Mkomamanga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2011
- 815
- 189
Mkuu hapo ilifungishwa ndoa kwa nguvu, si unaona!!!!
Ndoa ya mkeka ndo imezoeleka Zanzibar kwa hiyo hakukuwa na shida maana ndoa za mkeka ni ndoa za nguvu tu!
Mkuu hapo ilifungishwa ndoa kwa nguvu, si unaona!!!!
Ni kweli kabisa mkuu. Ishu haiko sawa kwani haijakamilika. Ni bora angesema huo ni mfano tu wa mkataba wenyewe.
Heshima zako mkuu,
Hivi haiwezekani mtu kufungua kesi kwenye mahakama ya kimataifa, I mean kesi kama zile za Mtikila kudai hizi article ambazo ziwekwe wazi.
Kama ikithibitika kwamba kweli haziko, basi maana yake hazikuwahi kuweko na hivyo muungano ni batili.
Sijui unasemaje na mnasemaje?
Mtoto anapotaka kuiona hati ya ndoa baina ya baba na mama yake inakueleza nini?.. bila shaka tatizo analo mtoto mwenyewe hajiamini kama kazaliwa na wazazi hao..
Mkataba wa muungano kasaini mkwawa na msekwa? Jamani!
Ilitakiwa na Zanzibar nako Bunge likaujadili huo Mkataba, tatizo mara baada ya Mapinduzi ya mwaka 1964 Zanzibar kulikuwa hakuna vongozi wa kuchaguliwa na wananchi. Na Zanzibar ilifanya uchaguzi wake wa kwanza miaka 16 baada ya Mapinduzi hapo mwaka 1980. Mkataba ungejadiliwa na nani wakati nchi ilikuwa inaendeshwa na wanamapinduzi chini ya Baraza la Mapinduzi Zanzibar?
Bunge lililopitisha mkataba tar 25/4, lilikuwa la Tanganyika peke yao au lilihusisha wazanzibari? Sijaona sehemu spika wa Zenji akitajwa.
Mimi naomba kuuliza,
Mapinduzi ya Zanzibar yalikuwa ni ya kwanza hapa East Africa. Mapinduzi mengine hapa East Africa ni yale yaliyotokea Uganda January 25, 1971 yaliyomuondoa Obote na kumuweka Idi Amin.
Hivyo, utawala wa Idi Amin na Karume unafanana kwa kitendo cha wote wawili kuingia madarakani kwa mapinduzi. Wote wawili hawakupigiwa kura hadi walipong'oka madarakani.
Sasa linakuja swali langu.
Je, iwapo baada ya mwezi tangu Amin kumpindua Obote, Nyerere angekuwa rafiki wa Amin na kwa urafiki huo tukaungana na Uganda kama tulivyoungana na Zanzibar, je muungano huo ungehesabiwa kuwa ulikuwa na ridhaa ya watu wa Uganda?
Wakati mnanijibu kumbukeni kazi ya mapinduzi duniani kwanza kabisa huondoa katiba iliyopo na vyombo vyake kama Bunge, mahakama na kadhalika na ndivyo ilivyofanyika Uganda na Zanzibar.
Natumaini majibu tele.