Huu ni baadhi tu ya ufisadi mkubwa ndani ya CHADEMA; ni kuhusu mamilioni ya Sabodo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huu ni baadhi tu ya ufisadi mkubwa ndani ya CHADEMA; ni kuhusu mamilioni ya Sabodo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TUNTEMEKE, Mar 14, 2012.

 1. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  BAADHI YA UBADHILIFU WA DR.SLAA NA MCHUMBA WAKE JOSEPHINE

  2. Dkt. Slaa yeye amedhihirisha ni jinsi gani mnafiki kwani pamoja na kujidai kupinga posho lakini bado ameshindwa hata kuusimamia mfumo wa posho ndani ya chama chake nitatoa mfano;-
  i. Amelazimisha chama kumlipa mke wake milioni kumi kama malipo ya kutengeneza mfumo wa komputa wa kusimamia mahesabu ya chama.
  ii. Anajilipa posho ya shilingi 250000/= kwa siku kila aendepo ziara na kwenye kesi yake kule Arusha ambapo yeye, mke wake pamoja na yaya wao husafirishwa kwa ndege kila safari na wote wanalipwa 250,000/= ya kujikimu wakati wote wanalala chumba kimoja?. Haya ni matumizi mabaya ya ruzuku ya chama ambazo ni kodi za wananchi.
  iii. Amejikopesha pesa ya chama kujengea nyumba yake kule kunduchi ambapo yeye mwenyewe ndio msimamizi mkuu wa pesa za chama na ndio mlipaji mkuu na wala hajafuata mfumo wowote wa malipo na ukopeshaji na haijulikani ni lini atarudisha fedha hizo za wanachama na kwa utaratibu upi?.

  MAJIBU YA DR.SLAA NI HAYA HAPA

  AKAULIZWA TENA
  NAOMBA DR.SLAA AJIBU TENA HUJUMA HIZI ANAZOZIFANYA NDANI YA CHAMA YEY PAMOJA NA JOSEPHINE:


  1.Hivi unaweza ukatuambia ni kwanini kesi ya chama yako tu ndo igaramiwe na chama wakati kesi ya chama ya susan kiwanga na Kasurumbai wanajigaramia wenyewe?. mbona wewe na hao wote mnalipwa sawa milioni 7 kwwa mwezi?.

  2.Unaweza ukatueleza watu wenye akili zetu ulitumia kikao gani kuidhinishiwa mkopo uliojengea nyumba yako ambao unatokana na pesa za wananchama?.

  3.Unaweza ukatueleza ni kwanini ulipindisha maamuzi ya kamati kuu ya kuhakikisha kila mwezi chhama kiweke 25% ya ruzuku kwenye akaunti ya uchaguzi kwa ajili ya uchaguzi ujao?. unaweza ukasema ni kwanini mpaka hii leo kuna shilkingi 0 kwenye akaunti ya uchaguzi?.

  4.Unaweza ukasema ni kwanini wewe ukishirikiana na mapacha wenzako wawili mlikwenda kupindisha maamuzi ya kamati kuu ya kuweka 20% ya ruzuku ya chama kila mwezi kwa ajili ya Investments za chama na mpaka hivi sasa chama hakina hata Baiskeli ya mbao iliyonunua tangu uchaguzi mkuu uishe?.

  5.Unaweza ukasema ni kwanini chama kimlipe posho ya 250000 mkeo kila akienda kusikiliza kesi yake pale mahakamani arusha na haimpi hata senti moja Dady Igogo ambaye naye pia ni m,shitakiwa kwenye kesi kama hiyo?.

  6.HIVI UNAWEZA KUSEMA MBELE YA WATU KUWA WEWE NI KIONGOZI WA WANYONGE KWELI HALAFU UNALALA HOTEL YA 280000?. sasa kama ndio hivyo inakuwaje muwalipe wenzenu mliowatuma uzini na arumeru elf 30 kwa siku au wewe na mbowe ndio mnajua sana kulala kuliko wenzenu?

  7.Unaweza ukatuambia ni kwanini House Girl wako alipwe na chama shilingi 250000 kila siku pindi muwapo arusha wakati hata kadi ya chama hana?.

  8.Unaweza ukasema ni kwanini ulimwamuru MWIGAMBA AJIUDHURU baada ya kukataa kulipa milioni 10 za kutengeneza acuonting system za chama?.

  9.Unaweza ukasema ni lini tangazo la ma volunteer wanaoweza kutengeneza acoounting system lilitangazwa hapa kwenye ubao bnwa matangazo wa chadema hadi hawara ako akashinda hiyo nafasi?..
  karibu tena utupatie majibu tafadhali.

