Huu ndo uhuru wa mahakama kwani ni mhimili unaojitegemea katika maamuzi yake...!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huu ndo uhuru wa mahakama kwani ni mhimili unaojitegemea katika maamuzi yake...!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tanzania 4 Life, Apr 30, 2012.

 1. T

  Tanzania 4 Life Member

  #1
  Apr 30, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uhuru wa Mahakama ndo huu juzi nilitoka kuzungumzia hili kuwa Mahakama ni muhimili wa Dola unaojitegemea kwa maamuzi yake.
  Juzi Tundu Lissu(Chadema) alishinda kesi yake ya Uchaguzi bt hii leo HILARY AESHI(CCM) ameshindwa kwenye Kesi yake ya Ubunge wa Sumbawanga Mjini......Je Serikali ya CCM inamkono wake???
  Naomba tuiachie Mahakama iwe huru cz ni Chombo kinachojitegemea na tusilete Siasa kwenye maamuzi yake!!!!!
  Kumbuka bado kesi ya Makongoro Mahanga(Segerea) na John Mnyika(Ubungo)
   
 2. K

  Kijana wa CCM New Member

  #2
  Apr 30, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kule Arusha walisema Ikulu inamkono wake......Kule Singida Mashariki walisema Tundu Lissu ameishinda Serikali ya CCM
  Je,hii leo watasemaje juu ya Kuvuliwa Ubunge Mhe.Aeshi wa CCM?
   
 3. S

  Supermwanangu Member

  #3
  Apr 30, 2012
  Joined: Apr 18, 2012
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongera wana sumbawanga, jiandaeni kwa uchaguzi mpya na pia zingatia changamoto zilizosababisha mkanyimwa haki zenu! Tuipongeze mahakama kwa kufanya kazi zake vizuri na pia yawe mafundisho kwa majaji wanaoamua kupindisha haki kwa kuondekeza ubinafsi. Mara zote haki ya mtu hailiwi bali inacheleweshwa.Ole wenu mnaichelewesha haki ya watanzania kwani siku zenu zinahesabika.
   
 4. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2012
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,450
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Wewe umetumwa? post yako ya kwanza unakuja namna hii!
  Join Date : 29th April 2012
  Posts : 1
  Rep Power : 0
  Likes Received:0
  Likes Given: 1

  Wenzako wanajenga hoja kutokana na jinsi Jaji alivyojenga hoja kufikia hukumu. Wanatumia hoja za kisheria kuonesha mashaka na udhaifu wa hukumu. Unapotupa mifano ya Singida na Sumbawanga haina uhusiano na kesi ya Arusha.

  Arusha CDM hawakuishia kulalamika, wamechukua hatua za kisheria kukata rufaa. Kama nyie pia mna hoja za kisheria za kuhoji hukumu, mbona mnaruhusiwa sana kukata rufaa.

  Fundisho kwa CCM: RUSHWA inakiangamiza chama chenu.
   
Loading...