Huu ndo ukweli, Mungu peke yake ndio anayejua si binadam

habari ya hapa

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
12,793
8,739
Amani iwe nanyi wana wa Mungu

Kwanza kabisa namshukuru Mungu kwa uzima na afya tele aliyonipa, naamini hata we ulipo uko mzima wa afya na mwenye nguvu.

Bibilia imeandikwa Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na dunia, na baada ya kumaliza kuumba mbingu, Mungu akahamishia makao yake mbinguni ambapo ndiko kiti cha enzi kilipo na duniani ni pahala pa kuweka miguu yake,

Je kabla Mungu hajaumba hiyo Mbingu Mungu huyu alikiwa akiishi wapi?

Mbingu inayosimuliwa ktk misahafu haijawahi kuonekana machoni kwa binadam yeyote, pamoja na kwamba watafiti wa mambo ya anga kutengeneza darubini nzur za kisasa ambavyo huwawezesha kuona umbali wa matrilion ya maili angani, lkn hawajaweza kukutana na ukuta unaozuia wasiendelee kuona mbele ambao ni ukuta wa mbingu,

Pamoja na umakini wa hali ya juu unofanywa na watafiti hawa wa anga naamini km mbingu ingalikiwepo wasingekosa kutoa taarifa za kuwapo kwake.

Km kwel kuna mbingu, basi ni Mungu peke yake ndo anajua pahala ilipo na si binadam! Maana hakuna aliyewahi kwenda huko na kurudi akaleta habari za uwepo wake.

Hadaa hii imedumaza bongo za watu wengi na kusababisha binadam aendelee kuishi kwa kutegemea mawazo duni ya waliotuletea uvumi huu.

Na rudia tena, km mbingu IPO ni Mungu pekee tu ndiye anajua pahala gani IPO na si mwanadam, tuache kuhadaana.
 
Mi nauliza hivi; yule jamaa mliye panga nae nyumba moja aliyekua anakuomba uwe room mate wako mlifikia nae wapi bana!? Haya mambo ya mbinguni ni magumu, yana proof through the Bible only, mengine haya ya mahusiano ni yetu binadamu
 
Wewe huoni ile inayoonekana blue ndio mbingu. Kama huamini kaa kimya maana mambo ya imani yahitaji imani thabit.
 
Mie sijawahi kwenda Marekani ila rais wa Marekani namjua ni nani,sina haja ya kusubiri mtu arudi kutoka marekani ndiyo aniambie rais wa Marekani ni nani.
Na japokuwa hujawahi kufika, kuyofika kwako huko hakuifanyi Marekani isiwepo duniani. Hivyo kwa mleta mada pia, kutofika kwake mbinguni, hakufanyi mbinguni kusiwepo.
 
Ieleweke hivyo mkuu,

Km mbingu na kuzimu kupo basi hiyo imebaki kuwa siri ya Mungu peke yke,
swali langu ,
kwanini amfiche mwaye?
au hatupendi?
hivi unaweza kuwa na mtoto alafu usimonyeshe nyumbani?
au sisi ni watoto wa kambo katutelekeza, wazungu ndo wana wake wapendwa? maana wao kila kitu kwao kiko sawa.
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom