Huu ndio ukweli kuhusu andiko linalomtuhumu DC wa Tabora Mjini, Komanya Kitwala kutokuwa na maelewano na watumishi

Nyasa Girl

Member
Jul 11, 2017
10
19
Ndugu wana JF

Kumetokea juzi andiko ambalo linamtuhumu Dc wa tabora mjini ,Mh. Komanya Kitwala kwa mambo mbalimbali , kiufupi hayo mambo ni ya kutunga na uzushi mkubwa ambao unazushwa na wanufaika wa ufisadi na watu waliozoea kufanya kazi kwa mazoea.

Uzi wa tuhuma huu hapa Mkuu wa Wilaya ya Tabora ndugu Erick Komanya Kitwala hana maelewano na mtumishi yeyote ndani ya wilaya anayoiongoza

UKWELI NI HUU HAPA
  • Mkuu wa Wilaya alipoingia madarakani baada ya kuteuliwa alikuta kuna zabuni ya shilingi bilioni 4.2 ujenzi wa barabara za kwa Nyembo, Transfoma, Kuya, Heri na Nyerere.Katika zabuni hiyo Halmashauri ilitaka kumpa mtu zabuni bila kufuata utaratibu wa zabuni wa kutangaza, ambapo Mkuu wa Wilaya aliingia kati na kuamuru itangazwe na hatimaye kuleta mvutano ambapo Halmashauri ilikataa kutangaza na hatimaye viongozi wa juu wakaingikia kati na zabuni ikatangazwa na hivyo yule mtu waliyemtaka Manispaa akakosa kazi hiyo na akapata mtu mwingine.

  • Mvutano huu ulikuwa baina ya madiwani walioko katika Kamati ya Fedha, Mkurugenzi na watu wa manunuzi dhidi ya DC.Baada ya vita hiyo ya DC kusimamia Utaratibu na kufuatwa, kukawa na vita ya chini kwa chini.Ambapo mwaka huu 2019, mwezi Februari , Makamu wa Rais alitembelea Tabora ambapo baadhi ya madiwani waliaandaa mpango wa kumchafua DC, sababu tu alizuia zabuni kutoka kiholela bila Utaratibu kwa msukumo wa madiwani, hivyo baadhi ya madiwani waliozoea kutumika na wafanyabiashara walichanga hela na kumpa Mzee mmoja aitwaye MALIFEDHA ili atumike kumchafua DC kwa makamu wa Rais, kuwa DC hafai, n.k , Bahati nzuri Makamu wa Rais Mama Samia, alipopewa tuhuma hizo aliwatuma watu wake wachunguze, na walipochunguza wakagundua kuwa ni njama na Mkuu wa Wilaya hana hatia bali ni chuki na majungu yanapikwa.

  • Baada ya uchunguzi na kupata taarifa sahihi, katika Vikao vya majumuisho ya ziara yake mkoa wa Tabora , aliwaambia waache majungu na pia kwenye mkutano wa nje aliwaambia watumishi wa serikali na viongozi wa kuchaguliwa wafanye kazi waache kuchafuana ( Rejea clip za ziara You tube). Pia alisisitiza akisema watu wa Tabora acheni majungu...Mnataka kuletewa malaika?

  • Wakati DC anaingia madarakani mwezi wa 9 mwaka jana 2018 alikuta Halmashauri inazo milioni 400 za ujenzi wa Kituo cha Afya cha Maili 5.Mpango uliokuwepo ni kutaka kuongeza majengo mawili ya nyumba za wachina waliyoyaacha baada ya mradi kukamilika ,nyumba walozokuwa wanakalia ziko Maili 5 , viongozi walitaka kutafuna pesa za majego mapya kwa kufanya replacement ya majengo ya wachina ili waseme majengo 5 yamekamilika.Mkuu wa Wilaya alisimama kidete na kuwabana Halmashauri kuwa nawapa siku 3 mnionyeshe wapi mtajenga kituo cha Afya.Baada ya siku 3 walimwonyesha Mkuu wa Wilaya eneo jingine mbali na walilokuwa wamesema mwanzo tofauti ya majengo yaliyoachwa na wachina.
    Hali hiyo ilileta mtafaruku mkubwa sana.Ikumbukwe katika vita hizi zote Mkuu wa Wilaya hana sapoti kutoka popote kwa sababu anasimamia pesa za wavuja jasho zitumike katika maendeleo kusudiwa hivyo kwa kuwa amekata mirija ,anatafutwa na wahafidhina kila kona.

  • Mkuu wa Wilaya alipoingia madarakani aliwapa mbinu Halmashauri juu ya kuongeza mapato, ambapo baada ya hapo yalipanda sana kuanzia mwezi Oktoba mpaka February 2019.Baada ya hapo DC akaanza kusikia kuna watu wanaenda kuomba rushwa kwa wafanyabiashara ili wapate nafuu ya kodi inayotokana na Service Levy na Hotel Levy, baada ya taarifa hizo kama mkuu wa Ulinzi na usalama alifanya uchunguzi na kuchukua hatua, Ambapo alishauri Afisa Mapato abadilishwe aliyekuwa akijulikana kwa jina la Sylvester na kuwekwa mtu nwingine.Kumbe Sylvester alikuwa na mtandao mkubwa wa rushwa ndani ya Idara ya Uhasibu wakaanza mgomo wa chini kwa chini, baada ya DC kupata taarifa za kina kuhusu mtandao huo wa kifisadi, ndipo Mkuu wa Wilaya alitoa maagizo atolewe katika Idara hiyo lakini Mkurugenzi hakufanya hivyo mpaka hivi majuzi DC alipotoa maagizo tena kwa ukali sana, ndio Sylvester akatolewa.

  • Baada ya Mr. Sylvester kutolewa , akawekwa mtu anaitwa Ibrahim ambaye naye akawa anapokea rushwa na hali hiyo ikapelekea Mh DC kwa kushirikiana na Takukuru Mkoa wa Tabora waliweka mtego na alikamatwa na sasa tunavyoongea Afisa Mapato huyo ana kesi mahakamani na genge lake ndio hao wanamchafua DC huku wakijua kesi iko mahakamani na Dc ahusiki.

  • Mtandao huo una baadhi ya wakuu wa Idara ambapo yupo Mkuu mmoja wa Idara ambaye aliwahi kufanya kazi Mwanza ambaye ana uraia wa Kinyarwanda( tutamlipua kwa kumtaja jina muda ukifika) ambaye kwa kushirikiana na wafanyabiashara wachache na viongozi wa CCM wasiowaaminifu wamekuwa wakishirikiana kupambana na DC ili ashindwe kutekeleza Majukumu yake na kuzusha uongo mwingi.Kiongozi huyo wa CCM ni mjumbe wa Kamati ya Siasa katika Wilaya ya Tabora na Kiongozi mmoja wa CCM Mkoa wa Tabora wote hawa wamekuwa wakisambaza maneno ya kutia wafanyakazi hofu kumhusisha DC na viongozi wakubwa wa serikali nchini na chama cha mapinduzi taifa.

MAJIBU YA TUHUMA KATIKA ANDIKO LA Mwanamagongo na wenzake
  • Hakuna Dereva yeyote ambaye amekosana wala kutimuliwa na DC, huu ndio mwendelezo wa siasa chafu unaofanywa na genge nililolitaja katika Maelezo ya huko juu, kwa akili ya kawaida hakuna mtu anaweza gombana na Kuomba abadilishiwe madereva 15, maana Dc kuingia mwaka 2018, mwezi wa 9, hadi sasa ana mwaka mmoja na miezi kama 2, kwa akili ya kawaida maana kila wiki 3 alikuwa anaomba abadilishiwe Dereva ,huu ni uzandiki na uhuni, na kama wanasema kweli wawataje hao madereva 15

  • Hakuna mtumishi yeyote anayetukanwa wala kudhalilishwa ,Dc ni mwanasheria Kitaaluma anafahamu taratibu za utumishi wa umma ,toka Anafanya kazi wizara ya ardhi , hivyo huu uzushi ni mbinu zilezile za wabadhirifu kubanwa na kutaka kumchonganisha Dc na watumishi wenzake

  • Kwa wanaofanya kazi katika halmashauri wanatambua kabisa DC hana uwezo wa Kumwambia mhasibu , atoe pesa maana kuna taratibu zake ,kinachofanyika ni watu wachache ambao wamezoea kutumia pesa visivyo ndio maana wana hahaa kumchafua DC ,ambaye Anafanya makubwa katika wilaya ya tabora.
 
