HUU NDIO URAFIKI WA KWELI!...muoneni x-pin na hommie wake kaizer enzi zao kule MKUU

hahahaa hii inafurahisha sana,xpin na kaizer!hapo wenyewe walikuwa wanajiona wajanja huwaambii kitu!lol
 
@Iribini na lile shati lako la JULIANA unalikumbuka?
 
heheheeh hii miondoko inaonekana kama panaenda kuibiwa kuku wa jirani sehem sehem.
 
Hapo sisi ambao baba zetu walikuwa mahediticha wa praimari skuli ndio tulikuwa tunapiga pamba kuliko watoto wote mtaani. Hiyo raba mtoni niliyoitinga umeiona lakini?

Dah! Usinikumbushe mbali mamushka. Ukitinga lile na safari buti zako..... aaah! tartiiiiibu unatesa kijijini.

heheheeh hii miondoko inaonekana kama panaenda kuibiwa kuku wa jirani sehem sehem.
Vipi, malaria imepanda kichwani? Yani kuku afukuzwe wakati watu tumetinga nguo za sikukuu?
 
hehehehehe!nimecheka hadi kichwa kinauma

Mpwazz biggy alitambia sana hiyo nyepesi nyepesi
hahaaaaaa that JULIANA name was connected na kaugonjwa fulani au mafaili yangu hayajakwa retrieved vizuri???
 
Umekosea kidogo. Hizo raba mtoni aliniletea anko wangu. Alivipora Uganda wakati wa vita dhidi ya Iddi Amin. Ulikuwa umezaliwa wewe?

Baelezeee hommie nakumbuka enzi izo chini nna "raba mtoni" kati nimepiga "michael Jaksoni" juu nna shati la bahama hapo tayari kwa kuelekea kwa Bakhresa kula Koni he he he those days bana nauli ya UDA shilingi moja tu!!
 
Mpwazz biggy alitambia sana hiyo nyepesi nyepesi
hahaaaaaa that JULIANA name was connected na kaugonjwa fulani au mafaili yangu hayajakwa retrieved vizuri???
Enzi hizo ndio kale kaugonjwa ketu ndio kalikuwa kanaingia. Basi ukitinga Juliana watu wanajua tayari umeshakanyaga adui wa Kakobe.
 
Hapo sisi ambao baba zetu walikuwa mahediticha wa praimari skuli ndio tulikuwa tunapiga pamba kuliko watoto wote mtaani. Hiyo raba mtoni niliyoitinga umeiona lakini?

hehee nimeliona lakuchumpa,hapo usikute mama anawasubiri sikukuu ikiisha raba inarudishwa sandukuni,ndo mana mnaonekana mko ktk mwendo wa kasi ili kuwahi kila sehemu raba ionekane.!ila chachacha za kaizer na huo mwendo lazima miguu ijae vumbi.lol
 
Enzi hizo ndio kale kaugonjwa ketu ndio kalikuwa kanaingia. Basi ukitinga Juliana watu wanajua tayari umeshakanyaga adui wa Kakobe.

ha ha ha hommie hapo kwenye RED nimecheka mpaka hangover inaanza kuisha!
 
hehee nimeliona lakuchumpa,hapo usikute mama anawasubiri sikukuu ikiisha raba inarudishwa sandukuni,ndo mana mnaonekana mko ktk mwendo wa kasi ili kuwahi kila sehemu raba ionekane.!ila chachacha za kaizer na huo mwendo lazima miguu ijae vumbi.lol
Hahaha! Ikifika saa 12 lazima raba unamkabidhi mama. Zinahifadhiwa mpaka sikukuu itakayofuata. Wakati huo madogo wanakuombea kwa Mungu mguu wako ukue ili sikukuu itakayofuata raba zikubane wao wakabidhiwe umiliki.
 
mi nilikuwa nakasirika sikukuu ikiisha mnaambiwa haya haya vueni hizo nguo,zinafuliwa halafu hizoo zinafichwa hehee kazi kweli those days.lkn ilikuwa raha jamani!
 
kipindi hicho muziki ulikuwa THENK YOU MISTAA DIIJAAAY AMERI MOTAAAAAAAAAAAA
 
Hehehe!
Wakati huo kina bht walikuwa bado kuzaliwa.
Sorry, natoka kidogo. Ngoja nikazimue naona mateso ya hangover yamenishinda nguvu.
 
kipindi hicho muziki ulikuwa THENK YOU MISTAA DIIJAAAY AMERI MOTAAAAAAAAAAAA

Yeee Masaweee.... Yesu Mkomboziiiii (Umkombothi hiyo ya Chakachaka ndio ilikuwa my fevareti). Wakati huo somo la kimombo linaanzia darasa la tatu......
 
Kikuku kinanukiaaaaaax2.....Yekeyeke kua yekeyeke (More kante).
Nani alishawahi kuvaa viatu vya omega (made in kenya)? Vilikua vya plastic ila kama vya ngozi veusi, tuliviita mwisho saa sita.
 
ikitoka hiyo dijei anaunganisha na MAIKO JAKSON NJOOOO SITAKIIII KAMA HUTAKI NENDA.LOL
halafu inafuata:

HOLIDEEEEEI..... IFI YU TUKU HOLIDEI....... Titititititit AND YU STATI SELEBREIT
Nikusihiii, nikusihi soooojaaaaa!
 
hehehhe...nimecheka kweli humu ndani mna vituko...

na kucheza 'MABREKA' jeee?hheehe
 
Back
Top Bottom