Huu ndiyo ukweli, hata wa-tz mkiukataa bado utabaki kuwa ukweli!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huu ndiyo ukweli, hata wa-tz mkiukataa bado utabaki kuwa ukweli!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by LATTICE BOND, Mar 10, 2012.

 1. L

  LATTICE BOND JF-Expert Member

  #1
  Mar 10, 2012
  Joined: May 30, 2011
  Messages: 219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ifuatayo ni hadithi ya kweli nilisimuliwa na Baba Yangu mwaka 1987. Nimeona nichangie nanyi. Ipo Hivi:-
  Mnano mwaka 1987 jioni nimetoka shule ya msingi mimi na baba tulikuwa tunasikiliza taarifa ya habari RTD baadaye ikasomwa habari kwamba Rais Mwinyi alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa kiwanda [sikikumbuki]. Mara Baba akaanza kuniambia, Gavana alikuwa sahihi ile miaka ya 60s!! nami nikamuuliza "alikuwa sahihi kwa lipi?" akaniambia: Wakati nafanya kazi mkoani katika kitengo cha utafiti maralia kipindi hicho ndio tunapigania uhuru ilikuwa mwaka 1960, jamaa mmoja aliitwa Yusuf alichelewa kazini Asubuhi na kusababisha mjadala na Govana na mambo yalikuwa hivi:-
  Gavana: Yusuf Kwanini umechelewa kazini?
  Yusuf: Mimi sina Gari kama wewe!
  Gavana: Mbona jana uliwahi?
  Yusuf: Usinibabaishe wewe mzungu, kwanza siku zenu zinahesabika mtarudi kwenu muache kutunyanyasa!!!
  Gavana: ni kweli karibu tunarudi ulaya! lakini baada ya miaka 15 mtatufuata ulaya mkitubembeleza turudi Tanganyika
  Yusuf: Wewe Mgonjwa wa akili!!! tuje kuwabembeleza kwa lipi?!! [alizungumza kwa kejeli].
  Gavana: Ninyi Watanganyika hamuwezi kujiongoza. kwa hiyo baada ya huo muda serikali yenu haitakuwa na uwazo wa kuwatunza!!
  Yusuf: Kwanini?
  Gavana: Kwa sababu hamjui Kwiba
  Yusuf: How?!!
  Gavana: Ninyi mna tabia ya kuzoa hadi mtaji hamuangilii kiasi cha kuiba bali mnazoa tu. Sisi hatuibi pesa ya mtaji wala pesa ya serikali bali tunaiba leseni ya serikali. ndiyo sababu serikali inaendelea kupata faida zake ilhali nasi tunaendelea kuneemeka ikiwema na wafanyakazi. Ndio maana wewe kila mwisho wa mwezi unapata bonus lakini ninyi mtakapojitawala hutaipata hiyo bonus!!!.
  nimeyatafakari sana hayo mazungumzo hadi nimeamua niwahusishe
  UNA MAONI GANI KUHUSU HAYO MAJIBIZANO?
  NI MAJIBIZANO YA KWELI WALA SIJATUNGA!!
   
 2. W

  We know next JF-Expert Member

  #2
  Mar 10, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mkuu mazungumzo hayo yanatuweka uchi watanzania...kwa hakika ni matokea ya kutokuwajibika tunakokuona, ufisadi kukidhiri na mafisadi kushika dola. Maneno ya wazee ni busara sana, hasa wazee wa zamani sio hawa wa siku hizi wanaoitwa Diamond kila kukicha.
   
 3. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #3
  Mar 10, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ilibaki kidogo sana huyo Gavana angeitwa Nabii!!
   
 4. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #4
  Mar 10, 2012
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hatuibi mtaji tu, TUNAKOMBA KILA KILICHO MBELE YETU hata UCHAFU!
   
Loading...