JEKI
JF-Expert Member
- Aug 16, 2013
- 4,845
- 2,937
Wapo watu wakitokewa na jambo wasilolipenda basi huona ni mkosi pasipo kujua labda ingekuwa kama wanavyotaka wangepata balaa kubwa. Ni katika muktadha huo nami nipo njia panda, kila ninapokuwa na mtu ninayemheshimu ndo hapo ninapokutana na mwanamke mrembo, mfano ninapokuwa nimeongozana na mpenzi wangu au baba yangu au mama yangu na hata labda bosi wangu au hata bibi na babu, hapo ndo ninapokutana na mwanamke mrembo, hapo nakuwa hata siwezi kuchomoka kumfatilia mrembo yule, lakini nikiwa mwenyewe nitatembea siku nzima wala sikutani ni mwanamke wa kunivutia. Huu ni mkosi au bahati??????????