Huu ndiyo UTAWALA BORA wa SERIKALI ya CCM au ni KUWATAPELI WANANCHI?

May 24, 2012
54
10
Nimesikitishwa sana na tangazo lililotolewa na Halmashauri ya wilaya ya Mufindi-Iringa linalohusu ugawaji wa viwanja eneo la IGOWOLE ,jambo ambalo binafsi nimeona ni mpango wakuwaibia wananchi.

1.Tangazo linamtaka kila anayehitaji kiwanja kulipia Tshs.80,000/- kama ada ya fomu ya maombi ambazo hazirudishwi hata kama hutapata kiwanja
2.Tangazo lenyewe halitaji idadi ya viwanja vitakavyouzwa
3.Tangazo halitaji bei ya kiwanja chenyewe
4.Tangazo pia linaagiza malipo yafanywe dirishani (siyo benki)
5.Mwisho wakulipia ada ya maombi ni siku 21

Maswali ninayojiuliza: Ni kweli halmashauri wana nia njema kwa wananchi? au wanataka wasio na kipato kikubwa wasipate? hasa wanapopanga gharama kubwa ya maombi na kutoa siku 21 tu au wanataka wananchi washindwe ili wapeane wenyewe..., Na je! kwanini malipo hayoyasifanyikie benki? kuna nini kimejificha nyuma yake? JE! HUU NDIYO UTAWALA BORA AU NI KUWATAPELI RAIA? MH. MENDRAD LUTENGANO KIGOLA (MBUNGE MUFINDI KASKAZINI) LIANGALIE JAMBO HILI kama unatembelea JF, Na kama yupo mwenye simu yake amjulishe hili. Na madiwani sijui wapo auwapo likizo...!
MWANA JAMVI HEBU NA WEWE TOA MAONI YAKO JUU YA JAMBO HILI ILI HAWA WALIOPEWA MADARAKA WAWEZE KUELEWA
 
Wenyeji wengi hawatapata viwanja hivyo kwani wengi wao hawana kipato kikubwa. Kuna hatari ya viwanja kupewa wageni.
 
Back
Top Bottom