Huu ni msimu wa Atletico de Madrid na el Cholo, Laliga ni yenu

Ziroseventytwo

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
7,909
13,476
Sina shaka na uwezo wa kocha na wachezaji wa club hii kongwe ya pale mjini Madrid. Kwa miaka mingi Elcholo alijaribu kutengeneza kikosi cha kupambana na Barcelona na Real Madrid bila mafanikio. Kwani vilabu hivi viwili vilikuwa na vikosi bora kwa zaidi ya miaka kumi.

Ila kwa sasa wale golden boys wao wote wamefikia mwisho wa uwezo wao. Madrid iliyokuwa ikibebwa na Bale Benzema na Cristiano kwa sasa huo utatu mtakatifu haupo tena. Marcelo mmoja wa mabeki bora kabisa wa pembeni kutokea kwenye hii dunia kafika mwisho sasa anaanzia bench. Bale kabadilika kawa mcheza golf.

Barcelona Messi naye kafikia mwisho na haoni future tena pale Nou camp. Pique, Busquet, Alba, Ratikic, Umtiti ote kwa sasa ni everage players na umri ndio umeenda.

Sasa ni kazi ya el chola kuwatumia vijana wake ambao mbali na vipaji pia wana spirit ya hali ya juu. Chini ya captain Koke, Saul, Carrasco, Joao Felix, Lodi mwamba Patey huu ndio msimu wenu wa kunyanyua kwapa kwa kubeba kikombe cha Laliga.

zitto junior
 
Hii ni fursa kweli kweli changamoto ni hii Covid-19 imeiacha Atletico haina kitita kabisa cha kufanya sajili. Wanapwaya eneo la forward hasa Diego Costa na Morata bado hawajaweza kufumania nyavu inavyopaswa.
Ila eneo la Beki wakiongozwa na mwamba Gimenez, Felipe na Savic. Hapo kati kuna kisiki Partey, Herrera, Saul na Koke. Aah wana ukuta imara haswaa.

Ila mbele wanakosa mmaliziaje wa mipira na pasi zenye macho kutoka kwa Carrasco/Llorente ama Felix/Correa. Otherwise kma Griezmann angebaki Atletico naona huu msimu ndoo ni yetu kabisa.

Tusubiri tuone kma kuna sajili ya forward itakuja
 
Sina shaka na uwezo wa kocha na wachezaji wa club hii kongwe ya pale mjini Madrid. Kwa miaka mingi Elcholo alijaribu kutengeneza kikosi cha kupambana na Barcelona na Real Madrid bila mafanikio. Kwani vilabu hivi viwili vilikuwa na vikosi bora kwa zaidi ya miaka kumi.

Ila kwa sasa wale golden boys wao wote wamefikia mwisho wa uwezo wao. Madrid iliyokuwa ikibebwa na Bale Benzema na Cristiano kwa sasa huo utatu mtakatifu haupo tena. Marcelo mmoja wa mabeki bora kabisa wa pembeni kutokea kwenye hii dunia kafika mwisho sasa anaanzia bench. Bale kabadilika kawa mcheza golf.

Barcelona Messi naye kafikia mwisho na haoni future tena pale Nou camp. Pique, Busquet, Alba, Ratikic, Umtiti ote kwa sasa ni everage players na umri ndio umeenda.

Sasa ni kazi ya el chola kuwatumia vijana wake ambao mbali na vipaji pia wana spirit ya hali ya juu. Chini ya captain Koke, Saul, Carrasco, Joao Felix, Lodi mwamba Patey huu ndio msimu wenu wa kunyanyua kwapa kwa kubeba kikombe cha Laliga.

zitto junior

Mbona walishabeba ile 2012 boss, kwasasa wasubilie labda 2027 hukooo
 
hao Atletico ni kama Azam tuu hapa bongo, msimu ulioisha ndio msimu ulokua na Madrid mbovu na Barca mbovu ila bado wakaishia wa 3, sawa na Azam kumaliza nyuma ya Yanga mbovu

Sent from my Nokia 1 using JamiiForums mobile app
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom