Huu ndio wizi wa vodacom mpesa!!!

HARRISON ONE

Member
Jan 8, 2014
42
30
Toka juzi majira ya saa kumi jioni Mtandao wa vodacom mpesa umekuwa haupatikani na hata ikitokea umebahatika kupata menyu ya mpesa bado ilikuwa ni vigumu kutoa au hata kuweka fedha kama ambavyo imezoeleka!! vodacom mpesa kwa makusudi kabisa wakijua kuwa mtandao wao una matatizo bado waliendelea kukata fedha za walalahoi ambao wamekuwa wakijaribu kuingia katika mtandao huo,kwa kutaka kuuliza salio,au hata kujaribu kutuma au kutoa fedha!!sasa kwa hali ya kawaida hii ni haki??mtu kutokupata huduma anayoihitaji but still unamkata fedha!!Mamlaka ya mawasiliano Tanzania,mnaliona hili?
 
Ni majanga ndugu yangu. sina hamu tena na Vodacom. Jana nilipatwa na matatizo nikaangalia salio mfukoni halitoshi nikampigia ndugu yangu anirushie hela kwa m pesa niliteseka sana. alituma ikawa hainifikii, na hata iliponifikia nikashindwa kutoa hela mpaka leo iko kwenye simu.
 
Kabla ya kulalamika unapaswa kuwapigia simu Vodacom kwanza vinginevyo tunawezaona ni majungu tu.
 
Mqmbo mengine huwa nashindwa kuelewa mnalalamika nini...hama hamia mtandao mwngne....

haijakukuta kaka hiii imeathiri watu wengi sana.....just imagine mgeni kashuka ubungo usiku na hela ipo mpesa.
 
Toka juzi majira ya saa kumi jioni Mtandao wa vodacom mpesa umekuwa haupatikani na hata ikitokea umebahatika kupata menyu ya mpesa bado ilikuwa ni vigumu kutoa au hata kuweka fedha kama ambavyo imezoeleka!! vodacom mpesa kwa makusudi kabisa wakijua kuwa mtandao wao una matatizo bado waliendelea kukata fedha za walalahoi ambao wamekuwa wakijaribu kuingia katika mtandao huo,kwa kutaka kuuliza salio,au hata kujaribu kutuma au kutoa fedha!!sasa kwa hali ya kawaida hii ni haki??mtu kutokupata huduma anayoihitaji but still unamkata fedha!!Mamlaka ya mawasiliano Tanzania,mnaliona hili?

Mkuu walaumu kwa mtandao kutokuwezesha kutuma ama kutoa pesa basi ila ukiuliza salio siku zote kuna fee kwa kazi hiyo na hupaswi kuwalaumu kumbuka hii ni Technology ambayo inaweza fail at some time na hata USA Mwaka 2001 walihesabu kura kwa mikono baada ya tatizo la Technology na pia Kenya Mwaka Jana na Hata Malawi Mwezi uliopita. Cha Msingi nashauri Vodacom Wajitahidi kurejesha huduma ila mie siwalaumu hata kidogo mkuu! Pole kwa kupingana na ww na pia si mfanyakazi wa Voda wala sina Line ya Voda kwa sasa.
 
Nashindwa kutoa hukumu kwa kusikiliza upande mmoja wa shilingi. Ila kama ni kweli nawapa pole wote walifikwa na matatizo hayo na nawaomba wayafikishe malalamiko yao panapohusika. Na mimi pia ni mteja mkubwa wa Vodacom na m-pesa.
 
Kabla ya kulalamika unapaswa kuwapigia simu Vodacom kwanza vinginevyo tunawezaona ni majungu tu.

Hata ukiwapigia customer care nao huwa hawana majibu ya kuridhisha mnaishia kukwaruzana bila sababu
 
Well said Mummy! Nice hedging technique nakubaliaa nawe lakini ukisema ulaumu na upate assurance ya active network throughout bila breakdown @ times ni sawa na kujiaminisha kuwa utaish milele kisa afya yako ni njema kwa ss na misuli mingi wakati wa ujana wako!
kwa sasa bila kuwa na simu/line mbili/tatu mambo hayaendi
 
  • Thanks
Reactions: lin
Mkuu walaumu kwa mtandao kutokuwezesha kutuma ama kutoa pesa basi ila ukiuliza salio siku zote kuna fee kwa kazi hiyo na hupaswi kuwalaumu kumbuka hii ni Technology ambayo inaweza fail at some time na hata USA Mwaka 2001 walihesabu kura kwa mikono baada ya tatizo la Technology na pia Kenya Mwaka Jana na Hata Malawi Mwezi uliopita. Cha Msingi nashauri Vodacom Wajitahidi kurejesha huduma ila mie siwalaumu hata kidogo mkuu! Pole kwa kupingana na ww na pia si mfanyakazi wa Voda wala sina Line ya Voda kwa sasa.

Nakubaliana na wewe kuwa its the matter of technology!!but kumbuka ili hizo switch kzao ziweze kufanya a particular action it must be COMMANDED to do so!!!hata hizo tsh 50 kwa kila transaction ya kuingia na kuuliza salio tu ni kuwa wameset zikate amount hiyo!!kama ni hivyo basi walikuwa wana nafasi nzuri ya kuamua hizo hela zisikatwe hadi wasolve technical problems za mitambo yao ya mpesa!!thats what l mean
 
kwa kweli vodacom ni majanga mi toka hiyo juzi transactions zote na fanya kwa tigo pesa kwa kweli wapo vizuri big up kwao
 
Wanafanya hivyo makusudi ili kujipatia hela haramu za kuulizia salio na kutuma hela. Imagine ni wateja wangapi wanatumia mpesa na kama kuna shida wanakimbilia kwenye balance. Wezi wakubwa nakampuni ya simu hela zao nyingi ni za wizi.
 
kama zali tu la mentali juzi jmosi saa 7 mchana nilitumiwa 1.5m kwa mpesa mda huo huo nikampigia wakala mmoja kuwa natoa laki 6 aniingizie tigopesa baada ya kumaliza kutoa na kuwekewa tigopesa kuna mtu nikataka kumtumia hela mpesa kila nikijaribu inagoma,
 
kuna mdau kanidokeza ati wanarekebisha viwango vya kukata hela ili kuongeza ushindani, nashindwa kuelewa connection ya kupunguza makato na kutopatikana huduma ya mpesa siku 3, ama tunaelekea kwenye DESI ya pili nini?
 
Na hakuna chombo chochote cha habari itazunguzmzia suala hili au kuwasema vodacom kwa kuwa watakosa matangazo
 
Back
Top Bottom