HUU ndio UNAFIKI wa WAANDISHI wa HABARI TANZANIA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

HUU ndio UNAFIKI wa WAANDISHI wa HABARI TANZANIA

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mizambwa, Sep 14, 2012.

 1. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #1
  Sep 14, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Ajali zaua 1,800 nchini


  na Mwandishi wetu


  JUMLA ya Watanzania 1,800 wamepoteza maisha katika ajali mbalimbali zilizotokea nchini kati ya Januari na Juni mwaka huu.

  Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Silima, alipokuwa akikabidhiwa stika za Wiki ya Nenda kwa Usalama zilizotolewa na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Kampuni ya mafuta ya Puma.

  Alisema katika katika kipindi hicho zilitokea ajali 11,163 ambazo mbali na kusababisha vifo hivyo, pia zimesababisha watu 9,000 kupata ulemavu wa kudumu.

  “Kulingana na takwimu hizo, maana yake ni kwamba kila siku watu 10 wanapoteza maisha kwa ajali. Hatuwezi kuruhusu hali hii iendelee.

  “Nawashukuru wadhamini kwa kampeni ya Wiki ya Nenda kwa Usalama mwaka huu Kampuni ya Airtel na Puma kwa kutoa mchango wao pamoja na kushirikiana na Jeshi la Polisi Usalama Barabarani kufikia malengo kwa kuhakikisha usalama wa raia na kupunguza ajali za barabarani,” alisema.

  Pamoja na hilo, aliwahimiza watu wanaomiliki vyombo vya moto kwenda kukaguliwa ndani ya wiki hiyo na kwamba wasiofanya hivyo watachukuliwa hatua za kisheria.

  Aidha, alisema katika wiki ya maadhimisho hayo watatoa mafunzo maalumu kwa waendesha pikipiki, kwani ajali nyingi zinazotokea zinahusu vyombo hivyo.

  Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Airtel, Beatrice Singano, alisema kampuni hiyo inajivunia kuwa sehemu ya juhudi za kuokoa maisha ya Watanzania na mali zao.

  Naye Mkurugenzi Mkuu wa Puma, Maregesi Manyama, alisema moja ya malengo ya kampuni hiyo ni usalama kazini kwa kutopata ajali, hivyo mchango wao huo utafanikiwa ikiwa utafanikisha kuepusha kifo hata kimoja.
  ========================================================================================================

  Source: Tanzania Daima, Mwananchi tarehe 13/09/2012 Pia Taarifa ya Habari saa mbili usiku ITV tarehe 13/09/2012.
  ====================================================================================================

  MYTAKE: Sasa waandishi wa habari ambao walisema kuwa wanagoma kuandika habari zote zinazohusu jeshi la Polisi, na hususani wiki ya "Usalama Barabarani", wameishia wapi??? kwani habari hii inahusu Wiki ya Usalama barabarani na wanaohusika ni jeshi la Polisi, tena Waziri Nchimbi ameongea, hata jana ITV tumemuona!!!!

  Je, kwanini walimfukuza pale jangwani?? au ndio unafiki wetu Watanzania????

  Sikutegemea habari zhizi kutoka katika vyombo hivi ningeona katika gazeti Habari Leo, uhuru, Mzalendo au Radio Uhuru, TBC1 hapo nisingelikuwa na la kusema.

  Waandishi tuelezeni harakati zenu zimeishia wapi??????  MIZAMBWA
  IANNIUMA SANA!!!
   
 2. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #2
  Sep 14, 2012
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Asante sana umenisaidia kuliona hili, hata mimi nimeshangazwa sana, sijui njaa au nini? waandishi wafafanue basi ni habari gani juu ya polisi ambazo hawataandika! maana pia gazeti la jana la Mwananchi kuna picha ya kamanda mmoja simkumbuki vizuri akiwa ameonesha silaha walizo kamata! sasa mimi nikajiuliza waandishi kulikoni?
   
 3. REMSA

  REMSA JF-Expert Member

  #3
  Sep 14, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,569
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hawana lolote wanafiki wakubwa,ilikuwa hivihivi ilipofungiwa mwanahalisi,wanaibukaga kwwa msisimko halafu kila mmoja anaangalia maslahi yake.Mtu kama Meena toka pale jangwani alishajionyesha ni mnafiki kwa kujifanya kumpoza Nchimbi.Eleweni Mungu hadhihakiwi,yamemkutamwangosi kesho kwenu.
   
 4. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #4
  Sep 14, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Kuna member humu simkumbuki jina ila alitumia neno ".........bahasha zetu zileeee..."
   
 5. Ben Mugashe

  Ben Mugashe Verified User

  #5
  Sep 14, 2012
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 939
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Mhariri wa Mwananchi ni Katibu wa Jukwaa la Wahariri TZ, Ndugu yangu Nevine Meena..Sijui hili tamko halikuwa la jukwaa?
   
 6. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #6
  Sep 14, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Inaonyesha walikuwa wanajitafutia umaarufu kwa kupitia mgongo wa kifo cha Mwangosi. Walisema mengi sana hata katika maandamano yao walichonga sana. Na wananchi wakasema sasa ngoma imepata wachezaji.

  Kumbe ngoma yenyewe ya "KITOTO" haikeshi.

  Kusema ukweli kama misimamo yenu ndio hii, mmejidhadharirisha sana ndugu Waandishi.  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
Loading...