  KUHUSU UBADHILIFU WA MAMILLION YA SABODO


  CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO(CHADEMA) ni moja kati ya chama kilichojizolea umaarufu sana hapa nchini na kusema ukweli muundo wa katiba yake na sera zake umekaa kiukombozi haswaa!!!!wananchi wengi tunaipenda chadema..hasa namna viongozi wake akina Mbowe na Slaa wanavyojua kuhadaa watanzania wanapokuwa kwenye majukwa ya siasa.

  Ikumbukwe ni hawa hawa akina Slaa na Mbowe ndio waliotaja List of Shame pale mwembe yanga...walifichua ufisadi mkubwa sana unaofanywa na serikali ya ccm kupitia viongozi wake.

  Lakini leo hii inashangaza sana kuona Mbowe na Slaa ndio haohao wanaoongoza kwa ufisadi mkubwa ndani ya chama na kwa watanzania kwa ujumla wao

  WAKATI wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2010 tunakumbuka wote kuwa Mfanya Biashara maarufu Tanzania SABODO alitoa kwa mara ya kwanza Million 100 kwa CHADEMA ilikuimarisha nguvu ya kampeni na kukijenga chama kipindi chote cha kampeni.

  AWAMU ya pili alitoa millioni mia moja (100) kwa ajili ya kujenga chuo pale KIBAHA cha CHADEMA ilivijana wawezekupata mafunzo ya kisiasa,uzalendo ndani ya chama na nchi yao.

  Akaahidi kutoa Million 100 zingine kwa ajili ya ujenzi wa chuo hicho pale KIbaha,ambazo kwa mujibu wa ripoti unaonyesha kuwa amezitoa.

  AWAMU ya tatu ametoa MIllion Mia Moja(100) kwajili ya ujenzi wa visima miambili (200) katika maeneo ya majimbo yanayoongozwa na wabunge wa chadema.

  Jumla ya pesa taslimu aliyoitoa hand to hand ambazo watanzania ni Million mia tatu(300).

  LAKINI cha kusikitisha pesa hizo zimeenda kukarabati ukumbi wa starehe unaomilikiwa na MH.freeman Mbowe ule wa BILLICANAS(Kama unabisha nenda Billcanas ukaone ujenzi unaondelea na fedha zimechotwa kwenye account ya uchaguzi ya chama).

  Napia ametumia pesa hizo kwenda kununua nyumba ya kifahari pale DUBAI ambayo hadi dakika hii anaifanyia ukarabati kwaajili ya kuipangisha na kuhamishia baadhi ya ndugu zake pale Dubai.

  View attachment 49351

  PESA nyingine toka kwenye account ya UCHAGUZI 2015 imetumika kujengea nyumba ya katibu mkuu Ndugu W.P.Slaa maeneo ya KUNDUCHI(amehamia hapo kunduchi mwaka huu).Kabla ya hapo alikuwa anaishi PALE ABLA APARTMENT pale Kijitonyama ambapo ameishi kwa muda wa miaka miwili na malipo ya kodi kwa siku ni Tsh.250,000(laki mbili na nusu,watanzania uzalendo wa Dr.Slaa upo wapi katika hili) ambapo pesa hiyo ilikuwa inalipwa na chama na hapo ndipo matokeo ya mgombea urais yalihesabiwa na kauli ya kwamba tumechakachuliwa ilitolewa hapo.

  View attachment 49350

  WAKATI HUO HUO,Mh.mbowe amekuwa akiwahadaa watanzania kwa kurudisha gari la kifahari la serikali ambalo ni maalumu kwa ajili ya kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni,Alirudisha gari hilo kwa mbwembwe kweli na vyombo vya habari vililizungumzia sana jambo hili.

  NASASA amelichukua kimyakimya na huku watanzania wasijue kuwa anaendelea kulitumia.Yeye na chama chake walisema hawataki posho za bunge lakini mpaka leo hii mbowe anachukua posho na pia Dr.slaa anachukua posho akiwa katika kazi za ujenzi wa chama ambayo kwa siku analipwa Laki moja,Dreva wake analipwa 30000 na mlinzi wake analipwa 30000 hiyo ni mbali na mshara wa milioni saba (7000,000) kwa kila mwezi(wakati huo ikumbukwe makati wa kuu wa mikoa wa chama,makatibu wakuu wa wilaya n.k wa chadema hawalipwi chochote,hawapewi posho hata sent moja)...

  View attachment 49353

  Na pia kanisa analo sali mchumba wake CHAMA kinawalipa walinzi wawili lakitano kwa mwezi kila mmoja kwaajili ya ulinzi wa kanisa hilo analosali JOSEPHINE MSHUMBUSI.

  MAJIBU YA DR.SLAA YALIKUWA HIVI;

  Upotoshaji si vema kuuchia. Mnyika yuko Joeburg kikazi hivyo naomba kufafanua mwenyewe.

  1. Fedha za Sabodo ni kweli zimepokelewa kwa awamu mbili @100m. Hizi zilikuwa kwa ajili ya Kampeni Uchaguzi Mkuu na tumezitolea taarifa ya matumizi mara kadhaa hadharani. Taarifa pia ipo kwa Msajili wa vyama kama mhusika anataka kujua zaidi.

  2. Fedha za Sabodo ahadi ya 150m kwa ajili ya ujenzi wa Chuo. Ilikuwa ahadi na hatua tuliyopo sasa ni ku process "title Deed" eneo la ekari 100m Soga, Kibaha. Fedha za Sabodo bado ziko kwa Sabodo kwa kuwa ujenzi haujaanza. Sijui kama Sabodo anaweza kujifisadi mwenyewe.

  3. Fedha za visima 200m toka Sabodo. Wajibu wa Chama ilikuwa kuomba. Wajibu wa Sabodo ni survey, design, kuchimba na kukabidhi visima vilivyokamilika( turn key). Sijui kwenye Turn key project ufisadi una sura gani. Labda mimi sielewi.

  4. Nyumba ya Dr Slaa. Hivi mhusika alitaka niishi Abla milele au alitaka nikope kwake ili ajue siyo ufisadi. Anaruhusiwa kupekua pote na aanike hadharani ushahidi wake

  4. Sihitaji kumtetea Mbowe. Ni mfanyibiashara asiyejificha. Sources za ujenzi wa Bilicanas si siri aache uvivu wa kufikiri na kutafiti kisayansi.

  Nauliza hivi!
  1.Uadilifu wa viongozi wa chadema uko wapi?
  2.Je huu sio ufisadi? au ufisadi ni EPA,MEREMETA na DOWANS tu?
  3.Hivi unapo wadanganya watanzania kuwa umerudisha gari wakati nyuma yake umelichukua kimya kimya inaleta picha gani?
  4.Hivi kunautofauti gani kati ya mwamvita makamba aliyejenga nyumba hapa TZ na MBowe aliyekwenda kununua nyumba nje ya nchi ?
  5.Hivi hatari ya kuwaamini viongozi kama hawa ambao machoni niwasafi,moyoni wanaroho ya mbwa mwitu mwisho wake itakuwaje?
  6.Hivi kunaulazima gani kuweka walinzi kanisani anakosali mchumba wa Dr.slaa kwa kutumia ruzuku ya chama?
  7.Hivi CHADEMA watachukuaje nchi,ikiwa pesa iliyoazimishwa na kamati kuu baada ya uchaguzi mkuu wa 2010 kuwa asilimia 25% ya ruzuku yote kwa kila mwezi iwekwe kwenye account ya uchaguzi kwaajili ya 2015,lakini mpaka sasa hakuna hata shillingi zote zimechukuliwa na wajanza wa chache?
  8.Josephine mbona anatuharibia chama chetu?mbona mke wa mbowe yupo kimya?Josephine ni mchumba tu na sio mke rasmi wa Dr.slaa lakini amekuwa na nguvu sana ya kuendesha mambo ndani ya chama?

  Naomba kiongozi wa CHADEMA yeyote yule aliyemo humu JF aje akinzane na ukweli huu...ili tuweze kuweka data kamili hapa.
   
 2. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2012
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Umejiunga leo na umeaanza na pumba, Hebu weka ushahidi wako hapa sio unatoa povu kama yule Fisadi Mkapa anayesubiria ukombozi wa kweli na kupelekwa jela.
   
 3. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  tuhuma zako hazina ushahidi wa kutosha kutufanya sisi tuamini hayo usemayo.kama una ushahidi mwingine uweke hapa lkn sio huu ulioutoa
   
 4. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #4
  Mar 14, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Uchaguzi BAVICHA umejeruhi wengi sana. Maombi ya majeruhi ni CDM kishindwe Arumeru kwa Propaganda kama hizi. Mshindwe!
   
 5. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #5
  Mar 14, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  hii ni mwanahalisi gazeti? au ni jina tu la member. Umetuchanganya wengi sana hapa, toa ufafanuzi kabla hatujaanza kutoa comment
   
 6. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #6
  Mar 14, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nadhani TUNTEMEKE anaongoza kwa kuwa na ID nyingi humu JF!
   
 7. Prishaz

  Prishaz JF-Expert Member

  #7
  Mar 14, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 1,928
  Likes Received: 1,461
  Trophy Points: 280
  hiki ndicho kilichokufanya ufungue hii ID? inaonekana kuna kitu umekosa mahali flani
   
 8. +255

  +255 JF-Expert Member

  #8
  Mar 14, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 1,908
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 180
  Kwa kuwa kazungumzia CDM mnahitaji ushahidi, ila ingekuwa side B sijui ka ungeandika post ka hy.
   
 9. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #9
  Mar 14, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Toa chanzo mkuu ili tuichangie fresh!
   
 10. MwafrikaHalisi

  MwafrikaHalisi JF-Expert Member

  #10
  Mar 14, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 1,746
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Tunathibitishaje kama ni kweli au la? Eti twende billicanas tukaangalie ujenzi, kweli? Billicanas yenyewe inauwezo wa kugenerate zaidi ya millioni 100 kwa mwezi. Please come up with something vivid sio unatunga stori kama za Shigongo. Kila mtu anaweza kuamka na kuandika kama ulichoandika!
   
 11. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #11
  Mar 14, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  hizi zote ni shutuma zisizo na evidence'unataka kusema huko chadema ni mbowe na slaa peke yao?hakuna watu wengine wenye uwezo wa kujua hela zinatumika vipi?umechemsha mkuu
   
 12. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #12
  Mar 14, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nimemuona Ritz yupo Online anasoma hii thread. Ngoja tusubiri coment yake!
   
 13. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #13
  Mar 14, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,152
  Likes Received: 2,399
  Trophy Points: 280
  Hoja zako ni za msingi sema hazina mashiko kabisa zinaonekana ni p.umba.
   
 14. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #14
  Mar 14, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Haya mambo yanaweza kuwa majungu ama la. Ila kwa ujumla wake yanatisha sana hasa ikizingatiwa CDM na viongozi wake ndio tegemeo la watanzania kuondokana na minyororo ya CCM. Haya mambo yanahitaji majawabu.

  Moja nimelisikia kama miezi miwili hivi iliyopita; kwamba KUB amelichukua kimya kimya gari la rasmi la KUB. Hayo mengine sijui. Ila linalotisha zaidi ni hili la Mwenyekiti wa CDM kununua nyumba Dubai na kuikarabati kwa ajili ya kuwahamishia ndugu zake huko. Kama ni jungu basi ni jungu baya sana inabidi litolewe kauli si la kuacha hivi hivi. Kama kiongozi ana mpango wa kuhamishia ndugu zake ughaibuni hapa kuna ujumbe gani?
   
 15. L

  Laptani Member

  #15
  Mar 14, 2012
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Sometimes you want peoples to read you from a different angle.
  Pouwa tumekusoma fikra zako, zinakutosha wewe mwenyewe na waliokutuma ila kwa taarifa yako watz wako makini sana n' no one is going to buy that cheap bite!!!!!!
   
 16. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #16
  Mar 14, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,152
  Likes Received: 2,399
  Trophy Points: 280
  Hivi mil 300 unaweza kufanya mambo yote aliyoyataja huyu jamaa? Kununua nyumba dubai ni sh ngapi? Kujenga nyumba kunduchi sh ngapi? Kufanya ukarabati wa billz sh ngapi? Mtoa mada akajipange upyaaaa!!
   
 17. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #17
  Mar 14, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Huyu ni TUNTEMEKE,atoe chunusi zake hapa.jamaa anataka cheo kwelikweli.uzushi utamuua
   
 18. MNAMBOWA

  MNAMBOWA JF-Expert Member

  #18
  Mar 14, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,983
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Hakuna aliye msafi, tena upande huu wa kivuli ndo kumejificha mengi maovu
   
 19. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #19
  Mar 14, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Mkuu unataka chanzo gani wakati jambo lipo wazi pesa alizotoa Sabodo mpenda maendeleo zipo wapi? au umeishawahi kusikia viongozi wa Chadema wamezitolea maelezo?

  Na nyumba ya Slaa, Kunduchi beach, ujenzi wa Billcanas.

  Mzee Sabodo pesa zako zinafanya kazi nyingine.
   
 20. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #20
  Mar 14, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0

  Inabidi ifike hatu tumshauri Dk Slaa ampe kazi angalau ya Ulinzi pale Makao Makuu. Ni Mjinga na hana adabu - Benjamin William Mkapa!
   
Loading...