Huu ndio uongo wa Padri Mapunda kwa CCM na mapenzi yake Chadema

Mleta mada ebu angalia orodha hii ya watoto waliochaguliwa UVCCM/NEC kisha linganisha na upuuzi wako ulioandika hapo juu:

RIDHIWAN KIKWETE,DICKSON MEMBE,FRED LOWASSA, ASHURU HUSSEIN MWINYI,BENY SAMWEL SITTA,DEBORA MWANDOSYA, IREN PINDA,FELSTER NDUGAI,SHARIFAR BILAL, HAWA KIGODA,JUDITH MUKAMA NA JEROME MSEKWA.
 
kwa akili za ma drasa usitarajie ataona hayo majina kazi yake ni kupambana na ukristo na chadema tu ndio aliyomezeshwa jamani
 
Wewe mwenyewe ndio unaonekana mnafiki na mzandiki, kama aliohubiri Fr. Mapunda ni uongo, uzushi na uchonganishi, 1. Ungemtafuta mwenyewe ukamuelezea ili Aweze kujirekebisha. 2. Ungeenda kumshtaki kwa viongozi wake sasa ulivyolileta hapa jamvini umesaidia nini kumrekebisha?.
 
Siku hizi kila anapojitokeza mtu yeyote kuipinga ccm, serikali yake ama kiongozi wa ccm ama serikali imekuwa ni kawaida kusikia akiitwa Chadema.

Kwamba mwananchi asiye na itikadi ya chama chochote cha siasa hawezi kuipinga ccm na seikali yake!

Kwa maneno mengine nchi hii chama cha upinzani ni Chadema tu. Hao akina cuf, nccr mageuzi, udp, tlp na vyama vingine ni matawi ya ccm!
 
kwanza ni uongo mimi ninamfahamu vizuri babtist mapunda,amri ya said kalembo haikufanya kazi,kwani kalembo wala dhaifu hakuna mwenye mamlaka ya kuzuia makasisi wa kanisaq katoliki kuongoza ibada,ni askofu wa jimbo husika kwa mapadre wa jimbo,lakini ni mkuu wa shirika na askofu kwa mapadre wa shirika kama baptist mapunda.katika alioongea hakuna uzandiki ni ukweli tupu aliosema.nakushauri acha kutumia makalio kufikiri tumia ubongo badala yake.NAOMBA MODS MUONDOE UCHAFU ALIOWEKA HUYU JAMAA.NAWASILISHA.
UKANA SHILUNGO.
 
AKIONGOZA misa katika Kanisa Katoliki la Manzese jijini Dar es Salaam, Jumapili iliyopita, Padri Baptiste Mapunda "alikemea tabia ya kupeana uongozi ndani ya familia moja" akidai itakwamisha utendaji wenye tija na maendeleo.

Mapunda ambaye ameondokea kuwa ni "padri mwanasiasa wa kambi ya upinzani nchini", alisema hali hiyo inaongeza pengo kati ya matajiri na masikini, kisha akawashutumu viongozi wa kisiasa akidai wameua Azimio la Arusha alilodai lilianzishwa na Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere na kuligeuza kuwa "azimio la wala rushwa na ufisadi".

Alimfananisha Rais huyo wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mtume Musa akisema alitumia hekima na busara, kuwaondoa Watanzania katika ukoloni bila ya kutumia silaha, na kwamba wakati wote wa utawala wake hapakuwepo migomo ya walimu, madaktari au kuuawa kwa mwandishi wa habari.

"Jambo la msingi tuhakikishe rais anapunguziwa madaraka na matumizi ya vyombo vya dola yasiwepo katika siasa, viongozi wengi hawakuchaguliwa kwa haki na ndiyo maana taifa limekuwa na majanga makubwa", alisema kama alivyonukuliwa na gazeti moja la kila siku nchini, Jumatatu wiki hii.

Nimewahi kukorofishana hadharani na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Meja Jenerali Saidi Kalembo nikimtetea Padri Mapunda alipopigwa marufuku asiongoze ibada yoyote mkoani humo mwaka 2003, zuio alilopewa kwa sababu alikuwa akihubiri siasa za uchochezi.

Nilifanya hivyo kwa imani kwamba ilikuwa bahati mbaya na angejirekebisha kama kiongozi wa kiroho, jambo ambalo ameshindwa kulifanya kwa miaka tisa sasa tokea wakati huo.

Kila Mtanzania mwenye akili timamu anafahamu kuwa Padri Mapunda "alikemea tabia ya kupeana uongozi ndani ya familia moja" baada ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete kupitisha majina ya wanafamilia yake kugombea nafasi za kisiasa katika chama hicho.

Walioteuliwa kugombea ujumbe wa NEC kwa wilaya za Lindi Mjini na Bagamoyo, mkoa wa Pwani na kumwibua padri huyo kusema hayo ni mke wa Rais, Mama Salma Kikwete na mtoto wao, Ridhiwani Kikwete.

Wote pia hawakupata wapinzani katika kinyang'anyiro hicho na kisha wakashinda siku za uchaguzi huo, lakini mwanafamilia mwingine ambaye ni mdogo wa Rais huyo, Mohammed Kikwete aliyeteuliwa kugombea uenyekiti wa chama hicho wilayani Bagamoyo alianguka.

Huo ndio wivu mbaya kabisa alionao kiongozi huyo wa kiroho unaokwenda sambamba na chuki, fitina za malengo ya kisiasa, majungu na uchonganishi unaolenga kuwapandikizia hasira za uasi wananchi ili kukidhi matakwa yake mwenyewe na wapambe wake.

Anafanya kila anachoweza ili wafuasi wake wa kiroho wamfuate pia katika itikadi zake za kisiasa na chuki zake kwa Rais Jakaya Kikwete, familia yake, CCM na Serikali ya Awamu ya Nne.

Sitaki niaminishwe kwa namna yoyote kuwa mahubiri yake hayo ni agizo la Kanisa Katoliki kutoka popote, hivyo nitabaki naamini katika moyo wangu wote kwamba hayo ni matakwa yake mwenyewe ya kisiasa na siyo ya kiroho na hata vinginevyo.

Ni ajabu kwa padri kusimama katika altare kanisani na kusema uongo huku akiwa ameshika Biblia Takatifu, lakini pia ni dhambi zaidi kuhubiri uzushi unaolenga kuwachonganisha watu ili wafarakane kwa namna yoyote.

Harakati za Mama Salma Kikwete, Ridhiwani Kikwete na Mohammed Kikwete kugombea nafasi hizo za kisiasa katika CCM hazikuanzia mikononi mwa Rais Kikwete wala ndani ya NEC isipokuwa wilayani wanakotoka.

Zilianzia Lindi Mjini na Bagamoyo walikoomba kugombea nafasi hizo baada ya kujipima wenyewe, kisha wakajiridhisha kuwa wanakidhi masharti ya Ibara ya 14(1) – (3) ya Katiba ya Chama Cha Mapinduzi ya Mwaka 1977 Toleo la 2010 inayosema ifuatavyo:

"Mwanachama yeyote (wa CCM) atakuwa na haki ya kushiriki katika shughuli zote za CCM kwa kufuata utaratibu uliowekwa, haki ya kuhudhuria na kutoa maoni yake katika mikutano ya CCM pale ambapo anahusika, (na pia) haki ya kuomba kuchaguliwa kuwa kiongozi wa CCM na ya kuchagua viongozi wake kwa mujibu wa katiba na taratibu…".

Walifanya hivyo kwa kuchukua, kujaza na kurejesha fomu na kuambatanisha vielelezo vyote walivyotakiwa kuviwasilisha katika ngazi zote za mchakato huo mrefu ulioanzia wilayani, mkoani hadi kwenye vikao vya kitaifa ambako uteuzi wao ulifanywa kwa kuzingatia Katiba ya CCM na siyo kwa matakwa ya Kikwete au ya familia yao.

Wote wanakubaliana na masharti yote ya Ibara ya 5(1) – (19), na pia wanakidhi matakwa ya Ibara ya 7, 8(1) – (7), 12(1) – (2) na 15(1) – (9) za katiba ya chama chao hicho na masharti yote yaliyotajwa na Ibara ya 2(1) – (2), 3(1) – (2) na 5(1) – (2)(a) – (d) za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 Toleo la 2005 inayotumika sasa.

Kabla ya kuteuliwa na NEC kugombea nafasi hizo, hatua ambayo pia haikuwa ya mwisho ya kuzipata nyadhifa hizo ila hadi wawili kati yao waliposhinda katika uchaguzi mkuu wa ngazi zinazohusika, kila mmoja alipaswa kujitetea mwenyewe kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wilayani kwake ili kuomba wamchague, hivyo ni uzushi na uongo mkubwa kudai eti kuwa kuna tabia ya "kupeana uongozi ndani ya familia moja" katika CCM.

Hata Rais Kikwete naye akitaka kugombea nafasi yoyote katika chama hicho hapewi tu wadhifa huo na familia yake iwe na mkewe, watoto wake, wadogo zake, wajomba zake, shangazi zake, binamu zake, mama zake, baba zake wala vinginevyo.

Itabidi atimize masharti yote ya Ibara ya 5(1) – (19), 7, 8(1) – (7), 12(1) – (2) na 15(1) – (9) za Katiba ya CCM na matakwa yote yanayotajwa na Ibara ya 2(1) – (2), 3(1) – (2) na 5(1) – (2)(a) – (d) za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mtu anapokurupuka na kudanganya utadhani ni mganga wa kienyeji kama alivyofanya Padri Mapunda anakuwa moja kwa moja ni mzandiki kinywani na amesheheni wivu mwili mzima, chuki binafsi, uchonganishi na uchochezi kwa misingi ya kisiasa.

Ndiyo maana anadanganya pia kwamba eti viongozi wa serikali ya CCM waliua Azimio la Arusha na kuligeuza kuwa "azimio la wala rushwa na ufisadi" huku akijua anaongea uongo.

Kama ambavyo lilianzishwa mwaka 1967 na kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya vyama vya Afro – Shiraz Party (ASP) cha Zanzibar na Tanganyika African National Union (TANU) cha Tanzania Bara, wakati huo vikiwa ni vyama pekee vya siasa kila upande kabla ya kuungana na kuwa CCM ilipofika mwaka 1977, azimio hilo pia lilifanyiwa marekiebisho mapya ya msingi mwaka 1992 kwa njia zote halali.

Sababu kubwa zaidi iliyosababisha kufanywa kwa marekebisho hayo ni Tanzania kuingia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa, jambo ambalo linaelezwa katika Ibara ya 3(1) – (2) ya Katiba ya nchi hii.

Padri Mapunda mwenyewe anajua kwamba Azimio la Arusha ni imani ya kisiasa ya TANU na ASP na baadaye CCM, hivyo isingewezekana liendelee kuwepo hata baada ya nchi kuwa ya vyama vingi kwani kila chama kinakuja na imani, itikadi na sera zake.

Ndiyo maana mwaka 1992, Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM iliyokutana Zanzibar iliona haliwezi tena kuendelea, badala yake likabaki kuwa ni dhana inayotajwa katika Ibara ya 3(1) ya Katiba ya nchi inayosema kwamba "Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa, isiyokuwa na dini na yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa".

Kana kwamba haitoshi, padri huyohuyo na Watanzania wengine wanafahamu namna gani vyama mbalimbali vya siasa vinavyopingana, vile ambavyo kuna vingine havitaki Tanzania iendelee kuitwa "nchi ya kijamaa" kwa sababu hiyo ni itikadi ya kisiasa ya CCM.

Vipo vinavyotaka neno hilo liondolewe kwenye Katiba, hivyo endapo lingekuwepo hadi sasa ingekuwa fujo, vurugu na kutumika kuwa kichaka cha baadhi ya watu kuitukana CCM, serikali na viongozi wake, hivyo ni uongo mkubwa kudai limegeuzwa kuwa "azimio la wala rushwa na ufisadi" ila ni chuki zake mwenyewe za kisiasa.

Aidha, siyo kweli kuwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alifanya kazi peke yake ya kuwaondoa wakoloni hapa nchini, badala yake ilifanywa na Watanzania wote waliokuwepo wakati huo. Tunachoweza kusema ni kwamba yeye alikuwa ni kiongozi wao kupitia chama cha TANU kwa Tanzania Bara, halafu Sheikh Abeid Amaan Karume aliyekuwa Rais wa ASP akiongoza mapambano hayo huko visiwani Zanzibar.

Kama ni hekima au busara kamwe haziwezi kumwendea yeye peke yake ila Watanzania wote waliokuwepo, lakini wendawazimu wachache wamekuwa wakimtumia kuonyesha chuki zao za kisiasa dhidi ya viongozi wa serikali iliyopo madarakani hivi sasa.

Kuhusu madai kuwa wakati wote wa utawala wa Serikali ya Awamu ya Kwanza haukuwepo mgomo wowote, Padri Mapunda pia aliamua kuzungumza uongo huo kwa sababu ya chuki hizohizo, hasira za mgombea urais aliyekuwa akimuunga mkono mwaka 2010 kushindwa vibaya, hali iliyoepusha kuundwa kwa serikali ya ubaguzi wa kidini na hasa ukatoliki nchini.

Mwaka 1967, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiwemo aliyekuja kuwa Spika wa Bunge mwaka 2005, Samwel Sitta waligoma kwa madai ya kisiasa dhidi ya Serikali ya Awamu ya Kwanza, kisha wakatimuliwa na Mwalimu Nyerere mwenyewe hadi walipokuja kumwangukia na kuomba radhi.

Aidha, hakuna ubishi kwamba wakati wote wa Operesheni Vijiji vya Ujamaa mwaka 1974, maelfu ya Watanzania walishurutishwa kuhama kwenye makazi yao ya asili huku nyumba zao zikichomwa moto kwa mtutu wa bunduki, na pia kuna wengine walipigwa risasi na kujeruhiwa kwa namna moja ama nyingine hasa waliokuwa wakigomea zoezi hilo.

Ilipofika mwaka 1982, askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) cha Jeshi la Polisi waliopelekwa wilayani Tarime, mkoa wa Mara, walitumia nguvu za ziada kuzima uasi na kumwaga damu dhidi ya raia waliokuwa wakivunja sheria na kutotii mamlaka ya serikali iliyokuwepo madarakani kwa kuwapiga risasi.

Akihutubia kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mwaka 1986, wakati huo akiwa Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho, Mwalimu Nyerere pia aliunga mkono mauaji yaliyofanywa na askari hao wa FFU kwa wafanyakazi wa Kiwanda cha Sukari Kilombero mkoani Morogoro waliokuwa wamegoma, kufanya vurugu na kuandamana kinyume cha sheria.

"Kazi ya bunduki ni kuua, kumbe zipo kwa ajili ipi? Kama watu hawataki kutii sheria za nchi hata kama ni mbovu, wanapambana na polisi hapo unadhani askari watafanya nini wakati wana silaha hizo mikononi?" Alisema Mwalimu Nyerere alipokuwa akiitetea Serikali ya Awamu ya Pili kwa kupambana kikamilifu na uvunjifu wa sheria kwa makusudi.

Katika hali hiyo, ni uongo mkubwa kudai kwamba mauaji dhidi ya watu wanaofanya hivyo yameanza wakati wa utawala wa Serikali ya Awamu ya Nne, na pia ni uzushi kuwa Baba wa Taifa aliwaunga mkono wendawazimu wachache wanaovunja sheria kwa kutotii mamlaka zilizopo madarakani.

Kama Padri Mapunda angekuwa halitumii Kanisa Katoliki kuhutubii siasa za uchonganishi, uchochezi na ubaguzi asingefanya ubaguzi wa kidini na chuki, badala yake angefuata nyayo za bosi wake hata kama kwa kuvunga, Mhashamu Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ambaye ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam anakofanya kazi katika Parokia ya Manzese.

Lakini kwa sababu ana ubaguzi wa kidini na itikadi za kisiasa, Padri Mapunda amekuwa hasemi chochote wakati viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wanapotoa kauli za uchochezi na hatari.

Hakusema chochote wakati Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa alipotangaza kwa kinywa chake mwenyewe, tena hadharani kuwa Tanzania isingetawalika aliposhindwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010. Alisema nchi ingemwaga damu, na kwamba Rais Kikwete kamwe asingefika hadi mwaka 2015 akiwa bado madarakani ila angeng'olewa kwa mabavu kinyume cha sheria na katiba ya nchi hii.

Hakusema chochote pale Mbunge wa Arumeru Mashariki mkoani Arusha, Joshua Nassari aliposema mkutanoni kwamba Chadema ina mpango wa kufanya uhaini wa kuitenga mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro na kuanzisha Jamhuri ya Watu wa Kaskazini.

Naamini hakuwakemea kwa sababu ya itikadi za kisiasa, upendeleo na ubaguzi wa kidini kwa sababu ni wakristo wenzake huku Dk. Slaa akiwa padri wa zamani wa Kanisa Katoliki, halafu Nassari ni mtoto wa Mchungaji Samwel Nassari wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mlima Meru.

Hakukemea mauaji yaliyofanywa na polisi kwenye Msikiti wa Mwembechai jijini Dar es Salaam mwaka 1997, na pia hakusema chochote baada ya mauaji ya Pemba mwaka 2001 kwa vile Rais aliyekuwepo madarakani wakati huo, Benjamin Mkapa ni muumini wa Kanisa Katoliki.

Hafanyi kama Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ambaye amekuwa mstari wa mbele kutetea watu wote wanaovunja sheria, kuhatarisha amani au kutoa kauli za uchochezi bila ya kujali imani zao kiroho na kukemea matendo yote maovu.

Amekuwa akiwa akifanya hivyo huku akiwataka watu wote kuheshimu sheria za nchi, kutii mamlaka au serikali inayokuwepo madarakani kwa vile zote "zinawekwa na Mungu" kama inavyosema Biblia Takatifu.

Kabla sijafikia mwisho, sasa ninaomba nionyeshe kuwa kauli ya Padri Mapunda ya kukemea kile alichodai ni "tabia ya kupeana uongozi ndani ya familia moja" siyo lolote wala chochote ila ni uzandiki, fitina, uchochezi na harakati zake za kisiasa dhidi ya CCM.

Kama angekuwa anakerwa na hali hiyo, tena kwa vitendo angekuwa amewakemea viongozi wa Chadema kwa kuwajaza wake zao, dada zao, watoto wao na ndugu zao wengine bungeni kwa kivuli cha Viti Maalum.

Wakati wa kutafuta wabunge hao mwaka 2010, Kamati Kuu ya Chadema iliyafuta matokeo halali ya washindi waliopigiwa kura na akina mama wenzao katika Baraza la Wanawake la Chama hicho (BAWACHA), uchaguzi ambao ulifanyika kikatiba katika Ukumbi wa PTA uliopo kwenye Uwanja wa Sabasaba, Mtoni jijini Dar es Salaam.

Katika uchaguzi huo uliosimamiwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ambaye pia ni Mshauri wa Kisiasa wa Chadema na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Mkumbo Kitilya, washindi wengi waling'olewa kwa sababu tu walitoka kwenye kambi inayomuunga mkono Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.

Waling'olewa kwa sababu hawakutoka kambi ya Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu, Dk. Wilborad Slaa na viongozi wengine wa kitaifa. Hapo ndipo uchaguzi huo ulipofutiliwa mbali na badala yake, wabunge hao wakateuliwa ofisini kwa kuangalia familia zao au mahusiano mengine kati yao na viongozi waandamizi wa chama hicho.

Baadhi ya wabunge hao ni Rose Kamili ambaye ni mke wa Dk. Slaa, Christina Lissu (dada yake na Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu wa Chadema, Tundu Lissu) na Raya Ibrahim Khamis, mtoto wa dada yake na Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Zanzibar), Saidi Issa Mzee.

Wengine ni Mhonga Saidi (binamu yake Zitto), Anna Komu (shemeji yake Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Anthony Komu), Lucy Owenya (binti wa Mwenyekiti wa Chadema wa Mkoa wa Kilimanjaro na Mjumbe wa Kamati Kuu, Philemon Ndesamuro) na Grace Kiwelu ambaye ni mke wa mtoto wa Ndesamburo na kadhalika.

Huu ndio uongo, uzushi, umbeya na uzandiki unaofanywa na Padri Baptiste Mapunda dhidi ya CCM na serikali yake, ule ambao unakwenda sambamba na mapenzi yake makubwa ya kisiasa kwa Chadema katika upande wa pili!

Nguvu kuubwa kuandika mlolongo wa habari na mapovu juu....kisa!!

Shida yako tumegundua kuwa ni 'Magamba yamekuziba macho' kama Saulo ktk biblia enzi hizo alivyopigwa na upofu kwa matendo yake maovu, hadi alipoongoka..., na hivyo Wewe, unatakiwa 'uongofu' ili uongoke, magamba yakudondoke ili uone yanayoendelea duniani katika ukweli halisi.
Kama ulikuwa muumini safi, ungelisemea tatizo lako katika vikao vya walei, au kamati za kanisa hilo! Kwa vile unaonekana wazi 'ulitumwa' wewe ndiyo ibilisi mpotoshaji...! Na kama si muumini ulikuwa umeendafanya nini kanisani hadi kuyasikia mahubiri yake?? Ila kwa ulivyojieleza, umeonekana wazi kuwa wewe ni miongoni mwa hilo 'kundi la waoga' (informers) wanatumwa kusikiliza na kukusanya yale wananchi wanasemaje kila pahala hadi ktk nyumba za ibada za wengine, ili kupeleka kuwatuliza 'Wakuu wenu' waliojaa wasiwasi, ambao ndio wanaopenda kuyasikia uliyosema pamoja na mengine unayowasilisha kwao ili 'upate sifa kuwa unafanya kazi nzuri' waweze kujituliza kuondoa woga! Ole wenu!

Tunajua, CCM wanaogopa sana kauli za raia yoyote yule inayowafichua uovu wao kwa jamii! Mnataka jamii yote ibakie wajinga! Wewe ukiwa miongoni wa hao waoga, taifa halitabaki nyuma kwa wizi na uoga wenu, na taarifa za uongo kama za akina IHEMA et al...! NOT NOW...NO WAY LATER!!

Kwa taarifa yako, hakuna alichoongea Padri Mapunda kilicho tofauti na ukweli ambao kila mwananchi wa sasa anaujua!...Wewe kaa chini, tubu na uongoke, magamba yatakutoka machoni, utafunguka macho, utaona taifa linakokwenda!! ...la sivyo, Ulale pema!!
 
Siku hizi kila anapojitokeza mtu yeyote kuipinga ccm, serikali yake ama kiongozi wa ccm ama serikali imekuwa ni kawaida kusikia akiitwa Chadema.

Kwamba mwananchi asiye na itikadi ya chama chochote cha siasa hawezi kuipinga ccm na seikali yake!

Kwa maneno mengine nchi hii chama cha upinzani ni Chadema tu. Hao akina cuf, nccr mageuzi, udp, tlp na vyama vingine ni matawi ya ccm!
I hope wale Hopeless wa Nepi waliotumwa huku watasoma hii na kuielewa.
 
mtoa mada unawadanganya Watanzania.nimeamini kuna watu ambao kwao UZUSHI ni sehemu ya maisha yao.Padri Mapunda hakusema hayo uliyoandika hapo.Alikuwa anafundisha maana na umuhimu wa upendo katika familia.Hayo uliyoandika ni ya kwako mwenyewe.
Umetumia siku tatu kutunga uzushi huu,mwombe msamaha Padri Mapunda.
 
AKIONGOZA misa katika Kanisa Katoliki la Manzese jijini Dar es Salaam, Jumapili iliyopita, Padri Baptiste Mapunda “alikemea tabia ya kupeana uongozi ndani ya familia moja” akidai itakwamisha utendaji wenye tija na maendeleo.

Mapunda ambaye ameondokea kuwa ni “padri mwanasiasa wa kambi ya upinzani nchini”, alisema hali hiyo inaongeza pengo kati ya matajiri na masikini, kisha akawashutumu viongozi wa kisiasa akidai wameua Azimio la Arusha alilodai lilianzishwa na Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere na kuligeuza kuwa “azimio la wala rushwa na ufisadi”.

Alimfananisha Rais huyo wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mtume Musa akisema alitumia hekima na busara, kuwaondoa Watanzania katika ukoloni bila ya kutumia silaha, na kwamba wakati wote wa utawala wake hapakuwepo migomo ya walimu, madaktari au kuuawa kwa mwandishi wa habari.

“Jambo la msingi tuhakikishe rais anapunguziwa madaraka na matumizi ya vyombo vya dola yasiwepo katika siasa, viongozi wengi hawakuchaguliwa kwa haki na ndiyo maana taifa limekuwa na majanga makubwa”, alisema kama alivyonukuliwa na gazeti moja la kila siku nchini, Jumatatu wiki hii.

Ndugu mtoa mada naona umeandika kwa kirefu sana; lakini kwa kusema ule ukweli ni kwamba uliyoandika yote mimi binafsi naona kama wewe ndiye unayetaka kuleta uchochezi hapa nchini.

Viongozi wa dini zote wapo kwa ajili ya kazi ya kiroho na kukosoa mabaya. Kumbuka ukweli unaweza kukupeleka kaburini. mfano Yohane Mbatizaji alikatwa kichwa kwa kusema ukweli.

Lakini haina maana kuwa Yohane Mbatizaji alikuwa anafanya kazi za Siasa kwa kumueleza ukweli Mfalme Herode kwa kitendo cha kumchukua Mke wa ndugu yake.

Yohane alikuwa anakemea kitendo kile na si kwamba alikuwa anaingilia mambo ya familiya.

Hivyo hata padri Mapunda alikuwa anakemea maovu yeye akiwa kama kiongozi wa kidini. hana kosa pale.

Ndugu yangu fikiria jambo lingine la kuitetea Serikali ya Kijambazi hii. Na kamwe usifananishe na Uongozi wa Mwalimu Nyerere. Eti walikuwa wanaua PTYUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUU!!!!!!!

Je, enzi hizo kulikuwa na mauaji ya kijinga kama haya tunayoshuhudia leo!!!!!!!

SHAME UPON YOU!!!!!!!!!!

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Huo ndio wivu mbaya kabisa alionao kiongozi huyo wa kiroho unaokwenda sambamba na chuki, fitina za malengo ya kisiasa, majungu na uchonganishi unaolenga kuwapandikizia hasira za uasi wananchi ili kukidhi matakwa yake mwenyewe na wapambe wake.

Anafanya kila anachoweza ili wafuasi wake wa kiroho wamfuate pia katika itikadi zake za kisiasa na chuki zake kwa Rais Jakaya Kikwete, familia yake, CCM na Serikali ya Awamu ya Nne.

Sitaki niaminishwe kwa namna yoyote kuwa mahubiri yake hayo ni agizo la Kanisa Katoliki kutoka popote, hivyo nitabaki naamini katika moyo wangu wote kwamba hayo ni matakwa yake mwenyewe ya kisiasa na siyo ya kiroho na hata vinginevyo.

Ni ajabu kwa padri kusimama katika altare kanisani na kusema uongo huku akiwa ameshika Biblia Takatifu, lakini pia ni dhambi zaidi kuhubiri uzushi unaolenga kuwachonganisha watu ili wafarakane kwa namna yoyote.

Kama Padri Mapunda angekuwa halitumii Kanisa Katoliki kuhutubii siasa za uchonganishi, uchochezi na ubaguzi asingefanya ubaguzi wa kidini na chuki, badala yake angefuata nyayo za bosi wake hata kama kwa kuvunga, Mhashamu Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ambaye ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam anakofanya kazi katika Parokia ya Manzese.

Lakini kwa sababu ana ubaguzi wa kidini na itikadi za kisiasa, Padri Mapunda amekuwa hasemi chochote wakati viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wanapotoa kauli za uchochezi na hatari.

Huu ndio uongo, uzushi, umbeya na uzandiki unaofanywa na Padri Baptiste Mapunda dhidi ya CCM na serikali yake, ule ambao unakwenda sambamba na mapenzi yake makubwa ya kisiasa kwa Chadema katika upande wa pili!

Ndugu najua umepoteza muda wako mwingi katika kuandika makala hii.

LAkini uelewe pia kuwa haya unayotaka kutuletea hapa ni uchonganishi. Unaanza kuingilia mambo ya Kanisa Katoliki na viongozi wake. Elewa kuwa Kanisani hakuna Imani za Kisiasa kwa sababu Kanisa lina waumini wa itikadi tofauti.

Hivyo mimi binafsi nakuomba samahani sana usituletee mgogoro ndani ya Kanisa Katoliki, nenda kwa hao waliokutuma kuandika Pumba hizi ukawaeleze kuwa Kanisa Katoliki ni Kanisa la Kitume na usituchanganye na njaa zenu za madaraka. Umekosa ya kuandika hadi uandike upumbavu huu kuleta mgogoro Kanisa Katoliki.

Wewe ni nani hata useme eti ulimtetea Padri Mapunda huko Songea, Mungu peke yake anayeweza kumtetea mtumishi wake. Mbona hukuwatetea na Wananchi wasio na hatia waliouawa na Afande Michael Kamuhabwa kule Ruvuma!!!!!!!!

Tunaomba liacheni Kanisa Katoliki liendelee na kazi ya kuhubiri injili kama unakwenda Kanisani kusali ni heri lakini kama unafuata chokochoko utatuletea balaa.

MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
Hivi kwa akili yako unategemea Padri Mapunda atakuwa chama gani.

hapa cdm wameshikwa pabaya. Hakuna hata mmoja anayeweza kuja na hoja za kupinga yaliyoelezwa hapo juu.

Rangi yao halisi inazidi kudhihiri, kumbe wana wapiga kampeni mpaka makanisana.

Tuendelee kuwaelimisha watanzania juu ya uhalisia wa cdm na hatari yao kwa taifa letu.
 
Nimewahi kukorofishana hadharani na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Meja Jenerali Saidi Kalembo nikimtetea Padri Mapunda alipopigwa marufuku asiongoze ibada yoyote mkoani humo mwaka 2003, zuio alilopewa kwa sababu alikuwa akihubiri siasa za uchochezi.
Nilifanya hivyo kwa imani kwamba ilikuwa bahati mbaya na angejirekebisha kama kiongozi wa kiroho, jambo ambalo ameshindwa kulifanya kwa miaka tisa sasa tokea wakati huo.
!

Mkuu acha Umbeya, Mkuu wa Mkoa hana hayo Mamlaka, Mkuu Magamba mpoje!!!!! Wezi nyie, Wa Mbeya nyie yan kila Tabia Mbaya nyie
 
Ndugu najua umepoteza muda wako mwingi katika kuandika makala hii.

LAkini uelewe pia kuwa haya unayotaka kutuletea hapa ni uchonganishi. Unaanza kuingilia mambo ya Kanisa Katoliki na viongozi wake. Elewa kuwa Kanisani hakuna Imani za Kisiasa kwa sababu Kanisa lina waumini wa itikadi tofauti.

Hivyo mimi binafsi nakuomba samahani sana usituletee mgogoro ndani ya Kanisa Katoliki, nenda kwa hao waliokutuma kuandika Pumba hizi ukawaeleze kuwa Kanisa Katoliki ni Kanisa la Kitume na usituchanganye na njaa zenu za madaraka. Umekosa ya kuandika hadi uandike upumbavu huu kuleta mgogoro Kanisa Katoliki.

Wewe ni nani hata useme eti ulimtetea Padri Mapunda huko Songea, Mungu peke yake anayeweza kumtetea mtumishi wake. Mbona hukuwatetea na Wananchi wasio na hatia waliouawa na Afande Michael Kamuhabwa kule Ruvuma!!!!!!!!

Tunaomba liacheni Kanisa Katoliki liendelee na kazi ya kuhubiri injili kama unakwenda Kanisani kusali ni heri lakini kama unafuata chokochoko utatuletea balaa.

MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!

mkuu usimuombe, toa hoja za kukanusha alicho sema.

Bibilia inatuambia tuseme kweli itatuweka huru.

Kanisa linachochea sana udini katika nchi yetu na ushahidi umetolewa hapo juu.

Tuseme kweli hatakama inauma, kuendelea kunyamaza ni kulea maovu.

Kama yatakuja kutokea machafuko ya kidini tanzania (MWENYEZIMUNGU NA ATUEPUSHE) basi kanisa litakuwa ndio chanzo kikuu.
 
Mleta mada ebu angalia orodha hii ya watoto waliochaguliwa UVCCM/NEC kisha linganisha na upuuzi wako ulioandika hapo juu:

RIDHIWAN KIKWETE,DICKSON MEMBE,FRED LOWASSA, ASHURU HUSSEIN MWINYI,BENY SAMWEL SITTA,DEBORA MWANDOSYA, IREN PINDA,FELSTER NDUGAI,SHARIFAR BILAL, HAWA KIGODA,JUDITH MUKAMA NA JEROME MSEKWA.

kwahiyo tunapima ukubwa wa kosa kati ya cdm na ccm?

Kosa ni kosa, linatakiwa likemewe.
Alie ua watu 3 na alieua 8 wote ni wauaji.
 
Mkuu acha Umbeya, Mkuu wa Mkoa hana hayo Mamlaka, Mkuu Magamba mpoje!!!!! Wezi nyie, Wa Mbeya nyie yan kila Tabia Mbaya nyie

jibuni hoja, acheni porojo.
Mleta mada kafafanua mambo mengi na kwa ushahidi, mngemjibu kwa hoja mngeeleweka.
 
Back
Top Bottom