Huu ndiyo uwezo walio nao Wabunge wangu wa CCM

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
"Mheshimiwa Spika, naona upinzani wamefikia pabaya, wanaikashifu serikali sikivu ya CCM. Chama kimefanya mengi sana, maendeleo makubwa tumepata, shule za msingi, sekondari na vyuo viko vingi leo, barabara za lami, umeme nchi nzima mpaka vijijini, lakini CHADEMA wanakebehi. Naipongeza sana serikali ya chama cha Mapinduzi. Mheshimiwa Spika, nikiendelea mbele naomba nielezee kwa kifupi matatizo ya jimbo langu. Kule hatuna shule ya sekondari katika kata sita, maji ni ndoto, tunategemea mvua. Shule zilizopo hazina ubora wala walimu wa kutosha. Rais alikuja sasa ni miaka sita akatuahidi umeme lakini mpaka leo hakuna lolote. Barabara ni mbovu hazipitiki. Nauliza ni lini serikali híi (ya CCM) ITATUSIKIA NA KUTULETEA MAENDELEO?"
(Makofi) kwa! Kwa! Kwa!
 
Hakuna cha kushangaza. Bosi wao hivyo hivyo na ndo maana tuna wateule majanga kama akina Mulugo , Muhongo ect !!

Kelele miingii nje na kulazimisha vinishani mbusi lakini ndani ya nchi sirikali hoi, blah blah kila siku na ona sasa watu wanatafuna hela mpaka za safari ya Rais, then sasa wamekomba za miradi ndani ya ofisi ya PM. Rais makini wala haina haja ya kusubiri sijui jangili kinana apande treni kuzuga watu eti anajali maisha ya watz, ningefukuzilia mbali wote kuanzia boss wao PM ili wengine wajue sasa hakuna mchezo.. !! Lakini kujivua gamba ilishindikana so hakuna lolote jipya

Lakini ni kujichekesha chekesha na mipasho tuu..... eti visasi sio powa hivi kweli huwaga anafikiria mambo au wanaomshauri ni wazima kweli ???

Hii ya wapambe kupita pita kulazimisha nishani na phD za kuomba omba na kujisifia utwawala bola liende inaudhi sana !!
 
namsikitikia sana mama yangu , maana alikufa akiwa mwanachama wa ccm , sijui mungu alimpokea ?
 
Msingwa alisema kuna mawaziri akili zao zimedumaa mi nadhani wabunge wa CCM, 97% akili zao zimedumaa kabisa.
 
Mimi ni mwana CCM jamani ila najitambua hadi naleta ambayo wabunge wangu hawasemi sawa .Je nami akili zangu ni mbofu mbofu kama wao ?
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom