Huu ndio ukweli kuhusu andiko linalomtuhumu DC wa Tabora Mjini, Komanya Kitwala kutokuwa na maelewano na watumishi

Mkuu wa Wilaya Cheo kimemzidi ukubwa,sidhani kama aiipelekwa semina.kufundishwa majukumu ya mkuu wa Wilaya,sidhani kama anayo miongozo ya ukuu wa wilaya,mapepe mengi na kutembea na saa 48 mfukoni ndio anachokumbuka kijana mwenzenu Komanya.hajui chochote kuhusu team work,intergrity,communication skill,flexibility and other leadership skill.anachojua ni matusi,kidhalilisha viongozi na kujimwambafy kwamba kazaliwa familia bora.
 
Halafu Kuna tuhuma ya Fedha za harambee kudhibitiwa na mtu mmoja,nimesikia kwamba yeye ndiye muhasibu ,ndiye mtunza kumbukumbu,yeye peke yake ndiye anajua nani katoa nini na nani hajatoa.

Yeye ndiye anagawa ,watu wanahoji Check and Balance.

Mkaguzi akitaka kujiridhisha kukagua matumizi ya hizo fedha ataanzia wapi?

Mbona mkurugenzi ambae ndiye acconting Officer wa manispaa hashirikishwi? Au ataiba?
 
Tabora kuna shida,pamoja na kuwa hatupo huko lakini ukiona pahala kuna moshi ujue kuna moto,kilichonitisha ni kiongozi wa juu katika wilaya kutoelewana na watendaji wake.

Hatua za haraka zichukuliwe,na hapa kuna machaguo mawili tu,kuhamisha wakuu wa Idara wote na mkurugenzi wao au kumuhamisha huyo Mkuu wa Wilaya anaelalamikiwa.

Kuna mahala kwenye andiko la kumshambulia DC watu wa Usalama wametajwa kwamba nao vijana wao waliwahi kufurushwa kwenye kikao kwa mtindo wa kufokewa,Idara hii kwakuwa ninaimani nayo,inaweza kusaidia kuweka wazi ukweli na kutamatisha kinachoendelea Tabora.

Viongozi wenye mamlaka wafanye maamuzi mapema kabla mambo hayajaharibika.
Maana kama hata madiwani wa CCM hawelewani na DC wao kuna shida.
 
kavyilu, Binafsi hata ilo la kushindwa kuelewana na viongoz wa chama naliona ni doa Kubwa Sana kwa DC.

Nashindwa kuelewa iyo ilani ya chama anaitekelezaje Kama haelewani na viongoz wa chama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ndiyo hujui taratibu za utoaji zabuni serikalini! Hakuna zabuni inatolewa bila kutangazwa hata kama kuna mtu ameshapangwa zabuni lazima itangazwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo statement ya Makamu wa rais ya Tabora mnataka kuletewa malaika?

Maana yake ni kwamba huyo DC ni kimeo ila kwa lugha ya kiutu uzima huyo mama anawaambia mvumilieni tu huyu DC na mapungufu yake,hio ni lugha ya kiutu uzima aliitumia hapo.


Hii statement ya
Mkuu wa Wilaya alipoingia madarakani aliwapa mbinu Halmashauri juu ya kuongeza mapato, ambapo baada ya hapo yalipanda sana kuanzia mwezi Oktoba mpaka February 2019.

Ni ya kujimwambafai sana kwamba DC ushauri wake uliongeza mapato na yakapanda sana,hahah
 
Hiyo statement ya Makamu wa rais ya Tabora mnataka kuletewa malaika?

Maana yake ni kwamba huyo DC ni kimeo ila kwa lugha ya kiutu uzima huyo mama anawaambia mvumilieni tu huyu DC na mapungufu yake,hio ni lugha ya kiutu uzima aliitumia hapo.


Hii statement ya
Mkuu wa Wilaya alipoingia madarakani aliwapa mbinu Halmashauri juu ya kuongeza mapato, ambapo baada ya hapo yalipanda sana kuanzia mwezi Oktoba mpaka February 2019.

Ni ya kujimwambafai sana kwamba DC ushauri wake uliongeza mapato na yakapanda sana,hahah
Mkuu 'muziki' wa makamu wa rais unaufahamu lakini, au unaongea kujifurahisha?

Huyo ni simba jike lisilotisha kwa umbile lakini ndiyo windaji la hatari!

