Huu ni muda sahihi wa viongozi wetu wa kisiasa kutuongoza kudai Katiba Mpya

Jul 23, 2018
46
66
Mchakato wa Katiba Mpya sote tunafahamu ulivyoenda na ulivyoharibiwa na "wahuni" wachache wasiolipenda Taifa letu la Tanzania.
Kwa kipindi cha miaka mitano (2015-2020) suala la Katiba Mpya limepuuzwa kabisa na aliyekuwa Rais wa wakti huo.

Viongozi wetu wa kisiasa walijaribu kulipenyeza lakini Magufuli akaligomea kabisa huku akisema "siyo kipaumbele chake".

Sasa tunaye Rais Mhe. Mama Samia Suluhu ambaye katika Bunge la Katiba alihudumu kama Naibu wa Spika (Makamu Mwenyekiti) wa Bunge la Katiba.
Pia katika hotuba zake tangu amekuwa Rais, amekuwa akitaja sana Katiba Mpya. Hii ni ishara ya kwamba tunahitaji nguvu kidogo tu za Viongozi wetu wa kisiasa kuisukuma agenda hii muhimu katika Taifa letu la Tanzania.

Lakini jambo muhimu la kukumbuka ni hili; kwamba tudai mchakato uanzie kwenye Rasimu ya pili ya Katiba pendekezwa iliyobeba maoni sahihi ya Wananchi.
Rasimu ya pili yenye jumla ya Ibara 271 ambayo ilikabidhiwa mwezi December 30, 2013. Hii ndiyo Rasimu yenye maoni ya Wananchi.

Rasimu ambayo kwa mfano, ukizingatia maoni ya Wananchi juu ya suala la Muungano maoni ya Wananchi yalikuwa hivi;

13% - Wananchi waliohojiwa kutoka Tanzania Bara (Tanganyika) walipendekeza kuwepo na Serikali moja.
24% - Wananchi waliohojiwa kutoka Tanzania Bara (Tanganyika) walipendekeza kuwepo na Serikali mbili.
61% - Wananchi waliohojiwa kutoka Tanzania Bara (Tanganyika) walipendekeza kuwepo na Serikali tatu (yaani Serikali ya Tanganyika, Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Muungano)

Lakini pia;
0.1% - Wananchi waliohojiwa kutoka Zanzibar walipendekeza kuwepo na Serikali moja tu.
34% - Wananchi waliohojiwa kutoka Zanzibar walipendekeza ziwepo Serikali mbili.
60% - Wananchi waliohojiwa kutoka Zanzibar walipendekeza kuwepo na Serikali ya Muungano wa Mkataba.

Hii ndiyo ilikuwa Rasimu ya Wananchi maarufu kama Rasimu ya Warioba. Hii ndiyo tunayoihitaji kwa mujibu wa maoni ya Wananchi.
Pamoja na maoni hayo mazuri ya Wananchi, lakini kikundi cha watu wachache kiliingilia mchakato ule na kuuharibu kwa "kupuuza" na "kunyofoa" maoni ya Wananchi kulingana na matakwa yao.

Tunawaomba Viongozi wetu wakuu wa Kisiasa watuongoze kama Taifa katika kudai mchakato huu uanze upya kuanzia Bunge la Katiba kwa kuanza na Rasimu ya Warioba.

Tunaomba wanaharakati na wanasheria watusaidie kutimiza jukumu hili muhimu katika jamii.

Tumeshampata Rais, sasa ni wajibu wetu kumkumbusha afanye nini juu ya Katiba yetu ya Taifa la Tanzania.

Mohonia JP
 
Tatizo wakubwa wanaposhika madaraka wanajisahau wakijiona wamekuja duniani kuishi milele na siyo kuandaaa urithi mzuri wa vizazi vya baadaye na muelekeo mzuri utakaowasaidia Kama wao walivyotengenezewa katiba na taasisi japo ni za watu wa enzi hizo lakini zinawaongoza waongoze kizamani lakini kutengenezea vizazi vyao na wajukuu hawataki wamebaki kujiona wataishi milele hata hili lililotokea haliwashitui wakajirekebisha wakaungana kutuletea katiba mpya na taasisi imara wakiamini wataishi milele ila wengi wao umri umekwenda tena wa kustaafu na kulea wajukuu Ila neema ya Mungu wamepata Ili wawepo kwenye kuongoza lakini wameziba masikio wakijiona watoto na Wala hawataki kuandaa urithi mzuri kwa Taifa lao.
 
"....nadhani wameni push push sana, katibaaa katiba lakini wasahau kidogo" - Rais Samia Suluhu Hassan
 
Back
Top Bottom