Huu ni Mwezi wa pili sasa tangu Ngeleja... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huu ni Mwezi wa pili sasa tangu Ngeleja...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Apr 20, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,418
  Likes Received: 81,463
  Trophy Points: 280
  ....atutangazie Watanzania kwamba Sakata la Mkapa kujiuzia Kiwira litaanikwa hadharani hapo February 18, 2009.

  Ngeleja kufichua siri ya Kiwira

  na Kulwa Karedia
  Tanzania Daima~Sauti ya watu


  SERIKALI imesema imejiandaa kuanika ukweli na hatima ya mgodi wa mawe wa Kiwira, wakati wowote kuanzia sasa kwa maslahi ya taifa.

  Akitoa taarifa ya serikali kwa waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam jana kuhusu kuuzwa kwa asilimia 75 za kampuni ya Williamson Diamond, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, alisema serikali imekamilisha kukusanya taarifa za mgodi huo ambao majibu yake yanasubiriwa na Watanzania wengi.

  “Napenda kuwaambia kwamba kila kitu juu ya mgodi huu kimekamilika, ni matumaini yangu kwamba wakati wowote kuanzia sasa tutaanika ukweli na hatima ya mgodi huu ambao umezua mambo mengi katika siku hivi karibuni,” alisema Waziri Ngeleja.

  “Hatuna sababu ya kuchelewesha suala hili, tuko tayari kufafanua mambo yote yaliyofanyika na yale ambayo tunaona yana faida kwa taifa katika siku zijazo,” alisema Waziri Ngeleja.

  Serikali haitakaa kimya kwani katika mkutano wa 14 wa Bunge uliomalizika wiki iliyopita mjini Dodoma, suala hili lilikuwa limewekwa kwenye orodha ya kujadiliwa lakini ilishindikana kutokana na muda.

  “Baada ya suala hili kutojadiliwa bungeni, watu wanaweza kusema tumeingia ‘mitini’…nasema ndugu zangu hapana…tupo pamoja kwa nia ya kujenga taifa letu,” alisema Ngeleja.

  Katika hatua nyingine, Ngeleja alisema serikali imeridhia uuzaji wa asilimia 75 za kampuni ya Williamson Daimonds Limited zilizokuwa zinamilikiwa na kampuni ya Willcroft Limited.

  Alisema baada ya uchunguzi wa kina kufanyika, serikali imeridhia kuuza kiasi hicho kwa kampuni ya Petra Diamond ambayo iliingia mkataba wa kununua kampuni ya Willcoft Limited.

  “Baada ya kupokea ushauri wa kamati ya wataalamu wa kisekta ya serikali na ule wa kamati ya ushauri ya Jaji Mark Bomani na kujiridhisha kuwa mbia, Petra Diamond ina uwezo wa kuendesha mgodi wa almasi, serikali imeona kampuni hiyo haina kikwazo, hivyo kukabidhiwa mgodi,” alisema Ngeleja.

  Masharti yaliyowekwa na serikali ni pamoja na Petra Diamond itambue mikataba iliyopo kati ya serikali na Willcroft na kuendeleza majadiliano ya kurekebisha hali ya mgodi huo ili uweze kuleta manufaa zaidi kwa taifa.

  Alisema serikali itaendelea na majadiliano na mbia wake huyo kupitia upya mkataba wa wanahisa ili uendane na wakati uliopo kwa manufaa ya pande zote.

  “Majadiliano yatahusu pia mradi wa upanuzi wa shughuli za uzalishaji wa almasi ili mgodi uweze kuzalisha kati ya karati 500,000 na 1,000,000 kwa mwaka badala ya 200,000 zinazozalishwa hivi sasa,” alisema Ngeleja.

  Serikali itahakikisha maslahi ya wafanyakazi wa mgodi huo yanalindwa na Petra itaendeleza miradi na huduma za kijamii zilizokuwa zinatolewa na kampuni ya De Beers na mradi wa Mwadui Community Diamonds Partenership (MCDP), unaohusu kuwaendeleza wachimbaji wadogo wa eneo la Mwadui.
   
 2. O

  Ogah JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Ngeleja hana kifua.........tusiwekane roho juu........kaandaliwa taarifa "ya kusawazisha" naye anakuja kuisoma
   
 3. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Ogah heshima yako,

  "Mkuu alikuwa safari ajamwaga wino kwenye hiyo report!". Tunato safari ndefu kuelekea kwenye utawala wa sheria...

  Lakini naona kama 'Mh.' Mramba kisha anza kutoa boriti za kwenye 'pandora box'
   
Loading...