paul sylvester
JF-Expert Member
- Mar 18, 2020
- 3,504
- 3,499
Kutokana na uzembe maofisini, Ni vyema sasa Mfumo wa ajira ukabadilika haraka iwezekanavyo.
Mfumo ambao upo, umewafanya watu kuzoea kazi ili hali huko nje kuna watu wachapa kazi na hawajapata chansi ya wapi wakatumikie taifa lao.
Mfumo uliopo, ndio ulioleta uzembe maofsini, Kwa sababu mtu akiajiriwa ndio basi, yeye anachojali ni mshahara wake mwisho wa mwezi.
Mfumo uliopo, ndio unaolifanya Taifa letu kuwa ombaomba kwa kuwa watu hawafanyi kazi maofsini, watoto wetu hawafundishwi mashuleni na wafanyakazi hawana wasi kwa kuwa wao wanajua, mtu ukishaajiriwa na Serikari, hiyo inakuwa ni ajira ya kudumu tofauti kabisa na ilivyo kwenye sekita binafsi, na ndiyo maana sekta binabisi zinafanya vizuri sana.
Watu Wenye uchungu na nchi yao, haiwezekani vyoo vya shule vichakae hadi viwe tishio Kwa watoto, eti hakuna kiongozi ambaye kaona hali hiyo, badala yake Ubalozi wa nchi fulani ndio waje kuona hali hiyo mbaya katika maeneo ambayo, mkuu wa wilaya anakaa, Mkurugenzi yupo, Mbunge yupo, makatibu tarafa, maafsa Elimu, walimu wakuu wapo, na mazingira hayo wanayaishi!! Hii Maana yake ni nini kama sio mfumo wa ajira kuwa hautufai kwa sasa.
Tunataka mfumo wetu wa ajira, waajiriwa wajaze mkataba wa angalau miaka mitatu mitatu baada ya hapo waombe tena, hii itasaidia watu kuheshimu kazi zao.
Mfumo wetu huu tulionao, ndiyo umetufikisha hapa tulipo, watu hawaheshimu muda wa kazi, watu hawafanyi kazi, wapo wapo tu maofsini, ubunifu wao hautufaidii chochote kwa kuwa wanajua mkataba wa kazi zao ni hadi mtu unastaafu.
Hovyo sana aisee!!