Huu ni muda mwafaka sasa kwa Serikali kuwaajiri Watumishi wote wa umma kwa mkataba maalumu!

paul sylvester

JF-Expert Member
Mar 18, 2020
3,455
2,000
Kutokana na uzembe maofisini, Ni vyema sasa Mfumo wa ajira ukabadilika haraka iwezekanavyo.

Mfumo ambao upo, umewafanya watu kuzoea kazi ili hali huko nje kuna watu wachapa kazi na hawajapata chansi ya wapi wakatumikie taifa lao.

Mfumo uliopo, ndio ulioleta uzembe maofsini, Kwa sababu mtu akiajiriwa ndio basi, yeye anachojali ni mshahara wake mwisho wa mwezi.

Mfumo uliopo, ndio unaolifanya Taifa letu kuwa ombaomba kwa kuwa watu hawafanyi kazi maofsini, watoto wetu hawafundishwi mashuleni na wafanyakazi hawana wasi kwa kuwa wao wanajua, mtu ukishaajiriwa na Serikari, hiyo inakuwa ni ajira ya kudumu tofauti kabisa na ilivyo kwenye sekita binafsi, na ndiyo maana sekta binabisi zinafanya vizuri sana.

Watu Wenye uchungu na nchi yao, haiwezekani vyoo vya shule vichakae hadi viwe tishio Kwa watoto, eti hakuna kiongozi ambaye kaona hali hiyo, badala yake Ubalozi wa nchi fulani ndio waje kuona hali hiyo mbaya katika maeneo ambayo, mkuu wa wilaya anakaa, Mkurugenzi yupo, Mbunge yupo, makatibu tarafa, maafsa Elimu, walimu wakuu wapo, na mazingira hayo wanayaishi!! Hii Maana yake ni nini kama sio mfumo wa ajira kuwa hautufai kwa sasa.

Tunataka mfumo wetu wa ajira, waajiriwa wajaze mkataba wa angalau miaka mitatu mitatu baada ya hapo waombe tena, hii itasaidia watu kuheshimu kazi zao.

Mfumo wetu huu tulionao, ndiyo umetufikisha hapa tulipo, watu hawaheshimu muda wa kazi, watu hawafanyi kazi, wapo wapo tu maofsini, ubunifu wao hautufaidii chochote kwa kuwa wanajua mkataba wa kazi zao ni hadi mtu unastaafu.

Hovyo sana aisee!!
 
Kinyungu

JF-Expert Member
Apr 6, 2008
10,774
2,000
Mkuu, unaonaje mfumo tulionao mkuu.
Huu mfumo uko vizuri sana. Tena waongeze muda wa kustaafu uwe miaka 65 au 70 kwa sababu tumefika uchumi wa kati maisha ya wananchi hasa watumishi yameboreka sana. Mstaafu wa miaka 60 ni kama mtu mwenye miaka 45 au 50.

Tukiongeza muda wa kustaafu itaisaidia serikali kupunguza mzigo wa pension kwa wastaafu kwa maana wastaafu watapungua na wakistaafu muda wao wa kuishi utakuwa kidogo
 
paul sylvester

JF-Expert Member
Mar 18, 2020
3,455
2,000
Na bado ndio mitano inaanza January mosi! Mtalia mmoja baada ya mwingine na bado hamtasikika! Mlipowmbiwa ccm ni shida mkajifanya viziwi na Leo unaongea habari ya choo Cha shule!
Endelea kuunga juhudi!
Wewe sasa uko salama?
 
denhoo

Member
Sep 11, 2016
83
150
Kutokana na uzembe maofisini, Ni vyema sasa Mfumo wa ajira ukabadilika haraka iwezekanavyo.