Tunatumia muda mwingi na rasilimali nyingi kukanyagana visigino bila sababu, dawa yake Magufuli hamishia kazi zote za ujenzi TANROADS, huku chini watu wanarumbana sana na fedha inaishia kwa madiwani wasio na taaluma yoyote, usanii mwingi, matumizi ya pesa mabaya wananchi wanataabika
 
Kanya acha kuwadanganya wanajamii forums,ulichofanya ni prejection defensive mechanism,unataka kuuaminisha umma kuwa Mkurugenze ni mwizi,madiwani ni wezi wakuu wa Idara ni wezi na watumishi ni wezi,bali wewe ndiye mtakatifu kiasi cha kila kiongozi Tabora mjini kukuchukia wewe.

Ukweli unabaki palepale kuhusu tiha za mahusiano,haiwezekani watu wote wawe wabaya ila wewe peke yako ndiye uwe mwema.

Maana yake unakiri kwamba huna mahusiano mema na wenzako.

Mkurugenzi inaemsimanga kawa mkurugenzi wewe ukiwa bado shule ya msingi,maana ni miongoni mwa wakurugenzi wazoefu na waliodu kwa miaka mingi sana,hajahudu Tabora pekee bali kahudumu halmashauri nyingi za Tanzania,watanzania wengi wanaujua Uadilifu wa Bosco Ndugulu,ni kwa uadilifu huo ndio maana kadumu kwenye hiyo nafasi kwa miaka mingi,sasa wewe limbukeni wa madaraka unaibuka na kuanza kuchafua watu wenye ligacy katika nchi?

Hivi halmashauri gani inaweza kigawa tenda bila kutangaza?au unadhani watanzania niwajinga?

Hoja ya kuhusu dereva,waambie watu ilikuweje ukawa hutumii gari yako kama Mkuu wa wilaya?

Kwanini ulikuwa ukitumia gari za TANROAD,mara TUWASA wakati wewe unagari yako.kwanini.hutaki kusema ukweli,yule Dereva mzee wa umri wa Baba yako uliekuwa unamtukana kama mwanao wa kimzaa mpaka akaamua kupaki gari unadhani watu hawakujua?

Unasema madereva hawajafika 15, jitomeze utuambie mpaka sasa unae dereva wangapi tangu umefika uhudumu ndani ya wilaya.

Kama unakiri huelewani na madiwani,huelewani na Mkurugenzi,huelewani na wakuu wa Idara,huelewani na watumishi,na ukienda mbali ukakiri huelewani na Viongozi wa CCM ,sasa hayo maendeleo ya wananchi utayasukuma vipi kama watekelezaji na watendaji wa mipango ya serikali ni adui zako?

Huoni kama unakosa uhalali wa kisiasa kushawishi watumishi wajitume kwakuwa huimbi wimbo mmoja na wenzako?

Huoni kama ni wakati muafaka kujizuru na kwenda kuendelea na kampeni za ubunge kule kwenu Magu?
 
Halafu hilo la zabuni ya bilioni 4 ujenzi wa Barabara ni uongo mtupu kwa sababu barabara hazisimamiwi na halmashauri kuna agency inaitwa TARURA madiwani hawahusiki kwa zabuni wala kupitisha chochote wala mkurugenzi wa halmashauri .

Kajipange tena bwana komanya hapa umetudanganya.
 
Kwahiyo DC ndo kakutuma? Au uneamua tu kuleta ukweli?
Hebu tuambie uko kitengo gani mpaka ukapata ukweli wote huu?
 
Back
Top Bottom