Huu ndio ukweli; ajira zipo ila Serikali haina pesa za kuajiri

Huu ndio ukweli ajira zipo ila serikali haina pesa za kuajiri na kulipa mishahara.

Je, tufanyeje ili kupata fedha za kuajiri na kulipa mishahara?

Nini maoni yako katika hili.

Wewe ungekua ndio kiongozi ungefanyeje ili kupata fedha za kuajiri na kuwalipa mishahara hao ambao utawaajiri?
Ajira zipo mashambani kama kikiboreshwa kilimo
 
Serikali tuchimbe madini tuuze Kisha zile pesa ziajiri..na gesi na umeme n.k na vyote
 
Huu ndio ukweli ajira zipo ila serikali haina pesa za kuajiri na kulipa mishahara.

Je, tufanyeje ili kupata fedha za kuajiri na kulipa mishahara?

Nini maoni yako katika hili.

Wewe ungekua ndio kiongozi ungefanyeje ili kupata fedha za kuajiri na kuwalipa mishahara hao ambao utawaajiri?
Hapo hakuna namna zaidi ya kuongeza usimamizi hasa kwenye maliasili kama vile sekta ya utalii na madini..
 
Kama hakuna uzalishaji hakuna pesa itapatikana ya kuajiri..

Kuna watu huwa wanasema eti degree zimetosha kitu ambacho si kweli, uhitaji wa wataalam kwenye sekta mbalimbali bado ni mkubwa sana.

Nchi bado ina uchumi mdogo ila cha ajabu vipaumbele tumeweka kwenye mambo yasiyo na tija. Kifupi bado hakuna viongozi wanaowaza kutukwamua toka hapa tulipo.

Ukiangalia hakuna miradi yeyote ya maana inayoanzishwa ya kuweza kutoa ajira, kama bandari ya Bagamoyo tu ambao ni mradi mkubwa sana ambao kwa namna moja au nyingine ungeleta ajira za kutosha, bado viongozi hao hao wakaupiga vita.
Kuna umuhimu mkubwa pia wa kusisistiza na kuweka mkazo wa proportionality ya waajiriwa toka nje , wazawa wapewe kipaumbele , hawa makanjanja makanjibai waliojazana humo na kukaba nafasi za wazawa , Kwanza hawalipi income tax na ni watoa rushwa wengi hawana qualifications wala expertise za kuhold nafasi za kazi , kick them out , waajiriwe wazawa .
 
Waajiri bhanaaa, watumishi kazi zimewazidia tangu mwendazake afanye redunduncy bila kufanya replacement ya maana plus wanaoendelea kustaafu...
 
Back
Top Bottom