Huu ni mwaka wa 5 sasa eneo la Pembamnazi Kigamboni, barabara hazijachongwa

vamda

JF-Expert Member
Aug 1, 2012
713
500
Habari wakuu,

Mnamo 2016 serikali kupitia wizara ya ardhi iliuza viwanja eneo la Pembamnazi (Kigamboni) jijini Dar es Salaam.

Huu ni mwaka wa 5 sasa barabara hazijachongwa. Wenye viwanja wanashindwa kujenga maana hakuna barabara za kupita magari kupeleka vifaa vya ujenzi. Na bado wenye viwanja wanalazimishwa kulipa kodi kila mwaka pamoja na faini wanapochelewa kulipa.

Serikali, kwa vile ndio iliyouza viwanja hivyo eneo hilo, itoe tamko tatizo liko wapi na litatatuliwa lini badala ya kukaa kimya.

Mhe. Lukuvi tunaomba ufuatilie ili kama kuna hujuma hapo wizarani wahusika wachukuliwe hatua kali. Haiwezekani huu ni mwaka wa 5 sasa eneo la Pembamnazi barabara hazijachongwa.

Nawasilisha.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom