Huu ndo utakuwa mchuano mkali 2020, CCM watakuwa Kitonga wakiserereka!

kajekudya

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2015
Messages
881
Points
1,000

kajekudya

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2015
881 1,000
Mwaka 2015 Chama cha Demokorasia na Maendeleo( CDM) kilikuwa ktk kilele chake cha mafanikio. Kama si technical error's walizofanya mwishoni kabisa, kushindwa kumuelewa mwenye ngoma waliyokuwa wakiicheza kwa mda mrefu ,uzoefu wa CCM, CCM kuwa chama Dora na mambo kadhaa ya kikatiba kuhusu uchaguzi ambayo hayajakaa sawa, basi CDM chini ya mwamvuli wa UKAWA walikuwa wanatinga magogoni!

Sasa baada ya tingatinga kuishika magogoni na mwenye ngoma kuanza kufanya kazi zake za asili za miaka yote( kumbuka NCCR ya 1995) sasa mambo yanabadilika kwa kasi mno.

Ni katika mukitadha huu nayaona mambo yafuatayo yakitokea kabla na mnamo mwaka 2020 kwenye medani za siasa kwenye kaya yetu tukufu!

1. CCM itakuwa imerudi kwenye level zake, CCM ile yenye uwezo wa hali ya juu kwenye proganda, CCM ile yenye uwezo mkubwa wa kimafia, CCM ile yenye think Tank zilizibobea, CCM ambayo vijana wadogo kama kina mnyika, Zitto, au tundu Lissu hawawezi kuitikisa hata kidogo!

2. Edward Ngoyaye Lowassa hatagombea uraisi, wengi watakipinga hili, lkn ukweli ni kuwa Lowassa ni mtu anayependa sana sehemu nzuri, anapenda sana ufahari. CDM( UKAWA) ya 2015 ilikuwa kama kigori wa kitutsi, ilikuwa inavutia, ulikuwa inapendwa na kila mtu, ilikuwa oxygen ya watanzania, iliwavutia Maaskofu, Mapadri, Mashehe hadi wachungaji, ninaamini hata mwenyekiti wa Chama aliyepita aliipenda CDM hii, yaani kuna wkt akikaa kwenye tv pekee yake alijikuta akitabasamu mwenyewe akiona jinsi CDM ilivokuwa tamu!
Mwaka 2020 CDM haitakuwa tena sehemu ya kujiskia ufahari, watakuwa wamekataa tamaa, morali itakuwa chini, yaani watakuwa wanapitia kipindi cha mpito baada ya mafanikio yaliyopatikana kwa kutumia nguvu kubwa( kwenye soka tunaita second season syndrome) hali ambayo ni ya kawaida sana baada ya kufika kwenye kilele cha mafanikio. Hivyo Lowassa kama mtu anayependa ufahari hata kuwa tayari kugombea kupitia CDM iliyo ktk kipindi cha mpito, CDM isiyo fahari, hata kuwa tayari kuona kile kilichomkuta Mrema mwaka 2000 au Lipumba mwaka 2010 kikimtokea yeye! Sana sana atasitafu siasa au atabaki kama Mzee Mtei na kuwaingiza vijana wake au wakwe zake chamani au hata kurudi nyumbani Lumumba!

3.Mchuano mkali utakuwa kati ya wanaUKAWA wa zamani. Hapa baada ya wanaUKAWA kugawanyika wataunda kambi mbili, zote hizo zitakuwa zikipambana kuwania nafasi ya kambi rasmi ya upinzani. Hapa ni kwakuwa itakuwa wazi kuwa CCM watashinda kwa kishindo hivyo hawa wawili watajikuta hoja zao ni kuomba ridhaa ya kwenda kuisimamia serikali kama kambi rasmi ya upinzani! Ikumbukwe upande huu mpya wa UKAWA ndipo mwenye ngoma ile walioicheza CDM miaka dahari anapojaribu kuihamishia ngoma yake,hivyo kabla 2019 tunakwenda kupata UKAWA nyingine kubwa na yenye nguvu!

3.Wakati wanaUKAWA hawa wa zamani wakichuana vikali kutafta nafasi ya kambi rasmi ya upinzani, CCM wao watakuwa pale kitonga wakiserereka, wakisubiri tu kujua wameshinda kwa asilimia ngapi! Na sababu kuu hapa ni kuwa tingatinga litakuwa limetifua vya kutosha na kueleweka vilivyo, hivyo kuipeperusha vyema Bendera ya Lumumba, pili, CCM sasa imeondoka kwenye kipindi cha mpito na sasa wameanza kujiorganise wkt watani wao ndo kwanza wanaingia kwenye kipindi cha mpito, tatu chama kimerudi kwa wenyewe hivyo ile CCM tunayoijua yenye fitina za kutosha inakuja nadhani tayari mmeshaona balaa lao.

Mwisho katiba itakayotumika 2020 ni hii ya sasa kama siyo hii ya sasa basi ni ile ya Joka, mpaka hapo mchezo umeshaisha!
 
kajekudya

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2015
Messages
881
Points
1,000

kajekudya

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2015
881 1,000
Kwa kifupi tuu nyakati za siasa kwa tanzania zinaelekea ukingoni hizi nyakati tulizonazo watu wanangaikia maisha yao ni bora tuu uchaguzi wa mwaka 2020 ufutwe maana vyama vya upinzani havina tena wagombea
Mkuu hatuwez kufanya hivyo, ni kawaida umarufu wa vyama kupanda na kushuka, hata CCM ya miaka kumi hii haikuwa sawa, sema tu kuwa chama Dora ndo kumewasaidia!
 
Katasheka jr

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2016
Messages
528
Points
500

Katasheka jr

JF-Expert Member
Joined Jul 28, 2016
528 500
Kwa kifupi tuu nyakati za siasa kwa tanzania zinaelekea ukingoni hizi nyakati tulizonazo watu wanangaikia maisha yao ni bora tuu uchaguzi wa mwaka 2020 ufutwe maana vyama vya upinzani havina tena wagombea
Na bora wawahi kupata fisadi wa mwisho mwisho, 2020 hawatapata fisadi, ccm itakuwa safi
 
Ninaweza

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2010
Messages
9,528
Points
2,000

Ninaweza

JF-Expert Member
Joined Dec 14, 2010
9,528 2,000
Bora za Bombadia mkuu kuliko za box!
ndugu maada yako ilivyo inabidi tusikitike tuu, kwa wale wapenzi wa masumbwi sidhani kama watufurahia mtanange wa ngumi hata kama wanaemshabikia katangazwa mshindi, endapo mpinzani wake aliingia ulingoni akiwa amefungwa mikono na miguu.
 
Katasheka jr

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2016
Messages
528
Points
500

Katasheka jr

JF-Expert Member
Joined Jul 28, 2016
528 500
N
Mwaka 2015 Chama cha Demokorasia na Maendeleo( CDM) kilikuwa ktk kilele chake cha mafanikio. Kama si technical error's walizofanya mwishoni kabisa, kushindwa kumuelewa mwenye ngoma waliyokuwa wakiicheza kwa mda mrefu ,uzoefu wa CCM, CCM kuwa chama Dora na mambo kadhaa ya kikatiba kuhusu uchaguzi ambayo hayajakaa sawa, basi CDM chini ya mwamvuli wa UKAWA walikuwa wanatinga magogoni!

Sasa baada ya tingatinga kuishika magogoni na mwenye ngoma kuanza kufanya kazi zake za asili za miaka yote( kumbuka NCCR ya 1995) sasa mambo yanabadilika kwa kasi mno.

Ni katika mukitadha huu nayaona mambo yafuatayo yakitokea kabla na mnamo mwaka 2020 kwenye medani za siasa kwenye kaya yetu tukufu!

1. CCM itakuwa imerudi kwenye level zake, CCM ile yenye uwezo wa hali ya juu kwenye proganda, CCM ile yenye uwezo mkubwa wa kimafia, CCM ile yenye think Tank zilizibobea, CCM ambayo vijana wadogo kama kina mnyika, Zitto, au tundu Lissu hawawezi kuitikisa hata kidogo!

2. Edward Ngoyaye Lowassa hatagombea uraisi, wengi watakipinga hili, lkn ukweli ni kuwa Lowassa ni mtu anayependa sana sehemu nzuri, anapenda sana ufahari. CDM( UKAWA) ya 2015 ilikuwa kama kigori wa kitutsi, ilikuwa inavutia, ulikuwa inapendwa na kila mtu, ilikuwa oxygen ya watanzania, iliwavutia Maaskofu, Mapadri, Mashehe hadi wachungaji, ninaamini hata mwenyekiti wa Chama aliyepita aliipenda CDM hii, yaani kuna wkt akikaa kwenye tv pekee yake alijikuta akitabasamu mwenyewe akiona jinsi CDM ilivokuwa tamu!
Mwaka 2020 CDM haitakuwa tena sehemu ya kujiskia ufahari, watakuwa wamekataa tamaa, morali itakuwa chini, yaani watakuwa wanapitia kipindi cha mpito baada ya mafanikio yaliyopatikana kwa kutumia nguvu kubwa( kwenye soka tunaita second season syndrome) hali ambayo ni ya kawaida sana baada ya kufika kwenye kilele cha mafanikio. Hivyo Lowassa kama mtu anayependa ufahari hata kuwa tayari kugombea kupitia CDM iliyo ktk kipindi cha mpito, CDM isiyo fahari, hata kuwa tayari kuona kile kilichomkuta Mrema mwaka 2000 au Lipumba mwaka 2010 kikimtokea yeye! Sana sana atasitafu siasa au atabaki kama Mzee Mtei na kuwaingiza vijana wake au wakwe zake chamani au hata kurudi nyumbani Lumumba!

3.Mchuano mkali utakuwa kati ya wanaUKAWA wa zamani. Hapa baada ya wanaUKAWA kugawanyika wataunda kambi mbili, zote hizo zitakuwa zikipambana kuwania nafasi ya kambi rasmi ya upinzani. Hapa ni kwakuwa itakuwa wazi kuwa CCM watashinda kwa kishindo hivyo hawa wawili watajikuta hoja zao ni kuomba ridhaa ya kwenda kuisimamia serikali kama kambi rasmi ya upinzani! Ikumbukwe upande huu mpya wa UKAWA ndipo mwenye ngoma ile walioicheza CDM miaka dahari anapojaribu kuihamishia ngoma yake,hivyo kabla 2019 tunakwenda kupata UKAWA nyingine kubwa na yenye nguvu!

3.Wakati wanaUKAWA hawa wa zamani wakichuana vikali kutafta nafasi ya kambi rasmi ya upinzani, CCM wao watakuwa pale kitonga wakiserereka, wakisubiri tu kujua wameshinda kwa asilimia ngapi! Na sababu kuu hapa ni kuwa tingatinga litakuwa limetifua vya kutosha na kueleweka vilivyo, hivyo kuipeperusha vyema Bendera ya Lumumba, pili, CCM sasa imeondoka kwenye kipindi cha mpito na sasa wameanza kujiorganise wkt watani wao ndo kwanza wanaingia kwenye kipindi cha mpito, tatu chama kimerudi kwa wenyewe hivyo ile CCM tunayoijua yenye fitina za kutosha inakuja nadhani tayari mmeshaona balaa lao.

Mwisho katiba itakayotumika 2020 ni hii ya sasa kama siyo hii ya sasa basi ni ile ya Joka, mpaka hapo mchezo umeshaisha!
Ni kawaida inzi kufia kwenye kidonda, masikio wanayo ila.... Macho wanayo lkn.., wakitoka Usingizini watakuta hata kile kidogo kimechukuliwa!
 
kajekudya

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2015
Messages
881
Points
1,000

kajekudya

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2015
881 1,000
ndugu maada yako ilivyo inabidi tusikitike tuu, kwa wale wapenzi wa masumbwi sidhani kama watufurahia mtanange wa ngumi hata kama wanaemshabikia katangazwa mshindi, endapo mpinzani wake aliingia ulingoni akiwa amefungwa mikono na miguu.
Watanisamehe Burr mkuu!!
 
mzalendo15

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2015
Messages
1,367
Points
2,000

mzalendo15

JF-Expert Member
Joined Sep 16, 2015
1,367 2,000
Kila zama na wakati wake unapoanzisha hoja kama hii lazima uangalie mazira ya sasa ukihusisha uelewa wa watu katika siasa pengine hiki kitakuwa kipindi kigumu sana kwa CCM kwa kuwa upinzani unafahamu kuwa kwa miaka mingi CCM imekuwa ikicjificha kwenye kivuli cha katiba na kushinda kirahisi.

Inawezekana kabisa vyama vyote vya upinzani vikaleta mswada wa kutokuwa na imani na tume ya uchaguzi ambayo kimsingi sio huru hivyo CCM wakajikuta wanasimama wenyewe kipindi cha uchaguzi. Hii inamaana kuwa itakuwa ni kielelezo cha utawala wa kiimla ambao umevaa ngozi ya demokrasia.
 
Forum statistics

Threads 1,392,902
Members 528,739
Posts 34,121,743
Top