Mfumo ambao upo, umewafanya watu kuzoea kazi ili hali huko nje kuna watu wachapa kazi na hawajapata chansi ya wapi wakatumikie taifa lao...
Pamoja na hayo lazima ukae chini ujiulize kwanini watu wanafanya kazi kwa mazoea, nilifanya kazi serikali miaka hyo nikaona najidumaza kiakili.

kwa uzoefu wangu nilichokiona serikali

1. Hakuna vitendea kazi huko unakutwa mtu umeajiriwa kama afisa mifugo dawa za mifugo unategemea anunue mwananchi umtibie ukinunua ww kashifa serikalini utasubir dokezo la hela ya dawa hadi ustaafu mazoea hayataacha kuisha

2. Mtu unaajiriwa hakuna semina elekezi ukipangiwa kituo ndio utajielewa mwenyewe hukohuko

3. Siasa uchwala ukileta utaalamu wako, utapigwa mizengengwe hadi uhame

4. Unaajiriwa hujui rushwa ukifika kazini wananchi utasikia tumuia ubinadamu yaishe nje na hapo nilipofanyia kazi utasumbuliwa ww na familia yako hadi na ww uanze kuwanga ukikubali unajikuta umefikia level ya mapapa wakubwa kwenye ufisadi

5. Mtu anapigishwa kazi weekend hakuna extra deuty wala nn ni mazoea pia

Kwa uchache mazoea yanaanza kuanzia kuajiriwa kupangiwa kituo, kupata masilahi, hata mikataba ikija bussiness as ussual tena huko ndio watu watapiga mihela na kusepa
 
Man Mvua

JF-Expert Member
Apr 12, 2016
1,727
2,000
Pamoja na hayo lazima ukae chini ujiulize kwanini watu wanafanya kazi kwa mazoea, nilifanya kazi serikali miaka hyo nikaona najidumaza kiakili
kwa uzoefu wangu nilichokiona serikali...
Upo sahihi sana boss. Kwa mfano ajira mpya za walimu.

1. Wamepangiwa vituo vya kazi wameripoti halafu hakuna chochote kilichoendelea yaani watajijua menyewe.

2. Hawajapewa mshahara wa pesa zao za kujikimu na wengine walienda kama walivyo huko vituoni hivyo kuwa na hali ngumu sana halafu baadae mnataka ajitume ili alete ufanisi hali ya kuwa mlimtelekeza mwanzo.

3. Hakuna semina, posho, per diem, uhamisho ugomvi, pesa ya mazingira magumu hakuna wala nyumba za watumishi.

4. Ongezeko la mshahara na kupanda madaraja hakuna miaka sita LAZIMA MTU ASIFANYE KAZI IPASAVYO.

USHUHUDA:
Nina rafiki yangu miaka 6 hajaongezewa mshahara wala kupanda daraja aiseee YUPO ILIMRADI YUPO siwezi hata kuongea.

SERIKALI ITIMIZE WAJIBU WAKE KWANZA.
 
kson m

JF-Expert Member
Jan 24, 2014
5,729
2,000
Kutokana na uzembe maofisini, Ni vyema sasa Mfumo wa ajira ukabadilika haraka iwezekanavyo.

Mfumo ambao upo, umewafanya watu kuzoea kazi ili hali huko nje kuna watu wachapa kazi na hawajapata chansi ya wapi wakatumikie taifa lao.

Mfumo uliopo, ndio ulioleta uzembe maofsini, Kwa sababu mtu akiajiriwa ndio basi, yeye anachojali ni mshahara wake mwisho wa mwezi.

Mfumo uliopo, ndio unaolifanya Taifa letu kuwa ombaomba kwa kuwa watu hawafanyi kazi maofsini, watoto wetu hawafundishwi mashuleni na wafanyakazi hawana wasi kwa kuwa wao wanajua, mtu ukishaajiriwa na Serikari, hiyo inakuwa ni ajira ya kudumu tofauti kabisa na ilivyo kwenye sekita binafsi, na ndiyo maana sekta binabisi zinafanya vizuri sana.

Watu Wenye uchungu na nchi yao, haiwezekani vyoo vya shule vichakae hadi viwe tishio Kwa watoto, eti hakuna kiongozi ambaye kaona hali hiyo, badala yake Ubalozi wa nchi fulani ndio waje kuona hali hiyo mbaya katika maeneo ambayo, mkuu wa wilaya anakaa, Mkurugenzi yupo, Mbunge yupo, makatibu tarafa, maafsa Elimu, walimu wakuu wapo, na mazingira hayo wanayaishi!! Hii Maana yake ni nini kama sio mfumo wa ajira kuwa hautufai kwa sasa.

Tunataka mfumo wetu wa ajira, waajiriwa wajaze mkataba wa angalau miaka mitatu mitatu baada ya hapo waombe tena, hii itasaidia watu kuheshimu kazi zao.

Mfumo wetu huu tulionao, ndiyo umetufikisha hapa tulipo, watu hawaheshimu muda wa kazi, watu hawafanyi kazi, wapo wapo tu maofsini, ubunifu wao hautufaidii chochote kwa kuwa wanajua mkataba wa kazi zao ni hadi mtu unastaafu.

Hovyo sana aisee!!
Wewe unafanya kazi kwa kiwango gani ? Au ni namna ya kutaka ufikiriwe kwenye ajira kwa kuchochea wenzako waondolewe kwenye ajira ?
 
Davan

JF-Expert Member
Jun 15, 2020
1,127
2,000
Serikali ni nani kwako wewe?
Huyo atakaetunga hiyo sheria na yeye itamuhusu nani atakubali kujiangamiza?
Kutokana na uzembe maofisini, Ni vyema sasa Mfumo wa ajira ukabadilika haraka iwezekanavyo.

Mfumo ambao upo, umewafanya watu kuzoea kazi ili hali huko nje kuna watu wachapa kazi na hawajapata chansi ya wapi wakatumikie taifa lao.

Mfumo uliopo, ndio ulioleta uzembe maofsini, Kwa sababu mtu akiajiriwa ndio basi, yeye anachojali ni mshahara wake mwisho wa mwezi.

Mfumo uliopo, ndio unaolifanya Taifa letu kuwa ombaomba kwa kuwa watu hawafanyi kazi maofsini, watoto wetu hawafundishwi mashuleni na wafanyakazi hawana wasi kwa kuwa wao wanajua, mtu ukishaajiriwa na Serikari, hiyo inakuwa ni ajira ya kudumu tofauti kabisa na ilivyo kwenye sekita binafsi, na ndiyo maana sekta binabisi zinafanya vizuri sana.

Watu Wenye uchungu na nchi yao, haiwezekani vyoo vya shule vichakae hadi viwe tishio Kwa watoto, eti hakuna kiongozi ambaye kaona hali hiyo, badala yake Ubalozi wa nchi fulani ndio waje kuona hali hiyo mbaya katika maeneo ambayo, mkuu wa wilaya anakaa, Mkurugenzi yupo, Mbunge yupo, makatibu tarafa, maafsa Elimu, walimu wakuu wapo, na mazingira hayo wanayaishi!! Hii Maana yake ni nini kama sio mfumo wa ajira kuwa hautufai kwa sasa.

Tunataka mfumo wetu wa ajira, waajiriwa wajaze mkataba wa angalau miaka mitatu mitatu baada ya hapo waombe tena, hii itasaidia watu kuheshimu kazi zao.

Mfumo wetu huu tulionao, ndiyo umetufikisha hapa tulipo, watu hawaheshimu muda wa kazi, watu hawafanyi kazi, wapo wapo tu maofsini, ubunifu wao hautufaidii chochote kwa kuwa wanajua mkataba wa kazi zao ni hadi mtu unastaafu.

Hovyo sana aisee!!
 
big IQ

JF-Expert Member
Dec 16, 2012
378
1,000
Nje ya mada kidogo,hivii wakuu MSHAHARA wa December umeshatoka?maana sikukuu hizi tule mbuzi na Serengeti
 
Fadhilim

JF-Expert Member
Feb 3, 2013
214
250
Nikajua baada ya vyama vya upinzani kuwekewa vizingiti kila kona ikiwemo idadi kupungua bungeni mambo haya hayatakuwepo tena.

Maana inasemekana wao walikuwa wanadidimiza maendeleo kwa kuyapinga.
Mbona anatafutwa mchawi tena na sasa wapo wapenda maendeleo.
 
steveachi

JF-Expert Member
Nov 7, 2011
6,845
2,000
Itakuwa byee sana,watulipe kwanza chetu chote kizima kizima kabla hatujauanza huo Mkataba mpya
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom