ?
 
Jamani The comeddy ni burudani naamini walikuwa wamefiti kabisa EATV maana huko burudani ndio nyumbani. Wapenda burudani walikuwa wanabanana huko toka mziki unajikuta uko ktk the commedy vinashabihiana. Ubaya wa TBC kama wataenda yanatoka mahojiano ya diwani wa nyalugusu inakuja commedy wapi na wapi. Watajikuta wanapoteza umaarufu wao maana wapenzi wa kuangalia TBC ni Prof Lipumba, Prof Mkandara, Prof ..... Dr Slaa, Dr Kamara,Dr..... na Mh Pinda, Mh Selelii, Mh Cheyo, Mh.... na ndugu Hosea, Ndugu Makamba Ndugu...... Hawa wote hawana muda wa kusimulia gengeni, kwenye daladala (maana wanamagari yao) uhodo wa jana wa the commedy. Wapenzi wa TV5 ni akina Saada, Shufa, Mwamba, Sela, Kivanda, Koni, Maimuna, Helena, Pdidy, ambao wanapanda ktk daladala na kuanza kulipuka habari za ze comeddy na kushtua genge zima ili marudio yake watahamasika kuyaona.
 
Wawe makini hawa vijana. Mimi nawatakia heri na ninatamani kuona wanafanikiwa ili waendelee kutupatia burudani yetu iliyokuwa inatuliwaza sana. Kwa mtindo wao pia, walikuwa wanashiriki katika kumkoma nyani giladi. Lakini niwakumbushe tu hawa vijana umuhimu wa historia, wajaribu kujifunza kutokana na historia na waepuke makosa yaliyowadororesha wenzao waliojaribu wanachotaka kufanya sasa. Seki mwenyewe alikuwa kwenye kikundi cha maigizo cha "Mambo Hayo", kilikuwa maarufu sana wakati ule ITV ilipoanza miaka ya 1990's. Waanzilishi walikuwa Aisha, Waridi, Sumbi na Bocha, watu wanne tu lakini walitufurahisha sana na vimbwanga vyao. Baadae kikundi kikakua wakaongezeka kina Bishanga na Richie, na baadae akina Seki wakapatia umaarufu huko. Lakini tangu "Mambo Hayo" ilipojitoa ITV kwa mbwembwe, wametokomea kusikojulikana, hakuna mafanikio tena! Mambo kama hayo pia yamewatokea kile kikundi maarufu cha Bw Jengua, sijui kimeishia wapi. Kina "Kaole" ndio hao nasikia wanasuasua. Huyu Seki na wenzie wamejiandaaje yasiwapate ya kuwatokomeza?
 
Tatizo hawa ndugu zetu wakishapata mfadhili basi hujisahau kabisa na kuona wamefika ,maana kama akina Bob Marley na wavuta bangi wengine wangelitegemea mfadhili basi leo tayari wangelikwisha sahauliwa , Bob alijitegemea kwa kila kitu na hadi hii leo tokea tape ,zikaingia kideo ,zikafika disk na sasa kuna blue ray Bob anaibuka nazo na bei mbaya haswa ukikutana na genuine version..inahitajika hawa watu nao waamshwe waache kutegemea hivi hawakumsikia Mwalimu Nyerere aliposema Ujamaa na kujitegemea sijui walimfahamu vipi Ila kila aliechagua ujamaa mwisho wake anasambaratika na wale wanaofuata mrengo wa kujitegemea bado wanatweta na kupeta . Kauli ya Mwalimu hiyo kama hamkuifahamu ndio nimewamegea kidogo tu.
 
Taarifa ni kwamba, hawa wamechukuliwa ili kuwamaliza. Watakula raha kwa muda wa miezi sita tu, watakua wamekwisha..... Alichukuliwa Pascal Mayala, na kiti moto chake, kiko wapi? TUSUBIRI MIUJIZA
 
Pascal Mayala Siku Hizi Yupo Kama Kawaida Anaendeleza Fani Lakini Siku Hizi Zaidi Anatengeneza Filamu Haswa Zinazohusu Mazigira Na Kadhalika Kama Umemuona Siku Za Karibuni Haendeshi Tena Ile Piki Piki Sasa Hivi Ana Gari Moja Nzuri Nzuri Inaonyesha Ameanza Kupata Mafanikio Kidogo .

Ningekuwa Mimi Kwanza Ningeenda Kusoma Zaidi Masuala Ya Sanaa Mikataba Na Kadhalika Kisha Nirudi Tena Hewani Kama Kawaida .

Vijana Hawa Sijui Kama Wamesomea Masuala Ya Sanaa Na Uigizaji Hata Seki Mwenyewe Sijui Kama Ana Ujuzi Au Elimu Na Masuala Hayo

Wawe Makini Sana Nawashauri Wakaongeze Ujuzi Kisha Waje Upya Na Wakati Huu Wawe Na Meneja Wao Kabisa Awatengenezee Filamu Kisha Wawauzie Hao Wenye Vituo Vya Tv Na Mitaani
 
Hawa vijana kwa sasa wanachofanya ni kutingisha kiberiti ili terms za mkataba ziboreshwe.Sasa hivi wameshajitengenezea jina na wana kila sababu ya kudai mkataba ulioboreshwa toka ITV kwa jinsi ambavyo wameweza kuongeza idadi ya watazamaji na matangazo kwenye kituo hicho, kama ITV hawataki kuongeza dau kuna vituo vingine vya TV vitawachukua for sure.
 
Kuna wakati mwaka jana niliandika hapa .Nilikaa chini na Masanja nikaongea naye .Alisema haya .Mzee Lunyungu kaka yangu usituone hapa .Kila tukiwa studio huwa hatuamini kama next day titakuwa salama .Maana tunapata vitisho sana toka kwa wakubwa serikalini na hasa tukiwa kandamiza pale .So ni kazi ngumu na inahitaji moyo .Je CCM kama kawaida wamesha nyoosha mkono?Lazima niangalie mbali zaidi ya mkataba .

Na kwa shy mpuuzeni anataka wenzake wakasome na yeye anaendeleza u snitch ? Si uende nawe ukasome ukomae akili uachana na u snitch ?
 
Back
Top Bottom