Huu ni mtazamo wangu - Nchi hii tujaribu kuwapa wachaga

Ndallo

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
7,619
4,292
Rejea heading yangu hapo juu ni kua kwa mtazamo wangu na tembea yangu Tanzania mikoa mingi palipo na kabila la mchaga lazima kuna kamaendeleo fulani na pia kama ukiwachunguza hili kabila utaona ni watu wanaopenda sana maendeleo na si kwao binafsi tu la hasha hata kwa jamii inayowazunguka! Tafadhali sana mniwie radhi sijaleta mada hii kwamba naingiza ukabila na wala mimi sio mchaga bali ni mtazamo wangu tu. Ili tuondokane na umasikini uliokidhiri hapa nchini kwetu na ndoto ya maisha bora kwakila mtanzania ni sawa na ile ndoto yakutaka kujenga gorofa angani! basi ni mchango wangu tu na mawazo yangu tu hembu tujaribu kuwatesti hawa jamaa na kama kuna mtu anapendekeza kabila jingine anakaribishwa kuchangia mada hii.
 
Hatumchagui Rais kutokana na kabila lake,Utanganyika wake,Uzanzibar wake wala Udini Wake.akijipambanua kwa hayo niliyotaja hapo juu HAFAI KUWA RAIS WA TANZANIA.%
 
Ni sawa mkubwa nimekupata, lakini maisha bora kwakila mtanzania mbona bado ni ndoto?
 
itapendeza zaidi tukiongozwa na Mramba pamoja na binamu yake Yona.
Rejea heading yangu hapo juu ni kua kwa mtazamo wangu na tembea yangu Tanzania mikoa mingi palipo na kabila la mchaga lazima kuna kamaendeleo fulani na pia kama ukiwachunguza hili kabila utaona ni watu wanaopenda sana maendeleo na si kwao binafsi tu la hasha hata kwa jamii inayowazunguka! Tafadhali sana mniwie radhi sijaleta mada hii kwamba naingiza ukabila na wala mimi sio mchaga bali ni mtazamo wangu tu. Ili tuondokane na umasikini uliokidhiri hapa nchini kwetu na ndoto ya maisha bora kwakila mtanzania ni sawa na ile ndoto yakutaka kujenga gorofa angani! basi ni mchango wangu tu na mawazo yangu tu hembu tujaribu kuwatesti hawa jamaa na kama kuna mtu anapendekeza kabila jingine anakaribishwa kuchangia mada hii.
 
Wachaga!!! Wachaga? Wachaga!!!
Tumeishiwa chakuongelea?
 
Hapa nimeamini kumbe hayati baba wa Taifa alikuwa anaona mbali ndo mana enzi zake ilikuwa huwezi upewa uhuru wakuongea. Lakini siku hizi baada ya waTZ kupewa uhuru wa kuongea siku hizi imekuwa balaaa!
 
Sio balaa! Je maandamano ndio suluhisho?
 
Wachaga!!! Wachaga? Wachaga!!!
Tumeishiwa chakuongelea?

Rejao ni mtazamo tu kwakua naoana kama naishi yale maisha aliyokua anaishi babu mzaa mababu wa wa mababu!
 
Wachaga!!! Wachaga? Wachaga!!!
Tumeishiwa chakuongelea?

Rejao! Huu ni mtazamo wangu tu lakini mimi naona kama maisha ninayo ishi ni kama yale maisha aliyokua anaishi babu yangu mzaa babu wa mababu!
 
Rejea heading yangu hapo juu ni kua kwa mtazamo wangu na tembea yangu Tanzania mikoa mingi palipo na kabila la mchaga lazima kuna kamaendeleo fulani na pia kama ukiwachunguza hili kabila utaona ni watu wanaopenda sana maendeleo na si kwao binafsi tu la hasha hata kwa jamii inayowazunguka! Tafadhali sana mniwie radhi sijaleta mada hii kwamba naingiza ukabila na wala mimi sio mchaga bali ni mtazamo wangu tu. Ili tuondokane na umasikini uliokidhiri hapa nchini kwetu na ndoto ya maisha bora kwakila mtanzania ni sawa na ile ndoto yakutaka kujenga gorofa angani! basi ni mchango wangu tu na mawazo yangu tu hembu tujaribu kuwatesti hawa jamaa na kama kuna mtu anapendekeza kabila jingine anakaribishwa kuchangia mada hii.

Eee bana una mawazo mazuri sana ila ndo hivyo si rahisi watu wakakuelewa manake watu wengi hasa kutoka yale makabila yaliyo nyuma zaidi kimaendeleo wanawaogopa wachagga sana na wamepandikizwa kitu kibaya kufikiri kwamba wachagga ni wezi.

Hii ilitokana hasa na historia ya nchi yetu wakati wa UJAMAA. Wakati ule kuwa na fedha au kuwa tajiri ilionekana kama dhambi na serikali ilikuwa inawafuatilia sana watu wenye hela na walikuwa wanatiwa matatani. Kumbuka wakati ule hata kuwa na nyumba ya kupanga ulikuwa unaonekana fisadi na kama una nyumba 2 ndio usiseme utaeleza umepata wapi pesa za kujenga.

Sasa hawa ndugu zetu wachagga wengi walishaingia kwenye biashara tangu zamani na walikuwa na pesa na walijenga majumba makubwa kwao na mijini pia. Kilichotokea watu hawakuweza kutambua walipata fedha wapi kwani watu wengi walikuwa hawajishughullishi na biashara waliona kama uhuni au wizi.

Ni kweli ukienda uchaggani kuna maendeleo sana. Kulingana na takwimu hasa za miaka ya sitini na sabini ulikuwa huwezi kufananisha Moshi na sehemu nyingine Tz na hadi sasa Kilimanjaro vijijini hakuwezi kufananishwa na sehemu nyingine yeyote vijijini kiujumla kuna maendeleo sana.

Nakumbuka wakati fulani waliandika katika kitabu kwamba MOSHI IS A DEVELOPED AREA IN A DEVELOPING COUNTRY. kwamba Moshi ni kama nchi iliyoendelea ndani ya nchi maskini.

Serikali tangu enzi za Nyerere ilifanya makusudi makubwa sana kuwazuia wachagga wasiendelee kwa kasi waliyokuwa nayo, lakini voingozi wengi walishangazwa na waha akina Mangi kwani ndio walifanya juhudi zaidi.

Nyerere aliwaogopa sana Wachagga kwani ndio waliokuwa mstari wa mbele kupinga sera za kimaskini za Ujamaa. wapo wengi tu waliopingana na Nyerere na ili kujilinda Nyerere alichofanya ni kuwafukuza serekalini. Mfano ni Edwini Mtei ambaye alitaka mabadiliko kutoka Ujamaa miaka ya 70 lakini mwisho wake Nyerere alimwona hatari kwa Ujamaa na aliishia kumtupa chini. Akina Maliti huyu naye alikuwa hata balozi wa Tz UN na ameandika vitabu vizuri sana kwasababu mawazo yake yalikuwa mbele sana walikosana na Nyerere na aliishia kuondolewa ili ujamaa upone.

serekali ya awamu ya 1 ilifanya jambo 1 baya sana kwa akina Mangi kuanzia miaka ya 70 mpaka 90 mwanzoni. Mimi nikiishi na wazazi wangu waliokuwa wakifanya kazi Moshi kama walimu, walinieleza baadaye kwamba nisingeweza kufaulu darasa la 7 kama wasingenihamisha kutoka shule ambayo walikuwa wakifundisha ambayo ipo Moshi vijijini. Sababu ilikuwa mpango wa serekali kwamba watu wa Kilimanjaro vijijini waliwekewa wastani wao wa kufaulu darasa la 7 ambao ulikuwa mkubwa mno zaidi ya 96% pass mark! Lengo lilikuwa kwamba wasiende mashule ya serekali kwani walionekana tayari ni wengi kule na pia serikali ilisema wao akina Mangi wanafedha nyingi za kahawa na hivyo wanaweza kuwapeleka watoto wao shule binafsi kwa hiyo hakuna kufaulu.

