Umasikini ndio Ugonjwa Mbaya kuliko yote Duniani

umaskini ni mpaka wa kufurahia maisha. Unabaki kutamani tu kila kitu kizuri na kinachotufariji ni kuwapangia matajiri matumizi ya pesa zao ambazo hatukusaidia kuzipata. Utasikia " yaani hawa matajiri wanatumia hela vibaya yaani baba na mama wanaondoka kila mtu na gari yake, si wangeenda pamoja au yaani nguo ya laki mbili ni kuchezea pesa, mara yaani hawa matajiri wangekuwa wanajua, wangekuja huku uswazi yaani kuku mmoja 15k lakini wanaenda kula makuku hayana afya na ndio maana wanakufa kwa ugonjwa".. Umaskini siooo tupambane tu
 
Maskini kila tajiri in Freemason na atafikia motoni. Maskin ndio anajiona ufalme was Mungu ni wake, kiukweli motoni kutajaa maskini kwa ajili ya kulalamika ovyo na Unafiki.
==
Tafuta hela dogo...
Aliniambia JF member mmoja.

hiyo kweli, maskini sisi ni ngumu kufika mbinguni maana huwa tuna bifu na watu ambao hata hawatujui maana mtu yoyote anayestareheka kwako ni adui, yaani unaona ni jukumu lake kuwasaidia
 
So sad
Kuna kabila nyingine msiba ukitokea mabinti wote wanakwenda na waume zao kwenye msiba kijijini.

Aliyeolewa na tajiri atashusha gunia la mchele na debe la mafuta ya kupikia. Atavutiwa kiti akae.

Aliyeolewa na masikini atawapa mikono ya pole wazee, anatolewa jamvi . Hajakaa vizuri anaitwa akawapasulie kuni wakina mama jikoni.
 
Ooohhhhhhpss maneno mazito kabisa hayo mkuu. .yamebeba ukweli wenye kuumiza fikira na moyo '' lakini ya kitutaka vijana tubadilike /ama tuongeze jitihada katika Kutafuta. ...

Kusema ukweli umasikini ni kitu kibaya kuliko jambo lolote lile chini ya Jua
 
66 Reactions
Reply
Back
Top Bottom