Huu ndio ukweli:mkianza kupeana kuwandana sumu wenyewe kwa wenyewe nani atawaokoa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huu ndio ukweli:mkianza kupeana kuwandana sumu wenyewe kwa wenyewe nani atawaokoa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MTENDAHAKI, Apr 2, 2012.

 1. M

  MTENDAHAKI JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,992
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  CCM imeshindwa vibaya arumeru mashariki katika kinyang'anyiro cha ubunge wa jimbo hilo lililoachwa wazi na marehemu jeremiah sumari!kushindwa kwa ccm hakujatokea kwa bahati mbaya,kiukweli hata kura hizo walizozipata ni nyingi mno na inaonyesha ni namna gani nguvu kubwa ilitumika kuwashawishi wananchi!najenga hoja hii kwa sababu uwezekano wa ccm kushindwa ulikuwa mkubwa mno kuliko kupata ushindi!sababu za ccm kushindwa ni hizi 1. CCM imegawanyika pande kuu mbili ambazo zinapingana kwelikweli wakati chadema ni wamoja sana (msisahau maneno ya wazee" umoja ni nguvu....") 2. CCM wanatuhumiana wao kwa wao kupeana sumu, na wanawindana kwelikweli kati ya makundi hayo mawili yanayohasimiana sana huku kundi moja likiwa na nguvu kubwa ya pesa ilihali lingine likungwa mkono na wanamapinduzi ambao hawajapoteza muelekeo 3.ccm ilikwenda na pesa zake za mfukoni kuwashawishi wananchi wakati chadema walienda kuomba kuwatumikia wananchi 4. CCM hawakutakiwa kueleza namna watakavyotatua matatizo na kero za wananchi kwani wao ndio waliokuwa wakishikilia jimbo bali walitakiwa waseme wametatua kero ngapi na ni ngapi zingine ziko kwenye hatua gani 5. Ahadi hewa lukuki zisingeweza kukinusuru chama hiki kwani kimeshindwa kutekeleza ilani yake kwa vitendo 6. Kitendo cha kuifanya nchi hii kuwa ya kifamilia kimeigharimu mno ccm arumeru,nchi hii ina watu wengi sana wanaoweza kushika madaraka na hakuna sababu ya kurithishana hii sio nchi ya kifalme 7. Vijana hawana nafasi ya kutosha kwa usawa ndani ya ccm labda uwe mtoto wa kigogo tofauti na ndani ya chadema ambako vijana wana usawa bila kujali wewe ni mjukuu wa ndesamburo au mtei huu ni mwanzo wa safari ya kifo cha kudumu cha ccm, na kwa namna hii watu wamebaki kujiegesha ccm kwa sababu ni chama tawala tu, siku kikianguka hakitainuka tena! Ni muda wa kufanya mabadiliko na kujirekebisha ili ccm itakapokuwa chama cha upinzani baada ya uchaguzi wa mwaka 2015 kilete changamoto za kweli kwa chadema asanteni wadau
   
Loading...