La ajabu ni kwamba hawa jamaa walijenga mashule mengi binafsi na Moshi imekuwa ikiongoza kwa mashule mengi tangu wakati wa uhuru na hadi leo bado shule za sekondari ni nyingi kuliko mkoa wwowote. Kuna sekondari zaidi ya 300 Kilimanjaro pekee wakati mkoa unaofuatia nadhani una shule 118.

Niseme tu kwa kuishi kwangu Moshi nimejifunza kwamba wachagga ni watu tofauti kidogo na makabila mengine ya Tz. Hawa jamaa wanapenda kazi sana. Akina Mangi wanaongoza kwa wingi vyuoni na si rahisi hata kuwagundua kwani wengi wao hawajioneshi. Binafsi nafahamu wachagga wengi waliomatajiri wakubwa lakini utashangaa walivyo wa kawaida.

Nilikuwa na Mkenya 1 na alishangaa kusikia Wachagga ni Watz kwani kule Kenya ni wengi na wanawachalenji wakenya sana. Hawa ndugu wana uvumilivu mkubwa na ujasiri wa kufanya mambo mengi.

Tatizo kubwa la tz ni kwamba tumekuwa tukiwapa uongozi watu ambao hawana vision na matokeo yake sote tumeyaona. Pengine sasa tufanye uamuzi mgumu wa kuwapa watu ambao ni aggressive kwenye maendeleo kama akina Mangi. Hawa jamaa ni wapiganaji sana angalia akina Mbowe, Mvungi, Mbatia, Lema naye nadhani ni wa huko na wenyeviti wa makampuni mbalimbali hasa binafsi. Lakini kwa ujumla serekali ya mafisadi hawapendi kuwapa uongozi wa nchi hii kwa sababu wanazojua wao.
 
huwezi kumpa mtu uongozi kwa sababu ya kabila,kwani Makufuli mchaga?Mwandosya mchaga?selelii Mchaga?Mwakyembe mchaga?Olesendeka Mchaga,Dr slaa Mchaga?, Sitta mchaga? Mnyika mchaga? baadhi ya wachaga mafisadi ni.Mlamba na mkurugenzi Tra,kimei, na wengine wengi! nawakubali tu wachache
 
pamoja na jitihada zako za kutetea hoja yako...hauko sahihi hata kidogo. hatuchagui viongozi kwa kufuata dini zao. inasikitisha bado watu tunamtazama mtz mwenzetu halafu tunamwona kwa kabila, rangi, jinsia au dini yake. nashukuru Mungu siko kwenye hilo kundi na kabila, dini ni maswali ambayo simuulizagi mtu hata kidogo. hayanisaidii chochote
 
mkuu ndalo..huo ni ukweli usiofichika,hii nchi tukitaka iendelee lazima apewe mchaga
 
huwezi kumpa mtu uongozi kwa sababu ya kabila,kwani Makufuli mchaga?Mwandosya mchaga?selelii Mchaga?Mwakyembe mchaga?Olesendeka Mchaga,Dr slaa Mchaga?, Sitta mchaga? Mnyika mchaga? baadhi ya wachaga mafisadi ni.Mlamba na mkurugenzi Tra,kimei, na wengine wengi! nawakubali tu wachache
Ni kweli wengi wa hawa uliowataja hapa ni wapambanaji haswa, lakini vita yao ya kupigania maendeleo ya nchi, ingelikuwa imewachinjia baharini kama sii bilionea mmoja wa kichaga(Mengi), kukaa upande wao na kuwapa support kwa kila namna. Hasa wale wanaotoka sisiem.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom