Huu ni baadhi tu ya ufisadi mkubwa ndani ya CHADEMA; ni kuhusu mamilioni ya Sabodo

300 Millions inatosha kununua na kukarabati nyumba Dubai? Inatosha kujenga nyumba kunduchi? Kukarabati Bilicanas?
Mtoa mada umekurupuka hvyo kajipange upya.
 
Mkuu niweke ushahidi wa visima au gari?

wacha kujichanganya nikuwekee ushahidi wa visima au gari kivipi..!!!! mmetumwa kututoa kwenye topic ya mkapa..hatulali tunaye leo..mpaka atarudia tena ile doz yake ya presha..
 
Kweli watu wanapenda kusikia wanayoyataka tu.
Hivi zile tuhuma alizozitoa Vincent dhidi ya Mkaa Hapa (Mkapa) zilikuwa na au zina ushahidi gani? Mbona sijasoma popote mkiomba ushahidi? Si mumeamua kuwa kizazi cha gossips? Au mnachagua story za kuomba source na evidence?
 
user-offline.png
MWANAHALIS

Junior Member Array

Join Date : 7th March 2012
Posts : 3
Rep Power : 0
Likes Received0Likes Given7

Join Date sio issue, issue ni kujibu hoja.
 
300 Millions inatosha kununua na kukarabati nyumba Dubai? Inatosha kujenga nyumba kunduchi? Kukarabati Bilicanas?
Mtoa mada umekurupuka hvyo kajipange upya.

Mkuu, soma vizuri hii thread msatari kwa mstari sio Sh300 Milioni ni Sh700 Milioni.
 
Mkuu, ebu tuambie hivyo visima vipo wapi au huo mradi wa visima unaendeshwa na kampuni gani?

ngoja niwaeleweshe ndugu..sabodo alitoa ofa ya kuchimba visima zaidi ya 600 nchi nzima.. (na hakutoa pesa ya visima..pesa aliyotoa ni kwa ajili ya kusapot mustafa sabodo academy) akatoa ofa ya kuchimba zaidi visima kwenye majimbo ya cdm..kutokana na shida ya maji igunga,cdm walimwomba idadi kubwa ya visima ielekezwe igunga badala ya kwenye majimbo yao..so aulizwe sabodo amefikia wapi..?sio cdm..na hata mwandosya aliahidiwa visima zaidi kwenye jimbo lake baada ya kwenda nyumbani kwa sabodo kumshukuru..
 
Mkuu unataka chanzo gani wakati jambo lipo wazi pesa alizotoa Sabodo mpenda maendeleo zipo wapi? au umeishawahi kusikia viongozi wa Chadema wamezitolea maelezo?

Na nyumba ya Slaa, Kunduchi beach, ujenzi wa Billcanas.

Mzee Sabodo pesa zako zinafanya kazi nyingine.

wala usidhani sabodo atashtushwa na hayo mayowe yako, namwamini sana huyu sabodo ni mzee makini,kama cdm wangekuwa hivyo asingetoa hiyo misaada yote tena mara tatu.mnatakiwa mkubali tu kuwa kuizima cdm hakufanikiwi kwa vimajungu hivi.tafuteni mbinu nyingine tena
 
mbona kwenye misaada ya sabodo hapo hamdai soure? Na kama hiyo mnaikubali mbona hamjibii nukta hiyo hiyo tulioko nje tupate faida?
 
kwa akili yako hiyo hela wewe ndo unaona inafaa kwenye hayo mambo.kweli wewe gamba

Mkuu mie sijakuambia inafaa wala haifai cha msingi ni wewe ungejibu hoja za mleta hii thread kupinga hayo mie utanionea bure mkuu wangu.
 
ngoja niwaeleweshe ndugu..sabodo alitoa ofa ya kuchimba visima zaidi ya 600 nchi nzima.. (na hakutoa pesa ya visima..pesa aliyotoa ni kwa ajili ya kusapot mustafa sabodo academy) akatoa ofa ya kuchimba zaidi visima kwenye majimbo ya cdm..kutokana na shida ya maji igunga,cdm walimwomba idadi kubwa ya visima ielekezwe igunga badala ya kwenye majimbo yao..so aulizwe sabodo amefikia wapi..?sio cdm..na hata mwandosya aliahidiwa visima zaidi kwenye jimbo lake baada ya kwenda nyumbani kwa sabodo kumshukuru..

Mkuu, kuna Sh200 Milioni alitoa Mzee Sabodo Hand to Hand unaweza kutuambia matumizi yake?
 
Mods tujenge heshima ya jukwaa hili haiwezekani mtu anaingia na kuandika vitu vya kuchafua watu tu bila ushahidi wowote.Mods hii si haki kabisa.Mtoa mada aweke uthibitisho ama sivyo ondoeni hii mada.Jukwaa hili lisitumike kupotosha na kuchafua watu.Nadhani sheria za JF haziruhusu hali kama hii.

kwani Vicent Nyerere alimwona Mkapa anamwekea sumu JK NYERERE? Mi kila siku nasema WANASIASA WOTE WEZI C CHADEMA WALA CCM
 
Hivi mil 300 unaweza kufanya mambo yote aliyoyataja huyu jamaa? Kununua nyumba dubai ni sh ngapi? Kujenga nyumba kunduchi sh ngapi? Kufanya ukarabati wa billz sh ngapi? Mtoa mada akajipange upyaaaa!![/QUOAsante sana kwa kuweka hali ya hewa sawa hapa uyu jamaa alishaaribu, so the guy alitaka aone akaunt ina 300Mil tangu 2010 to 2015...Jambo jingine nikwamba matokeo kuhesabiwa pale kwenye zile appartment hiyo sio proof,Kwakweli mtanzania umepotea na we simwana halisi bali Mzushi na kauli zakozinaonyesha ulianguka maali flan ukawekwapembeni sasa hasira zako unakichafua chama.Inadhihirisha kabisa upokaribu na chama lakini una data zauzushi kuwachafua watu unaowaona kama walio kukwamisha kwakua walikuona hufai nawe unatudhihirishia wana JF hapa. Ndugu yangu sio kila king'aacho nidhahbu inawezekana wewe ni bati tu......
 
Hivi mil 300 unaweza kufanya mambo yote aliyoyataja huyu jamaa? Kununua nyumba dubai ni sh ngapi? Kujenga nyumba kunduchi sh ngapi? Kufanya ukarabati wa billz sh ngapi? Mtoa mada akajipange upyaaaa!!
Na anasema zilitolewa mwaka 2010 kwa ajili ya uchaguzi akumbuke kuwa wakati wa Kampeni chama kilizunguka Tanzania nzima. Hana jipya. Toa taarifa au ufisadi ukiwa na vielelezo usiibuke tu. Watanzania wa leo sio wa mwaka 47 chunga sana. Bilicanas inajiendesha na hata ivyo Mbowe anabiashara zake, Halfu anunue nyumba Dubai aweke ndg zake ili iweje mara ya biashara. Dunia ya sasa uwezi kumdanganya mtu. Kama yangekuwa kweli Magamba yasingekaa kimya hadi leo umechemsha tafuta asprin ikutulize
 
Mods tujenge heshima ya jukwaa hili haiwezekani mtu anaingia na kuandika vitu vya kuchafua watu tu bila ushahidi wowote.Mods hii si haki kabisa.Mtoa mada aweke uthibitisho ama sivyo ondoeni hii mada.Jukwaa hili lisitumike kupotosha na kuchafua watu.Nadhani sheria za JF haziruhusu hali kama hii.

Mkuu, JF sio mali ya Chadema acha kulia lia kwa mods haya maneno yako mbona hatukayaona kwenye thread ya Mkapa kuhusu Nyerere.

Mkuu siasa ndivyo zilivyo kuna machungu na matamu chungu kumeza lakini vumilia.
 
Mods tujenge heshima ya jukwaa hili haiwezekani mtu anaingia na kuandika vitu vya kuchafua watu tu bila ushahidi wowote.Mods hii si haki kabisa.Mtoa mada aweke uthibitisho ama sivyo ondoeni hii mada.Jukwaa hili lisitumike kupotosha na kuchafua watu.Nadhani sheria za JF haziruhusu hali kama hii.

Mkuu naona mjadala unaenda vema so far, mtoa mada amedai ataleta ushahidi, lets wait a bit longer!
 
300 Millions inatosha kununua na kukarabati nyumba Dubai? Inatosha kujenga nyumba kunduchi? Kukarabati Bilicanas?
Mtoa mada umekurupuka hvyo kajipange upya.
ni pesa ya kununulia kiwanja kwa baadhi ya maeneo hapa dar.
 
Huyu mtoa mada yawezekana ana matatizo ya kisaikolojia, Na hata hivyo kama ana ushahidi na hajakurupuka si aende mahakamani au polisi? Chadema wakiwataja na kuwashitaki mafisadi kwa umma ni halali yao kwani hawana serikali, hata ccm mnalalamika kama mmeshindwa achieni madaraka.
 
Hii ni vita ni mapambano; katika vita - hasa classical warfare - lengo ni kuwashambulia majemedari. Tumeshaona kuwa CDM wanashambulia viongozi wa juu wa CCM na hiyo ni sehemu ya mapambano na anayefikiria kuwa watu wa CCM watakuja na kutoa pongezi kwa viongozi wa CDM anakosea. Tumeshaona toka mwanzo wa kampeni za Arumeru na kwingine viongozi wa CDM watashambuliwa siyo kwa mambo ya utendaji tu bali hata kwenye mambo binafsi. Hili limekuwa likifanyika kwa viongozi wa CCM vile vile.

Ni jukumu la watu kupima kila wanachokisoma na kupima uzito wa ukweli wake - au hata kupima uwezekano wa ukweli wake. Kama mtu anaweza kuyumbishwa na simulizi la kufikirika kwa sababu linasomeka vitamu atakuwa na matatizo.
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom