WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,459
- 952
Katika hali ya kawaida, mwakilishi wa wananchi mfano Mbunge au kiongozi mwingine wa kutumikia watu huchaguliwa kutokana na kukamilisha vigezo kama vile utendaji uliotukuka, uchapa kazi unaoendana na uadilifu, umakini, usikivu nk.
Aidha kunaweza kuwepo na kigezo kingine cha "affirmative action" kwa maana ya kutoa fursa kwa makundi maalum, ili kuhakikisha wale walioko pembezoni ( marginalised) kwa sababu ya pamoja na mambo mengine jinsia/jinsi, ulemavu, umri nk.
Uchaguzi wa mwaka huu umenipa somo kuwa inawezekana mtu akapata kura tena za kutosha kwa vile "anaonewa huruma". Mfano mzuri ni hoja ya baadhi ya wachambuzi wa mambo wanaosema kuwa Mrema wa TLP alichaguliwa kwa sababu "alionewa huruma" na wapiga kura kutokana na afya yake na kwamba akiwa bungeni basi ataweza kupata matibabu nk.
Hili linanitatiza kidogo, na kuniachia swali - hivi ni kwanini tunahitaji uwakilishi bungeni? Tunachaguwa wabunge wakajiwakilishe wenyewe kwa maana ya kutatua matatizo binafsi au tunawachagua ili kuweza kuratibu maswala ya mbalimbali ya maendeleo yenye kuhitaji ufumbuzi wa kimkakati - ikiwemo kufikisha kunakohusika? Nijuavyo mimi mbunge ni mjumbe wetu tunayemtuma akatusemee maana watanzania wote milioni zaidi ya 40 hatuwezi kujipeleka bungeni tukaseme kila kinachotuhusu au kutukera.Ingekuwa vurugu na haiwezekani kamwe.Mjumbe huyu tunamtarajia atufikishie yale tunayomtuma kama yalivyo na atuletee jibu pia!
Najaribu kufikiria - endapo Mrema atatumia fursa hiyo kwa manufaa binafsi kama "ilivyobarikiwa" na wapiga kura wake ( tuseme asilimia 60 ya wana-Vunjo waliopiga kura) je wale ambao hawakumchagua wakiwemo wa vyama pinzani, na walioshindwa kupiga kura kwa sababu mbalimbali ikiwemo kutokuwa na sifa ya kupiga kura kwa mfano watoto chini ya miaka 18, watawakilishiwa vipi maslahi yao?
Swali lingine la jumla ni kwamba, mbunge ni mwakilishi wa wale tu waliompigia kura? au ni mwakilishi wa watu wote? Kama ni wa watu wote kuna sababu kwa walioshinda kuwa na viburi na kutoa kauli za kukatisha tamaa au hata kubeza kuzielekeza kwa wale wanaohisiwa hawakutoa ushirikiano? nadhani hili halieleweki vizuri kwa watu wengi.
Naomba tujadili hili maana nadhani inabidi watanzania tuelewe zaidi ya tujuavyo na JF kuna magwiji wa uchambuzi watatupiga darasa.
Nawakilisha.
Asanteni