Hata siku1 hana uvumilivu kwenye 'mauozo', kungelikuwa na 'madudu' huyo Dc angeliondoka naye hima!

Kamuulize Rc mtumbuliwa Chiku Galawa wa Songwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu wana JF

Kumetokea juzi andiko ambalo linamtuhumu Dc wa tabora mjini ,Mh. Komanya Kitwala kwa mambo mbalimbali , kiufupi hayo mambo ni ya kutunga na uzushi mkubwa ambao unazushwa na wanufaika wa ufisadi na watu waliozoea kufanya kazi kwa mazoea.

Uzi wa tuhuma huu hapa Mkuu wa Wilaya ya Tabora ndugu Erick Komanya Kitwala hana maelewano na mtumishi yeyote ndani ya wilaya anayoiongoza

UKWELI NI HUU HAPA
  • Mkuu wa Wilaya alipoingia madarakani baada ya kuteuliwa alikuta kuna zabuni ya shilingi bilioni 4.2 ujenzi wa barabara za kwa Nyembo, Transfoma, Kuya, Heri na Nyerere.Katika zabuni hiyo Halmashauri ilitaka kumpa mtu zabuni bila kufuata utaratibu wa zabuni wa kutangaza, ambapo Mkuu wa Wilaya aliingia kati na kuamuru itangazwe na hatimaye kuleta mvutano ambapo Halmashauri ilikataa kutangaza na hatimaye viongozi wa juu wakaingikia kati na zabuni ikatangazwa na hivyo yule mtu waliyemtaka Manispaa akakosa kazi hiyo na akapata mtu mwingine.

  • Mvutano huu ulikuwa baina ya madiwani walioko katika Kamati ya Fedha, Mkurugenzi na watu wa manunuzi dhidi ya DC.Baada ya vita hiyo ya DC kusimamia Utaratibu na kufuatwa, kukawa na vita ya chini kwa chini.Ambapo mwaka huu 2019, mwezi Februari , Makamu wa Rais alitembelea Tabora ambapo baadhi ya madiwani waliaandaa mpango wa kumchafua DC, sababu tu alizuia zabuni kutoka kiholela bila Utaratibu kwa msukumo wa madiwani, hivyo baadhi ya madiwani waliozoea kutumika na wafanyabiashara walichanga hela na kumpa Mzee mmoja aitwaye MALIFEDHA ili atumike kumchafua DC kwa makamu wa Rais, kuwa DC hafai, n.k , Bahati nzuri Makamu wa Rais Mama Samia, alipopewa tuhuma hizo aliwatuma watu wake wachunguze, na walipochunguza wakagundua kuwa ni njama na Mkuu wa Wilaya hana hatia bali ni chuki na majungu yanapikwa.

  • Baada ya uchunguzi na kupata taarifa sahihi, katika Vikao vya majumuisho ya ziara yake mkoa wa Tabora , aliwaambia waache majungu na pia kwenye mkutano wa nje aliwaambia watumishi wa serikali na viongozi wa kuchaguliwa wafanye kazi waache kuchafuana ( Rejea clip za ziara You tube). Pia alisisitiza akisema watu wa Tabora acheni majungu...Mnataka kuletewa malaika?

  • Wakati DC anaingia madarakani mwezi wa 9 mwaka jana 2018 alikuta Halmashauri inazo milioni 400 za ujenzi wa Kituo cha Afya cha Maili 5.Mpango uliokuwepo ni kutaka kuongeza majengo mawili ya nyumba za wachina waliyoyaacha baada ya mradi kukamilika ,nyumba walozokuwa wanakalia ziko Maili 5 , viongozi walitaka kutafuna pesa za majego mapya kwa kufanya replacement ya majengo ya wachina ili waseme majengo 5 yamekamilika.Mkuu wa Wilaya alisimama kidete na kuwabana Halmashauri kuwa nawapa siku 3 mnionyeshe wapi mtajenga kituo cha Afya.Baada ya siku 3 walimwonyesha Mkuu wa Wilaya eneo jingine mbali na walilokuwa wamesema mwanzo tofauti ya majengo yaliyoachwa na wachina.
    Hali hiyo ilileta mtafaruku mkubwa sana.Ikumbukwe katika vita hizi zote Mkuu wa Wilaya hana sapoti kutoka popote kwa sababu anasimamia pesa za wavuja jasho zitumike katika maendeleo kusudiwa hivyo kwa kuwa amekata mirija ,anatafutwa na wahafidhina kila kona.

  • Mkuu wa Wilaya alipoingia madarakani aliwapa mbinu Halmashauri juu ya kuongeza mapato, ambapo baada ya hapo yalipanda sana kuanzia mwezi Oktoba mpaka February 2019.Baada ya hapo DC akaanza kusikia kuna watu wanaenda kuomba rushwa kwa wafanyabiashara ili wapate nafuu ya kodi inayotokana na Service Levy na Hotel Levy, baada ya taarifa hizo kama mkuu wa Ulinzi na usalama alifanya uchunguzi na kuchukua hatua, Ambapo alishauri Afisa Mapato abadilishwe aliyekuwa akijulikana kwa jina la Sylvester na kuwekwa mtu nwingine.Kumbe Sylvester alikuwa na mtandao mkubwa wa rushwa ndani ya Idara ya Uhasibu wakaanza mgomo wa chini kwa chini, baada ya DC kupata taarifa za kina kuhusu mtandao huo wa kifisadi, ndipo Mkuu wa Wilaya alitoa maagizo atolewe katika Idara hiyo lakini Mkurugenzi hakufanya hivyo mpaka hivi majuzi DC alipotoa maagizo tena kwa ukali sana, ndio Sylvester akatolewa.

  • Baada ya Mr. Sylvester kutolewa , akawekwa mtu anaitwa Ibrahim ambaye naye akawa anapokea rushwa na hali hiyo ikapelekea Mh DC kwa kushirikiana na Takukuru Mkoa wa Tabora waliweka mtego na alikamatwa na sasa tunavyoongea Afisa Mapato huyo ana kesi mahakamani na genge lake ndio hao wanamchafua DC huku wakijua kesi iko mahakamani na Dc ahusiki.

  • Mtandao huo una baadhi ya wakuu wa Idara ambapo yupo Mkuu mmoja wa Idara ambaye aliwahi kufanya kazi Mwanza ambaye ana uraia wa Kinyarwanda( tutamlipua kwa kumtaja jina muda ukifika) ambaye kwa kushirikiana na wafanyabiashara wachache na viongozi wa CCM wasiowaaminifu wamekuwa wakishirikiana kupambana na DC ili ashindwe kutekeleza Majukumu yake na kuzusha uongo mwingi.Kiongozi huyo wa CCM ni mjumbe wa Kamati ya Siasa katika Wilaya ya Tabora na Kiongozi mmoja wa CCM Mkoa wa Tabora wote hawa wamekuwa wakisambaza maneno ya kutia wafanyakazi hofu kumhusisha DC na viongozi wakubwa wa serikali nchini na chama cha mapinduzi taifa.

MAJIBU YA TUHUMA KATIKA ANDIKO LA Mwanamagongo na wenzake
  • Hakuna Dereva yeyote ambaye amekosana wala kutimuliwa na DC, huu ndio mwendelezo wa siasa chafu unaofanywa na genge nililolitaja katika Maelezo ya huko juu, kwa akili ya kawaida hakuna mtu anaweza gombana na Kuomba abadilishiwe madereva 15, maana Dc kuingia mwaka 2018, mwezi wa 9, hadi sasa ana mwaka mmoja na miezi kama 2, kwa akili ya kawaida maana kila wiki 3 alikuwa anaomba abadilishiwe Dereva ,huu ni uzandiki na uhuni, na kama wanasema kweli wawataje hao madereva 15

  • Hakuna mtumishi yeyote anayetukanwa wala kudhalilishwa ,Dc ni mwanasheria Kitaaluma anafahamu taratibu za utumishi wa umma ,toka Anafanya kazi wizara ya ardhi , hivyo huu uzushi ni mbinu zilezile za wabadhirifu kubanwa na kutaka kumchonganisha Dc na watumishi wenzake

  • Kwa wanaofanya kazi katika halmashauri wanatambua kabisa DC hana uwezo wa Kumwambia mhasibu , atoe pesa maana kuna taratibu zake ,kinachofanyika ni watu wachache ambao wamezoea kutumia pesa visivyo ndio maana wana hahaa kumchafua DC ,ambaye Anafanya makubwa katika wilaya ya tabora.
umekuja kujitetea,,,hope utajirekebisha....kila lakheri kwenye majukumu yako
 
Back
Top Bottom