Huu ni mwaka wa hasara kwa wakulima

Mk
Poa poa mkuu. Kwahiyo ni wilaya gani ili nijue hiyo sehemu siku nikija nisipate shida?
Mkuu njoo manchali.chalinze wilaya ya Chamwino gunia elfu30,Kigea Chimaligo Chunyu Wilaya ya Mpwapwa Bei ni debe 4000/gunia 24,000/
 
Hali ni mbaya sana!

Licha ya uchumi wa watanzania wengi kutegemea kilimo cha kutegemea neema za Mwenyezi Mungu kupata riziki zao lakini bado hali ya masoko imekuwa mbovu sana.

Katika hali ya kusikitisha sana mwaka huu sio mzuri sana kwenye mavuno hivyo uwezekano wa waliowekeza kwenye kilimo kupata hasara upo kwa kiasi kikubwa.

Mbaya zaidi hali ya upatikanaji wa masoko imekuwa mbovu zaidi kuwahi kurekodiwa katika kipindi cha mwongo mmoja uliopita.

Kuna baadhi ya watu watakuja hapa kuona kwamba hiyo ni hali nzuri kwao kuona kwamba mazao ya chakula na biashara hayana bei lakini wasisahau kuwa kilimo kinatumia mitaji na kama kinatumia mitaji maana yake ni sehemu ya uwekezaji. Mfano kwa sasa gunia la mahindi halizidi tsh.25000/= katika maeneo mengi nchini hususan maeneo ya vijijini, pia gunia la maharage halizidi 120000/= katika maeneo mengi ya vijijini yanapolimwa. Bado hatujui hali ya mbaazi na mazao mengine katika maeneo tofauti tofauti hapa nchini.

Je, watanzania wenzangu nini kifanyike ili angalau kuwezesha sisi wakulima tuweze kujifuta machozi kwa mwaka huu? Maoni yenu kwenye jukwaa hili ni ya muhimu sana kwani kwa zaidi ya 80% ya watanzania huwa wanategemea kilimo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Naamini suluhisho la peke kwa serikali kufungua milango ya kupeleke cha kula nje ya nchi , kuliko kukomaa na wakulima kuuza hapa nchi .
 
Hali ni mbaya sana!

Licha ya uchumi wa watanzania wengi kutegemea kilimo cha kutegemea neema za Mwenyezi Mungu kupata riziki zao lakini bado hali ya masoko imekuwa mbovu sana.

Katika hali ya kusikitisha sana mwaka huu sio mzuri sana kwenye mavuno hivyo uwezekano wa waliowekeza kwenye kilimo kupata hasara upo kwa kiasi kikubwa.

Mbaya zaidi hali ya upatikanaji wa masoko imekuwa mbovu zaidi kuwahi kurekodiwa katika kipindi cha mwongo mmoja uliopita.

Kuna baadhi ya watu watakuja hapa kuona kwamba hiyo ni hali nzuri kwao kuona kwamba mazao ya chakula na biashara hayana bei lakini wasisahau kuwa kilimo kinatumia mitaji na kama kinatumia mitaji maana yake ni sehemu ya uwekezaji. Mfano kwa sasa gunia la mahindi halizidi tsh.25000/= katika maeneo mengi nchini hususan maeneo ya vijijini, pia gunia la maharage halizidi 120000/= katika maeneo mengi ya vijijini yanapolimwa. Bado hatujui hali ya mbaazi na mazao mengine katika maeneo tofauti tofauti hapa nchini.

Je, watanzania wenzangu nini kifanyike ili angalau kuwezesha sisi wakulima tuweze kujifuta machozi kwa mwaka huu? Maoni yenu kwenye jukwaa hili ni ya muhimu sana kwani kwa zaidi ya 80% ya watanzania huwa wanategemea kilimo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kushuka bei ya chakula ni neema.
 
Back
Top Bottom