Huu ndiyo ukweli unaofichwa juu ya Diwani Clementi Mabina aliyeuawa na wananchi Kisesa,Mwanza

nyampanaga

JF-Expert Member
Nov 16, 2012
346
195
-Eneo la kilima cha Kanyama lilikuwa na mgogoro wa muda mrefu baina ya wakazi wa kitongoji hicho na mheshimiwa diwani wao juu ya umiliki na kupelekea kufunguliwa shauri mahakamani.

-Wakati mahakama haijatoa hukumu juu ya nani mmliki halali kati ya diwani na wananchi, wananchi waliendelea kuchimba mawe na kuponda kokoto kwa ajili ya kupata pesa waweze kujikimu, na hili ndilo lilokuwa linamkera Mabina.

-Ili wananchi wasiendelee kuponda mawe hayo kama ilivyokuwa imeamuliwa na mahakama mpaka pale itakapotoa hukumu kamili,Mabina alikuwa akifanya jitihada za kwenda kuweke vibao vya "marufuku kuingia" zoezi ambalo lilikuwa likikwamishwa na nguvu ya wananchi kwani mara zote walisimama kidete kumzuia

-Siku ya tukio lilopelekea kuuawa kwa Mheshimiwa Mabina,alikuwa amedhamiria vile vibao lazima aviweke kwa kanuni ya liwalo na liwe.

-Alifika kilimani akiwa na mabaunsa 6 ndani ya gari lake,2 miongoni mwao wakiwa na shotgun 2,ilhali yeye akiwa na bastola .

-Alimukuta kijana 1 maeneo yale na kumteka kwa nguvu kama kinga dhidi yake endapo wananchi watakuja kukwamisha tena zoezi lake na kuwaamuru mabaunsa wake waanze kuweka vile vibao.

-Haikuchukua muda baadhi ya wananchi walifika na kukuta zoezi la kuweka vibao likiendelea huku Mheshimiwa Mabina akizunguka na kijana aliyemteka huku amemwelekezea bastola kichwani,hali iliyozusha sintofahamu nakuanza kupiga yowe wakihamasishana kubeba kila ina ya silaha kwenda eneo la tukio.

-Mabaunsa kuona vile wakatimuka na kumwacha Mabina akiwa na yulemateka akiawaambia wananchi wa step back na wasimudhuru yeye ili nayeye pia asimudhuru kijana

-Kwa mnao wafahamu wasukuma mbinu aliyoitumia Mabina ilikuwa ngumu kueleweka,yaani warudishe majeshi nyuma wakati kijana wao kawekewa bastola kichwani?!...ikawa ....nduhuuuuu....nekelage tamuuuu....twalemagaaaa,Mabina akaendelea kukaidi hatimaye wasuma wakatamuka neon....chuuuuuuuu..neno hili ni sawa na LIWALO NA LIWE..ambalo msukuma hulitumia akifika kiwango cha mwisho kabisa cha uvumilivu,wakaanza mashambulizi dhidi ya Mabina...naye akajibu mapigo tena ...chuuuuuuuuu...akamtwanga risasi ya kichwa yule mateka wake.Hapo ndo wananzengo hawa wakacharuka na kummaliza.

-Mengine yote ni uzushi ukweli ndo huu anaybisha aende Kanyama,Kisesa

Source:Afande mzalendo
 

Marire

JF-Expert Member
May 1, 2012
12,065
2,000
umri wa kesi ulikuwa miaka 15 ni kweli?
~na nimesikia kuwa alitoka kanisani na kufika nyumbani kwake akaanza kuchochea bastola risasi na hapo mke wake akamzuia asiende popote na kuficha funguo za magari yeye akaenda kukodi hiace akaingia huko na hao mabaunsa wake .
hiyo nimesikia kwani niko mwanza na maneno ni mengi kweli
 

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
54,802
2,000
umri wa kesi ulikuwa miaka 15 ni kweli?
~na nimesikia kuwa alitoka kanisani na kufika nyumbani kwake akaanza kuchochea bastola risasi na hapo mke wake akamzuia asiende popote na kuficha funguo za magari yeye akaenda kukodi hiace akaingia huko na hao mabaunsa wake .
hiyo nimesikia kwani niko mwanza na maneno ni mengi kweli

Marire...
Mtu ambaye haisikii sauti ya mkewe kamwe hawezi kuitii sauti ya wazazi wake mwenyewe waliomleta duniani.
 
Last edited by a moderator:

Bill

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
6,478
2,000
Uongo mwingine bhana hata shetani hawezi kuukubali. Unatakatisha ufirauni kwa kuuremba. Je mabina anaruhusa ya kubeba smg, mamlaka ya kuteka watu kapata wapi? Je yeye ni mahakama hadi aende kuweka vibao vya marufuku?
 

Tatu

JF-Expert Member
Oct 6, 2006
1,079
1,225
Je una habari yoyote kama alipata mafunzo ya utekaji na utesaji wakati mmoja na Savimbi wa chama majanga? Kama ni ndio, aliyapatia China au kwenye makambi yao nchini?

Ni hayo kwa sasa. Shukrani kwa kutujulisha.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom